Batarokota amedai wimbo wake huo umebeba maudhui halisi ya utamaduni wa Kitanzania kwa Lugha ya kisukuma na ambao umechangia kumweka hapo halipo, Batarokota amesema kuwa mbali na kuanza muziki muda mrefu na kufanikiwa kuingiza nyimbo kwenye Tuzo za kili kwa mara ya kwanza lakini ataendelea na mapambano.
Hata hivyo msanii huyo ameamua rasmi kuimba muziki wenye vionjo vya asili na kuachana na muziki wa kutumia sapo ya beat za magharibi ambao alikuwa akiufanya hapo kwanza, ' kwejanga nyangisha ni nyimbo yangu ya pili nilitoka na Kamle Balongo nikiwa na Mama Nyamoko na nikaona ni vizuri nami nianze na hii, na tana nimekuja na Irombo rise, ila nimeshawahi kutoa songi nyingi zenye mahadhi ya kizazi kipya ukiwemo upendo kwa mama, ogopa 666, kiama sasa, vita vya wenyewe kwa wenyewe , ni mzuri tu we, total balaa, vichwa vya kale, tumerudi, ', alisema na kuongeza.