Week Hot newz

Teknolojia hii pia izingatie viwango vya ubora


Katika kuimarisha mahusiano ya kimataifa, kuimarika kwa uchumi wa nchi, uwekezaji na rasilimali za nchi nk. vyote kwa umoja wake ni biashara, hakuna ajenda itakayozungumzika karne hii kama haina maslahi ya kibiashara.

Wengine hudhani biashara inaweza kuanzishwa tu kiholela bila kuweka vigezo vinavyozingatia ubora wa bidhaa husika, wakati mwingine kutokana na unyeti wa teknolojia mpya, wachache huchukulia kama ni fursa ya kuingiza teknolojia hiyo sokoni bila kuangalia kama inakidhi viwango vya ubora.

Katika hatua za kuimarisha bidhaa zinazokubalika, Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wiki hii lilitangaza uwepo wa vipande vya umemejua ambavyo havina ubora kwa soko la ndani, na TBS tayari limetoa tahadhari kwa wananchi kuwa makini wanaponunua vifaa vya kutengenezea mfumo huo wa umemejua.

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Umma cha TBS, Roida Andusamile alisema kumepatikana taarifa za uchunguzi wa maabara uliofanywa kwa sampuli zaidi ya 10 za vipande vya umemejua ambavyo alisema vilichukuliwa vikiwa tayari madukani vikiuzwa.

Roida alisema iligundulika kuwa sampuli zote za vipande vya umemejua vilivyochukuliwa baada ya kupimwa havikuwa katika ubora unaokubalika kisheria.

Hilo ni tatizo kubwa, linahitaji mamlaka nyingine zisaidiane na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kupitia bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa kwa teknolojia mpya ya kisayansi ili kuthibitisha kuwa ni salama na zinakuwa katika ubora unaokubalika.

Zipo hasara kubwa mbili zinazoweza kutokea katika utumiaji wa bidhaa hafifu kama hivyo vipande husika vya umemejua, kwanza hitilafu ya umeme unaozalishwa na vipande hivyo unaweza kuathiri mfumo wa umeme unaozalishwa, na pili ni hasara ya fedha kwa kununua vipande hivyo visivyo na ubora.

Teknolojia ya kuzalisha umeme kutumia vipande vya umemejua imekua kwa haraka katika kipindi cha uhaba mkubwa wa umeme ambao ulisababisha kuwepo kwa mgawo wa umeme nchini.

Baadhi ya watu wakaamua kutumia njia mbadala ya kupata umeme, matokeo yake ni kubuni na kutengeneza vipande vya umemejua visivyo na ubora katika soko la ndani.

Hata hivyo TBS iligundua uwepo wa vipande hivyo baada ya kupewa malalamiko na watumiaji wa umemejua wakaamua kushirikiana na Taasisi ya Nishati Jadidifu (TAREA).

Baada ya kupata taarifa hizo, Roida Andusamile alisema maofisa wa wao pamoja na TAREA walishirikiana pamoja na kufanya manunuzi maalum kwenye maduka mbalimbali ya vifaa hivyo yaliyoko Kariakoo.

Roida anasema manunuzi waliyafaya kwenye mitaa ya Msimbazi na Kongo pamoja na eneo la Keko-Mwanga na kupata sampuli ambazo baada ya kuzipima wakagundua ziko chini ya viwango vya ubora.

Roida alisisitiza kuwa hata wataalam waliofanya kazi ya kuvipima vipande hivyo, waligundua uwepo wa kasoro nyingi ambazo zilisababisha vifaa hivyo viwekwe katika kundi la bidhaa zilizo chini ya viwango vya ubora.

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti Ubora cha TBS, Ashura Kilewela alitaja maduka ambako vifaa hivyo vilinunuliwa kuwa ni Keoali Power &Equipment Co Limited, Regal Solar Limited na duka la Nishati Electronics Limited.

Kilewela alisema walichukua hatua zaidi kwa kuzuia vipande 1,321 vya umemejua visiuzwe kutoka dula la Regal Solar, na pia vipande 164 kutoka duka la Nishati Electronics kutokana na kutiliwa shaka ya ubora wake, na baadaye ilithibitika kuwa vipande hivyo ni kweli vilikuwa havina ubora.

Tunaamini kuwa jitihada za kutambua bidhaa ‘feki’ zinazoingia sokoni zitategemea ushirikiano kutoka kwa walaji watakaotoa taarifa kwa mamlaka husika kama TBS ili wao waweze kuchukua hatua stahiki.

Katika kadhia hiyo, Katibu Mtendaji wa TAREA, Mathew Matimbwi alisema kulikuwepo na kasoro nyingine katika vipande hivyo ambazo ni seli za vipande hivyo kuwa na rangi mbili badala ya moja na pia hazikuandikwa nchi zilikotengenezwa.

Maoni: 0715-047304 au owdenkyambile@gmail.com
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

Daily Reading for Sunday, September 6th, 2015


Reading 1, Isaiah 35:4-7

4 and say to the faint-hearted, 'Be strong! Do not be afraid. Here is your God, vengeance is coming, divine retribution; he is coming to save you.'
5 Then the eyes of the blind will be opened, the ears of the deaf unsealed,
6 then the lame will leap like a deer and the tongue of the dumb sing for joy; for water will gush in the desert and streams in the wastelands,
7 the parched ground will become a marsh and the thirsty land springs of water; the lairs where the jackals used to live will become plots of reed and papyrus.

Responsorial Psalm, Psalms 146:7, 8-9, 9-10

7 gives justice to the oppressed, gives food to the hungry; Yahweh sets prisoners free.
8 Yahweh gives sight to the blind, lifts up those who are bowed down.
9 Yahweh protects the stranger, he sustains the orphan and the widow. Yahweh loves the upright,but he frustrates the wicked.
10 Yahweh reigns for ever, your God, Zion, from age to age.

Gospel, Mark 7:31-37

31 Returning from the territory of Tyre, he went by way of Sidon towards the Lake of Galilee, right through the Decapolis territory.
32 And they brought him a deaf man who had an impediment in his speech; and they asked him to lay his hand on him.
33 He took him aside to be by themselves, away from the crowd, put his fingers into the man's ears and touched his tongue with spittle.
34 Then looking up to heaven he sighed; and he said to him, 'Ephphatha,' that is, 'Be opened.'
35 And his ears were opened, and at once the impediment of his tongue was loosened and he spoke clearly.
36 And Jesus ordered them to tell no one about it, but the more he insisted, the more widely they proclaimed it.
37 Their admiration was unbounded, and they said, 'Everything he does is good, he makes the deaf hear and the dumb speak.'

Reading 2, James 2:1-5

1 My brothers, do not let class distinction enter into your faith in Jesus Christ, our glorified Lord.
2 Now suppose a man comes into your synagogue, well-dressed and with a gold ring on, and at the same time a poor man comes in, in shabby clothes,
3 and you take notice of the well-dressed man, and say, 'Come this way to the best seats'; then you tell the poor man, 'Stand over there' or 'You can sit on the floor by my foot-rest.'
4 In making this distinction among yourselves have you not used a corrupt standard?
5 Listen, my dear brothers: it was those who were poor according to the world that God chose, to be rich in faith and to be the heirs to the kingdom which he promised to those who love him.

St. Eleutherius

Short Cuts
Image of St. Eleutherius

Facts

Feastday: September 6
Death: 585

A wonderful simplicity and spirit of compunction were the distinguishing virtues of this holy man. He was chosen abbot of St. Mark's near Spoleto, and favored by God with the gift of miracles. A child who was possessed by the devil, being delivered by being educated in his monastery, the Abbot said one day: "Since the child is among the servants of God, the devil dares not approach him." These words seemed to savor of vanity, and thereupon the devil again entered and tormented the child.
The Abbot humbly confessed his fault, and fasted and prayed with his whole community till the child was again freed from the tyranny of the fiend. St. Gregory, the Great, not being able to fast on Easter-eve on account of extreme weakness, engaged this Saint to go with him to the church of St. Andrew's and offer up his prayers to God for his health, that he might join the faithful in that solemn practice of penance.
Eleutherius prayed with many tears, and the Pope, coming out of the church, found that he was enabled to perform the fast as he desired. It is also said that St. Eleutherius raised a dead man to life. Resigning his abbacy, he died in St. Andrew's monastery in Rome about the year 585.

Ndoa kadiri ya mpango wa Mungu ni kati ya Bwana na Bibi na wala si vinginevyo!

Kanisa linasadiki na kufundisha kwamba, Mwenyezi Mungu ambaye ni asili na kiini cha upendo amemuumba mtu kwa upendo na amemwita kupenda. Kwa kuumba mwanaume na mwanamke, aliwaita katika Ndoa kuwa na umoja wa dhati wa maisha na upendo kati yao, ndiyo maana si wawili tena, bali wamekuwa ni mwili mmoja. Mwenyezi Mungu amewabariki ili wazae na kuongezeka. Mafundisho ya Kanisa kuhusu ndoa yanaweza yasiwafuraishe baadhi ya watu ndani ya jamii lakini yataendelea kubaki jinsi yalivyo. Huu ni mkazo ambao umetolewa hivi karibuni na Kardinali John Onaiyekan, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Abuja, Nigeria wakati alipokuwa anatembelea Jimbo Katoliki la Makurdi. Itakumbukwa kwamba, wakati wa ziara yake ya kikazi Barani Afrika hivi karibuni, Rais Barack Obama wa Marekani akiwa nchini Kenya pamoja na mambo mengine aliitaka Serikali ya Kenya kuheshimu uhuru wa watu wanaoshabikia ndoa za watu wa jinsia moja na kamwe wasibaguliwe. Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya alijibu na kusema, ndoa za watu wa jinsia moja si kipaumbele cha Serikali ya Kenya.
Msimamo huu wa Rais Barack Obama umechafua mawazo ya wanachi wengi Barani Afrika kwa kusema kwamba, huu si utamaduni wa kiafrika na wala si kielelezo cha haki msingi za binadamu. Kardinali Onayekan anasema, Kanisa litaendelea kutangaza kweli na shuhuda za Kiinjili kwa watu wa mataifa, hata kama kumong’onyoka kwa misingi ya maadili na utu wema kunaonekana kuwa ni haki binafsi.
Kardinali Onayekani anasikitika kusema kwamba, mambo kama ndoa za watu wa jinsia moja yanaonekana kuwa ni mambo ya kawaida, kiasi hata cha kutungiwa na kushabikiwa na sheria. Hata kama yamekubalika katika baadhi ya nchi si kweli kwamba ni matendo ya haki. Hakuna ndoa ya kweli kadiri ya mpango wa Mungu kati ya watu wa jinsia moja.
Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican kwa msaada wa CISA.