Week Hot newz

Kesho ni Basetsana na Tanzanite

  1. Kila mmoja wetu anafahamu kwamba Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Rolihlahla Mandela
    amefariki dunia jana December 6, 2013. Rais JM Kikwete pia akatangaza siku 3 za maombolezo kuanzia leo Dec 6 mpaka Dec 8 na bendera ya Tanzania itapepea nusu mlingoti siku zote hizo.
    Lakini kesho jumamosi Dec 7, 2013 ile timu yetu ya Wadada iliyowabugiza Msumbiji bao KUMI BILA uwanja wa Taifa inatakiwa kucheza na wadada wenzao wa Afrika Kusini (Basetsana) kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kwa wasichana wenye umri chini ya miaka 20 katika Uwanja wa Taifa.

KOMBE LA DUNIA || BRAZIL 2014 MAKUNDI KAMILI.



Makundi yamejulikana , na pia imejulikana nani atamenyana na nani.
Hapana shaka wapenzi wa soka barani Afrika pamoja na kuomboleza kifo cha Nelson Mandela wamekuwa wanafuatilia Droo ya kombe la dunia kufahamu nani wapinzani wa timu tano zinazowakilisha bara hilo.
Cameroon wamejikuta katika kundi gumu la A pamoja na wenyeji Brazil, Mexico na Croatia.
Mabingwa watetezi Uhispania watakuwa katika kundi B pamoja na Netherlands waliokutana nayo fainali kombe lililopita, na timu zingine ni Chile na Australia.
Dua ya Ivory Coast ya kuepuka kundi gumu sana wakati huu inaonekana imesikika, wako katika kundi C pamoja na Colomboa, Japan na Ugiriki.England watakuwa na kibarua kigumu kwenye kundi D ambapo wapinzani wao ni Italia, Uruguay na Costa Rica.
Kwenye kundi E Ufaransa inacheka usiku huu kwani imepangwa pamoja na Uswizi, Ecuador na Honduras.Mabingwa wa Afrika Nigeria wako katika kundi F pamoja na Argentina Iran na Bosnia Harcegovinia, ambayo inashiriki kombe la dunia mara ya kwanza.
Ghana ndiyo inayoonekana kuwa matatizoni miongoni mwa timu za Afrika. Wamejikuta katika kundi G ambapo watapamaba na na Ujerumani, Marekani na Ureno.Timu ya tano ya Afrika Algeria itakuwa kwenye kundi H na wapinzani hapo ni Ubelgji, Korea Kusini na Urusi.



WORLD CUP Afrika Kusini mafanikio ya Mandela


Wanamichezo pia wamemkumbuka Mandela
Wanamichezo mashuhuri, duniani wametoa rambi rambi zao kwa hayati Nelson Mandela, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 95.
Mohamedi Ali
alisema: "Maisha ya Mandela yalikuwa na maana kubwa kwa dunia nzima , kwake mwenyewe, kwa taifa lake na dunia nzima.
Alitufanya sisi kugundua kua ni muhimu kumjali mwenzake na kuwa sisi ni ndugu licha ya rangi zetu.''
Mwanasoka mashuhuri Bofya Pele naye amesema "Mandela alikuwa mtu mwenye ushawishi mkubwa sana maishani mwake. Ni shujaa wangu.’’
Mwanamasumbwi Bofya Ali aliongeza kusema kua, atamkumbuka Mandela sana kwa kuwa mtu mwenye roho safi na alichukizwa sana na mambo ya ubaguzi wa rangi pamoja chuki na uhasama.
Aliwatia moyo wengine kufikia mambo waliyoyaona kama yasiyowezekana.''
"Bofya Ali amesema kua Mandela alifunza watu umuhimu wa kuwasamehe wenzao, na leo ameweza kuwa huru.’’
Bofya Tiger Woods, naye ambaye ni mchezaji golfu mashuhuri zaidi duniani, alisema daima atamkumbuka Mandela.
Aliyekuwa nahodha wa timu ya Uingereza, Bofya David Beckham alisema kuwa anamlilia sana Mandela na kuwa yuko pamoja na familia yake. ''Tumepoteza mtu muhimu sana na shujaa wetu,’’ Alisema Beckham.
Naye mkuu wa shirikisho la soka duniani FIFA, Bofya Sepp Blatter, amesema kuwa anaomboleza sana na anahisi uchungu mwingi kufuatia kifo cha Mandela.

Nelson Mandela Histori 1918-2013

Miaka ya Mapema

1952

Rolihlahla Mandela, mwanawe chifu, alizaliwa katika kijiji kimoja kiitwacho, Mvezo katika mkoa wa Eastern Cape nchini Afrika Kusini tarehe 18 Julai mwaka 1918. Alikuwa mtu wa kwanza katika familia yake kwenda shule. Mwalimu ambaye hata hangeweza kutaja jina lake vyema, alizoea kumuita Nelson. Alitoroka mjini Johannesburg mwaka 1941 ili kuepuka kulazimishwa kuoa mapema. Alikutana na Walter Sisulu aliyemsaidia kupata kazi katika kampuni ya ya Witkin Sidelsky na Eidelma. Pia alijiunga na chama cha (ANC)


Kesi ya Uhaini

1956

Mandela alifuzu kama wakili na kuanzisha kampuni ya kwanza ya sheria inayomilikiwa na mtu mweusi mwaka 1952 na kuiendesha kwa ushirikiano na Oliver Tambo, na kutoa huduma za kisheria kwa wale ambao walikosa uwakilishi. Akihofiwa kupigwa marufuku na serikali ya ubaguzi wa rangi, ANC ilimtaka Mandela kuhakikisha kuwa chama hicho kinaweza kuendesha harakati zake kimya kimya. Alikamatwa mwaka 1956 na kufunguliwa mashtaka ya uhaini yeye pamoja na wenzake 155. Baada ya kesi yake iliyochukua miaka minne, ilitupiliwa mbali . Mnamo mwaka 1958, Mandela alimuoa Winnie Madikizela.

Huru hatimaye

1990

Jamii ya kimataifa iliiwekea vikwazo zaidi serikali ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini. Vikwazo vya kwanza viliwekwa mwaka 1967.Shinikizo zilizaa matunda na mnamo mwaka 1990, rais FW De Klerk akakiondolea marufuku chama cha ANC. Tarehe 11 Februari, Mandela aliachiliwa baada ya miaka 27 jela. Umati wa watu ulimshangilia huku yeye pamoja na mkewe wakiondoka sehemu ya jela. Katika mkutano wa kwanza wa chama cha ANC mwaka uliofuata, Mandela alichaguliwa kama kiongozi wa chama .Mazungumzo yakaanza ya kuunda serikali ya pamoja ya waafrika weusi na wazungu.

Tuzo ya amani ya Nobel

1993

Mnamo mwaka 1993, Mandela na rais wa nchi hiyo wakati huo, walituzwa tuzo ya amani ya Nobel kwa juhudi za kuleta uthabiti Afrika Kusini. Akikubali tuzo hiyo, Mandela alisema kuwa '' tutafanya kila tuwezalo kuweza kuleta mageuzi duniani.''

Rais mpya

1994

Mnamo mwaka1994,kwa mara ya kwanza katika historia ya Afrika Kusini, watu wa rangi zote walipiga kura katika uchaguzi huru na wa kidemokrasia. Mandela alichaguliwa. Akihutubia umma, katika sherehe ya kuapishwa kwake, tarehe 10 mwezi Mei, mwaka 1994, alisema: "uhuru utawale, Mungu aibariki Afrika!'' Tatizo lake kubwa lilikuwa ukosefu wa nyumba za kutosha kwa watu maskini na mitaa ya mabanda iliendelea kuongezeka.Thabo Mbeki alichukua uongozi wa nchi huku Mandela akiuza sera za nchi hiyo kimataifa.


Akitoka Robbben

1995

Kuadhimisha miaka mitano baada ya kuachiliwa kwake, Nelson Mandela alizuru kisiwa cha Robben mwezi Februari mwaka 1995 alikozuiliwa kwa miaka 18. Ziara yake ilikuwa mwaka 1956 mwezi Februari pamoja na wafungwa wenzake waliowahi kufungwa kisiwani humo na kufanya kazi ngumu. Mapafu ya Mandela yanasemekana kuathirika alipokuwa anafanya kazi katika machimbo ya mawe.

Usiniite''

2004

Thabo Mbeki alichukua mamlaka kutoka kwa Mandela kama kiongozi wa chama tawala ANC na hata kushinda uchaguzi wa mwaka 1999.Mandela alimuoa Graca Machel, mjane wa aliyekuwa rais wa Msumbiji, akiwa na miaka 80. Aligunduliwa kuwa na saratani ya Tezi Kibofu na hivyo kuanza matibabu.Mnamo mwaka 2004, alitangaza kujiuzulu, akisema kuwa anataka maisha ya kimya nyumbani kwake na familia yake. Kwa mzaha aliwaambia wandishi wa habari wasimpigie simu.

Sherehe ya siku ya kuzaliwa kwake

2008

Wanamuziki, waigizaji na wanasiasa waliungana na Mandela katika sherehe kubwa uwanja wa Hyde Park mjini London kusherehekea miaka 90 ya kuzaliwa kwake. Akiongea na wale waliofika, aliwaambia, ''ni wakati kwa kizazi kipya kuchukua uongozi, kibarua kwenu sasa.''

Kuugua

2010

Mandela aliweza kuonekana hadharani mara kadhaa baada ya kustaafu. Ingawa alionekana katika sherehe ya kukamilika kwa dimba la kombe la dunia mwaka 2010 nchini humo. Januari mwaka 2011, alilazwa hospitalini kwa ukaguzi maalum, huku serikali ikiwakumbusha watu kuwa aliwahi kupata matatizo ya kupumua. Alipokea matibabu ya ugonjwa wa mapafu mwaka 2012 na pia mwaka 2013 .