Week Hot newz

البابا فرنسيس يستقبل رئيس جمهورية قبرص السيد نيكوس أناستاسيادس



استقبل البابا فرنسيس هذا السبت في القصر الرسولي بالفاتيكان رئيس جمهورية قبرص السيد نيكوس أناستاسيادس الذي اجتمع لاحقا بأمين سر دولة حاضرة الفاتيكان المطران بيترو بارولين وأمين سر الدولة للعلاقات مع الدول المطران دومينيك مامبرتي. وجاء في بيان نشرته دار الصحافة التابعة للكرسي الرسولي أنه تم التطرق خلال المحادثات الودية إلى العلاقات الجيدة القائمة بين الكرسي الرسولي وجمهورية قبرص، إضافة لبعض المسائل ذات الاهتمام المشترك، كالدور الإيجابي للديانة في المجتمع وحماية الحق في الحرية الدينية. وأضاف البيان الصادر عن دار الصحافة الفاتيكانية أنه تمت الإشارة بارتياح لاستئناف المحادثات الهادفة إلى حل متقاسم لتخطي الوضع الحالي للجزيرة، وتم التعبير أيضا عن القلق إزاء النزاعات وغياب الاستقرار السياسي في منطقة الشرق الأدنى والأوسط، ما يسبب آلاما خطيرة للسكان المدنيين، مع الأمل بأن تتمكن الجماعات المسيحية في البلدان المختلفة من مواصلة تقديم إسهامها لبناء مستقبل من الخير المادي والروحي.

هذا واستقبل البابا فرنسيس هذا السبت في الفاتيكان بطريرك الروم الملكيين الكاثوليك صاحب الغبطة غريغوريوس الثالث لحام ورئيس أساقفة ساو باولو في البرازيل، الكاردينال أوديلو شيرير.

Raslimali ya nchi itumike kwa ajili ya mafao ya wengi!


Kardinali John Onaiyekan wa Jimbo kuu la Abuja, Nigeria, hivi karibuni wakati wa Maadhimisho ya Ibada ya Misa takatifu katika kumbu kumbu ya Jubilee ya Miaka 70 tangu kuzinduliwa kwa Kanisa la Bikira Maria Malkia wa Nigeria, Jimbo kuu la Abuja amewataka viongozi wa Serikali na kutoka katika sekta ya watu binafsi kutumia vyema rasilimali ya nchi kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya wananchi wote wa Nigeria.

Kardinali Onaiyekan anasema kwamba, Mwenyezi Mungu ameikirimia Nigeria utajiri mkubwa wa maliasili ambayo kimsingi inapaswa kutumiwa kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya wananchi wote wa Nigeria bila upendeleo, kama kielelezo cha utekelezaji wa misingi ya haki, amani na maendeleo endelevu. Huu unaweza kuwa ni mchango mkubwa katika kukabiliana na changamoto mbali mbali zinazoendelea kujitokeza nchini Nigeria: ukosefu wa amani na utulivu unaoweza kuchangiwa kutokana na umaskini;

Wazee, hazina ya familia na Jamii....


Tunaendelea kujielimisha na masuala mbalimbali yanayohusiana na maisha mchanganyiko, tukiwa ndani ya familia ambamo kwa kawaida tuna baba , mama, watoto na wazee na wagonjwa. Wanasayansi wanasema kuzeeka ni suala la maendeleo kimaisha. Wazee ni chemchemi ya maisha

HISTORIA YA WAFRANSISKO


1.1. NDUGU WADOGO KUPAMBANA HADI KUTENGANISHWA (1226-1517)

 
1.1.1. MWANZO WA MAPAMBANO (1226-1318)
 
Mt. Fransisko alipokuwa hai alisongwa na kundi la Watumishi na wasomi wa utawa wake, likisaidiwa na viongozi wa juu wa Kanisa, ili alegeze masharti ya ufukara na kulinganisha zaidi shirika lake na yale ya zamani. Kwa karama yake ya pekee aliweza kukabili upinzani huo wote. Juhudi yake ya mwisho ya kuzuia shirika lisipotoke ni wasia aliouandika ili kusisitiza msimamo wake, kudai kanuni yake isifafanuliwe, pamoja na kukataza wanashirika wasimuombe Papa hati yoyote. Alipokufa utawa ukabaki mikononi mwa Watumishi hao, wakiongozwa na nd. Elia Bombarone, Mkuu wa shirika miaka 1221-1227, halafu 1232-1239.
Katikati ya hivyo vipindi vyake viwili vya uongozi, Mtumishi mkuu alikuwa nd. Yohane Parenti. Chini yake yalizuka mabishano makali kati ya walioshikilia wasia huo na wale waliotaka shirika lishindane na mashirika mengine. Yeye na Watumishi wengine wakadhani utatuzi unaweza kutokea kwa viongozi wa Kanisa tu. Akipokea ombi lao, Gregori IX (1227-1241)

Ombeeni amani Barani Afrika!



Vita, kinzani na migogoro inayoendelea kujitokeza Barani Afrika imekuwa ni chanzo kikubwa cha taabu na mahangaiko ya watu wasiokuwa na hatia. Kuna watu wanalazimika kuyakimbia makazi yao, wanateseka kwa njaa na magonjwa kutokana na ukosefu wa amani na utulivu.

Baba Mtakatifu Francisko kwa kuguswa na mahangaiko ya wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, anawaalika watumiaji wa mitandao ya kijamii, kumuunga mkono katika kusali kwa ajili ya kuombea amani na utulivu huko Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati na Sudan ya Kusini.

Rais wa Cyprus akutana na Papa!



Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi, tarehe 15 Februari 2014 amekutana na kuzungumza na Rais Nicos Anastasiades ambaye baadaye alikutana na Kardinali mteule Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameambata na Askofu mkuu Dominique Mamberti, Katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican.

Viongozi hawa wawili wamejadili pamoja na mambo mengine kuhusu uhusiano kati ya Cyprus na Vatican; mchango mkubwa unaotolewa na Kanisa Katoliki nchini humo pamoja na umuhimu wa kuendelea kusimama kidete kulinda na kutetea uhuru wa kidini. Kwa pamoja wameonesha matumaini makubwa baada ya kuanza tena majadiliano ya kisiasa yanayopania kupata ufumbuzi wa kudumu kutokana na hali ngumu inayoendelea nchini Cyprus kwa sasa.

Baba Mtakatifu na mgeni wake wameangalia pia kinzani, migogoro na vita huko Mashariki ya Kati ambayo imesababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao. Ni matumaini ya viongozi hawa kwamba, Jumuiya za Kikristo huko Mashariki ya kati zitachangia katika ustawi na maendeleo ya Ukanda huu.