Week Hot newz

Hakuna mbadiliko katika sheria msingi ya ndoa.


(Vatican Radio) Baba Mtakatifu Francisko wiki hii alitoa nyaraka mbili za “Motu proprio”zinazolenga kufanya mabadiliko katika Mfumo wa Mahakama ya Kanisa Katoliki juu ya uendeshaji wa kesi zinazohusiana na sheria ya ndoa.
Papa alitoa nyaraka hizo siku ya Jumanne, Motu proprio,  “Mitis Iudex Dominus Jesus”au Bwana Yesu, Hakimu mwenye huruma", ambayo inarekebisha kanuni za mahakama ya sheria ya kanisa (CIC) kwa Makanisa ya Amerika, na barua nyingine, “mitis et misericors Jesus"Msamaha na huruma  ya Yesu”, ambayo inafanya inarekebisha Kanuni za Makanisa  za Kanisa katika uendeshaji wa kesi za kubatilisha ndoa kwa Makanisa ya Mashariki (CCEO).

Profesa katika Sheria za Kanisa katika Chuo Kikuu cha Kipapa ya Gregorian cha Papa Rome, Padre James J. Conn, SJ, akizungumzia  marekebisho hayo ameiambia Redio Vatican kwamba,  kuna mabadiliko maalum matatu , hasa katika uharakisha wa kushughulikia  kesi za wanaondoa wanaotaka kubatilisha ndoa;  kuondolewa kwa haja ya mahakama kutoa hukumu mara mbili kwa tukio na kisha tena kupelekwa katika mahakama ya rufaa, kwa maana kwamba, inatosha kuzingatia maamuzi yaliyotolewa na mahakama kwa mara ya kwanza, iwapo  yanayoona kwamba , kuna ushahidi wa kutosha kwa ndoa kutanguliwa, na wahusika wanaweza kufunga ndoa   ndoa mpya kwa mujibu wa sheria Kanisa (au katika kupokea miungano ya ndoa ilifungwa  kwa sheria za kiraia , wakati huo huo kutambuliwa na Kanisa).
Pia kuanzishwa kwa uwezekano wa kesi kusikilizwa na hakimu mwenye uzoefu mara  moja, kama hatua ya kupunguza mzigo wa wingi wa kesi katika mahakama za majimbo, ambako watu wenye ujuzi ni wachache);  Na uundaji wa kueleka mchakato wa kesi  katika baadhi ya kesi , kutolewa maamuzi moja kwa moja na Askofu mahalia, kwa kesi ambazo zina ushahidi wa kutosha kutolewa hukumu ya kubatishwa na pande zote mbili zinaamini muungano wao ulikuwa batili. Katika mchakato huu hasa unaonyesha dhamira Papa Francisco  kugawana madaraka na Maaskofu wa majimbo duniani kote.

Prof Conn, SJ, aliendelea kufafanua kwamba - kinyume na uvumi uliotolewa na baadhi ya vyombo vya hata katika vyombo vya Kanisa, mabadiliko yamefanyika katika misingi ya uelewa wa Kanisa la asili na muundo wa kimsingi wa ndoa, na hivyo hakuna mabadiliko kaika Madhumuni msingi na wigo wa mfumo wa Kanisa mahakama. Na wala hakuna mabadiliko katika mafundisho ya Kanisa  juu ya kutengua ndoa, alisema Prof. Conn, SJ. Na kwamba, nayaraka mpya za mabadiliko hazibadilishi kanuni zinazofuatwa na Mahakimu katika  kubatilisha ndoa  na wala hazibadili uhalali wa ndoa,  hivyo, ndoa kubatilishwa linabaki ni jambo linalohitaji uwepo wa ushahidi wa kutosha .

Daily Reading for Friday, September 11th, 2015


Reading 1, First Timothy 1:1-2, 12-14

1 Paul, apostle of Christ Jesus appointed by the command of God our Saviour and of Christ Jesus our hope,
2 to Timothy, true child of mine in the faith. Grace, mercy and peace from God the Father and from Christ Jesus our Lord.
12 I thank Christ Jesus our Lord, who has given me strength. By calling me into his service he has judged me trustworthy,
13 even though I used to be a blasphemer and a persecutor and contemptuous. Mercy, however, was shown me, because while I lacked faith I acted in ignorance;
14 but the grace of our Lord filled me with faith and with the love that is in Christ Jesus.

Responsorial Psalm, Psalms 16:1-2, 5, 7-8, 11

1 [In a quiet voice Of David] Protect me, O God, in you is my refuge.
2 To Yahweh I say, 'You are my Lord, my happiness is in none
5 My birthright, my cup is Yahweh; you, you alone, hold my lot secure.
7 I bless Yahweh who is my counsellor, even at night my heart instructs me.
8 I keep Yahweh before me always, for with him at my right hand, nothing can shake me.
11 You will teach me the path of life, unbounded joy in your presence, at your right hand delight for ever.

Gospel, Luke 6:39-42

39 He also told them a parable, 'Can one blind person guide another? Surely both will fall into a pit?
40 Disciple is not superior to teacher; but fully trained disciple will be like teacher.
41 Why do you observe the splinter in your brother's eye and never notice the great log in your own?
42 How can you say to your brother, "Brother, let me take out that splinter in your eye," when you cannot see the great log in your own? Hypocrite! Take the log out of your own eye first, and then you will see clearly enough to take out the splinter in your brother's eyes.

Tanzania imezindua mradi wa Ujenzi wa kituo cha magonjwa ya moyo


Chumba cha cha upasuaji - ANSA
  
 Serikali imezindua mradi wa ujenzi wa kituo cha ubora wa sayansi ya magonjwa na mishipa ya moyo  nchini Tanzania kitakachokuwa na uwezo wa kutoa huduma za kitabibu na kitafiti kwenye magonjwa hayo kwa nchi zote za ukanda wa Afrika mashariki.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam Septemba 10, Mkurugenzi wa Elimu ya juu nchini, Profesa Sylivia Temu, alisema mradi huo unaotekelezwa na serikali kwa ushirikiano na Benki ya Maendeleo Afrika, ni mojawapo ya miradi minne ya afya inayotekelezwa kwenye ukanda wa Afrika Mashariki ikilenga kutatua changamoto mbalimbali za kiafya.
Vile alisema kila nchi ya Afrika inayo miradi ya aina yake kwenye sekta hiyo muhimu , na kwa upande wa Tanzania wamejikita katika kukabiliana na magonjwa ya moyo , mradi huo utakuwa chini ya uangalizi wa Chuo kukuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (Muhas), ambao utakwenda sambamba na ujenzi wa Kampasi mpya ya Chuo Kikuu hicho , kilichoko eneo la Mlonganzila  jijini Dar Es Salaaam.
 Profesa Temu akiongea pia kwa niaba ya Waziri wa Elimu a Mafunzo ya Ufundi Dk Shukuru Kawamba ,aliongeza kwamba mradi huo utasaidia kupunguza vifo vitokanavyo na magonjwa ya moyo nchini, na kupunguz gharama zinazolikabili taifa kwa sasa kutokana na kusafirisha nje idadi kubwa ya wagonjwa wa moyo kupata matibabu.
 Lakini pia kupitia kituo hiki kitakacho kuwa kikubwa kabisa hapa Afrika Mashariki, wanatarajia kwamba tafiti nyingi za masuala ya kiafya hasa kwenye eneo hili la magonjwa ya moyo zitakuwa zikifanyika  nchini Tanzania na pia kupitia Muhas, watazalisha wataalam wengi wa magonjwa hayo kwa manufaa ya vyuo vingine ndani na nje ya nchi, aliongeza.
Kwa upande wa Makamu Mkuu wa Muhas, Profesa Ephata Kaaya, alisema chuo chake kimejipanga kutekeleza mradi huo mkubwa utakaotekelezwa kwa awamu mbili, awamu ya kwanza utahusisha mafunzo pamoja na maandalizi ya vifaa huku awamu ya pili ikuhusisha ujenzi kamili wa kituo hicho alisema.
Meneja Miradi ya Jamii kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika, Hamis Simba, alizitaja baadhi ya sababu zilizosababisha benki hiyo kufadhili mradi ho kuwa ni pamoja  na kuvutiwa na mikakati ya Tanzania na nchi za Afrika Mashariki kwa ujumla katika kukabiliana na magonjwa ya moyo.
Na Shirika la Utafiti wa Magongwa na Tiba barani Afrika (Amref), limezindua zahanati zilizofanyiwa ukarabati kupitia mradi wa Afya ya uzazi ni haki ya vijana tuitetee' katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam Tanzania
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Amref, Meneja wa Mradi huo na mtaalamu wa afya ya uzazi na afya ya watoto, Dk. Beatus Sambili, alisema mradi huo ulianzishwa kwa ajili ya kuwakusanya vijana na kuwapatia elimu juu ya namna ya kupambana na magonjwa ya ngono, maambukizi ya Virusi vya Ukimwi, matumizi ya dawa za kulevya na mimba za utotoni. 
Mbali na uzinduzi wa zahanati hizo, pia  Amref imekabidhi vifaa mbalimbali vitakavyotumiwa na zahanati hizo.Baadhi ya vifaa hivyo ni viti, benchi la kukalia wagonjwa lililotengenezwa kwa plastiki, televisheni, deki, ving'amuzi, meza za ofisini na mbao za matangazo. Aidha, alisema mradi huo ulianzishwa kwa kuzilenga Manispaa za Kinondoni na Ilala kwa Jiji la Dar es Salaam na Manispaa ya Iringa kwa Nyanda za Juu Kusini.
 Alizitaja Zahanati zilizonufaika na huduma hiyo kuwa ni Kiwalani, Vingunguti, Mongo la Ndege na kituo na Pugu Kajiungeni. Wakizungumzia mradi huo, Waganga Wafadhili  wa Zahanati zilizofanyiwa ukarabati na Amref, walisema watatumia fursa hiyo kupambana na changamoto zilizokuwa zikiwakabili katika utoaji wa elimu na huduma mbalimbali kwa vijana kutokana na upungufu wa vifaa.

St. Paphnutius

Short Cuts
Image of St. Paphnutius

Facts

Feastday: September 11


The holy confessor Paphnutius was an Egyptian who, after having spent several years in the desert under the direction of the great St. Antony, was made bishop in the Upper Thebaid. He was one of those confessors who under the Emperor Maximinus lost the right eye, were hamstrung in one leg, and were afterwards sent to work in the mines. Peace being restored to the Church, Paphnutius returned to his flock, bearing all the rest of his life the glorious marks of his sufferings for the name of his Crucified Master. He was one of the most zealous in defending the Catholic faith against the Arian heresy and for his holiness. As one who had confessed the Faith before persecutors and under torments, he was an outstanding figure of the first General Council of the Church, held at Nicaea in the year 325. Paphnutius, a man who had observed the strictest continence all his life, is said to have distinguished himself at the Council by his opposition to clerical celibacy. Paphnutius said that it was enough to conform to the ancient tradition of the Church, which forbade the clergy marrying after their ordination. To this day it is the law of the Eastern Churches, whether Catholic or dissident, that married men may receive all Holy Orders below the episcopate, and continue to live freely with their wives. St. Paphnutius is sometimes called "the Great" to distinguish him from other saints of the same name; the year of his death is not known. His feast day is September 11.

Papa akutana na Waziri Mkuu wa Kuwait


Papa Francisko akimpokea Waziri Mkuu Kuwait Sheik Jaber Mubarak Al-Hamad Al Sabah - ANSA

(Vatican Radio)  Jumatano, Septemba 10, 2015, Papa Francis alimpokea na kuzungumza nae , Waziri Mkuu wa Kuwait, Sheikh Jaber Mubarak Al-Hamad Al-Sabah. 
Katika mazungumzo yao ya kirafiki , waligusia mandhari mbalimbali ya maslahi kwa pande zote ikiwemo  michango chanya ya kihistoria ya Wakristo wachache miongoni mwa jamii Kuwait. Na pia walilenga umuhimu wa elimu katika kukuza utamaduni wa kuheshimiana,  mshikamano na ujenzi wa amani kati ya watu tofauti na wenye dini tofauti.

Baada ya Kukutana na Papa,  Waziri Mkuu Sheikh Jaber na ujumbe wake alikutana na Katibu wa Nchi wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin,akiwa amefuatana Askofu Mkuu Paulo Ghallager , Mkuu wa Idara ya mahusiano ya nchi za nje wa Vatican. Lengo la kukutana kwao ilikuwa  kutia saini katika Mkataba wa Maridhiano kati Sekretarieti ya Nchi  ya Vatican na Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi ya Kuwait . Utiaji huo wa saini,  ulifanywa na  Askofu Mkuu Paulo Gallagher na Waziri  Sheikh Sabah Khalid Al-Hamad Al-Sabah, Naibu Waziri katika  waziri wa Mambo ya Nje, Kuwait.
Taarifa inataja kuwa Mkataba huo,  unawezesha utendaji thabiti zaidi kwa pande zote mbili, kuimarishwa  zaidi na kuwa na mahusiano thabiti baina ya nchi, katika kushirikiana , kuheshimiana, kujenga  amani na utulivu wa kikanda na kimataifa.