MOROGORO,TANZANIA.
MSANII wa bongo fleva na mkali wa kurap kwa lugha 31 Batarokota, amesema tangu alipofariki mke wake mpendwa mwaka 2005 kwa ajali ya gari kugonga treni, amesema tangu 2006 hana mpango wa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.
Msanii huyo mwenye umri wa miaka 42, amedai hana
sababu ya kuisherehekea siku hiyo kwa kuwa atakuwa na machungu ya
kumkumbuka mke wake wa mwanzo kwa kuwa ndie alikuwa akimwandalia kila
kitu kama keki, chakula, nguo, na sehemu za sherehe nk.
Batarokota anatarajia kufikisha miaka 42 Aprili 14 mwaka huu, siku hiyo
ataifanya maalumu kwa ajili ya kusali na kuwaombea marehemu wote
walikuwanae katika sherehe zake za kuzaliwa hapo mwanza kama mke wake
Marehemu Saula Kapama, shemeji yake Patricia Kapama, Babu yake Zachalia
Kapoja, Bibi yake Zachalia Kaboja, Dada yake mpendwa Happy Linda, Mwanae
Ruth Linda na wengine wengi ambao wametangulia mbele ya haki.
“Tangu mke wangu Mama Ngw`bis aliyofariki sijawahi kufanya sherehe ya kuzaliwa kwangu kwa kuwa najisikia vibaya, nakumbuka miaka ya nyuma nilikuwa nafanya hivyo nikiwa na mke,mtoto, na marafiki zangu mara zote na ndiyo maana nimeshindwa kufanya peke yangu kwa kipindi chote.
“Wiki ijayo nitakuwa natimiza miaka 42, hivyo nimeona ni vizuri siku hiyo kuitumia kwa kumkumbuka watu wote wapendwa, ila sina mpango wa kusherehekea tena,” aliandika Bataokota kwenye akaunti ya Instagram baada ya baadhi ya makampuni yakitaka kufanya sherehe ya kukumbuka kuzaliwa kwake.