Week Hot newz

Mwanamke wa miaka 72 ajifungua mtoto India

Mwanamke wa umri wa miaka 72 amejifungua mtoto mvulana katika hospitali moja nchini India.Mwanamke huyo alipachikwa mimba kupitia njia ya kitaalamu ya IVF ambapo yai la mwanamke hutolewa kutoka kwenye ovari, kutungishwa mbegu ya kiume na kisha kurejeshwa kwenye mji wa mimba. Yai hilo linaweza kutolewa kwa mwanamke mwingine.
Njia hiyo hutumiwa kuwawezesha wanawake tasa kupata watoto.
Daljinder Kaur alijifungua mtoto wake baada ya kupokea matibabu kwa miaka miwili katika hospitali iliyoko jimbo la Haryana.
Matabibu walifanikiwa kumtungisha mimba kupitia IVF mara yao ya tatu.
Mumewe Kaur ana umri wa miaka 79.

Wajibu wa wabatizwa kumtangaza Kristo kila mahali.

Umati wa watu wakimsikiliza Papa Francisco wakati wa sala ya Malkia wa Mbingu
08.05.2016 - REUTERS


Baba Mtakatifu Francisko, Jumapili  akisali sala ya Malkia wa Mbingu,Jumapili ya saba ya kipindi cha Pasaka, alihimiza Wakristo kumhubiri Kristo, kila mahali duniani bila woga. Himizo hilo alilitoa  mbele ya maelfu ya mahujaji na wageni  waliokusanyika  katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro , Jumapili hii ambayo pia Mama Kanisa alikuwa akiadhimisha Sikukuu ya Kupaa Rabbi, na Siku ya Mama wote .
Akitoa hotuba fupi juu ya siku kuu  ya Kupaa Rabbi , Papa alisema, "awali kabla ya kuwaacha marafiki zake , Yesu alifanya rejea katika kifo na ufufuko wake , akisema ninyi ni mashahidi wangu. Na kumbe Yesu anawataja mitume wake waliokuwa mashahidi wakati wa mateso kifo na ufufuko wake pia wanakuwa mashahidi wake wakati wa kupaaa kwake Kristo"