Week Hot newz

Maaskofu Ufilipino, wametoa wito wa Novena.


Maaskofu Katoliki wa Ufilipino, wametoa wito wa Novena, sala na fadhila, kwa waathirika na familia zilizopigwa vikali na maafa ya kimbunga kilichopita hivi karibuni na kuua mamia ya watu na kuharibu mali nyingi, zikiwemo nyumba. 


Mosinyori Pedro Quitorio , Mkurugenzi wa vyombo vya habari katika Baraza la Maaskofu Katoliki ya Philippines , alisema fedha zitakazo tolewa wakati wa kipindi cha Novena , iliyoanza Jumanne 12 na

Kwaheriii Dk. Sengondo Mvungi







Papa atembelea Ikulu ya Italia - "Quirinale"

Baba Mtakatifu Francisko Alhamis hii 14.11.2014 majira ya saa nne, kwa mara ya kwanza tangu kuwa Papa mwezi March mwaka huu, alifanya ziara rasmi, kumtembelea Rais wa Italia, Mheshimiwa Giorgio Napolitano, aliyekuwa akimsubiri katika jengo la Ikulu la Qiurinale. Papa amefanya ziara hii Ikulu kama kulipa fadhila kwa Rais Giorgio ambaye alimtembelea Papa June 8, mwaka huu. Papa Francisko ametembelea makazi haya ya Rais wa Italia, ya Quirinale, ambayo awali yalikuwa ni makazi ya Papa kwa karne nyingi hadi 1870.


Baada ya ukimya wa miaka mingi, ziara za Papa kutembelea Quirinale, zilianzishwa mwaka1939 na Papa Pius X11 alipomtembea Mfalme wa Italy Emmanuel 11 aliyekuwa akiishi katika jengo hilo. Na Mapapa waliofuatia wakaiga pia utamaduni huu wa kutembelea Ikulu wa Italia kama ishara ya mahusiano mazuri.