Pichani juu kutoka kushoto Daniel Renatus akiwa na Msanii wa bongo fleva na mziki wa asili
ya kitanzania Batarokota.
Nyota wa muziki wa kizazi kipya na mziki wa asili ya Kitanzania , Batarokota, aliyetamba
na nyimbo za 'kwejanga nyangisha' na 'sauti ya haki ', amekanusha tuhuma mbaya
zinazomzunguka kwamba anatumia dawa za kulevya.
Akizungumza na 'http://batarokota.blogspot.com/' leo asubuhi, msanii Batarokota alisema anahisi kufananishwa kwake na
nyota wa Bongofleva, 'Chid Benz' aliyekuwa akitumia dawa
hizo huenda ndiyo chanzo cha kuzushiwa kashfa hiyo.
"Kiukweli mimi situmii dawa za kulevya hata kidogo, na huwa naumia
sana ninapoambiwa taarifa hizi, sijui hata ladha yake, ila nadhani watu
wanakuwa wakinifananisha, unajua mimi huwa nafananishwa sana na Chib Benz,
hivyo labda ndiyo sababu ya kuwapo kwa taarifa hizi mitaani, ila
kiukweli mimi si mtumiaji wa dawa za kulevya," alisema.
Pichani juu kutoka kushoto msanii Shingwengew akiwa na Msanii wa bongo fleva na mziki wa asili
ya kitanzania Batarokota
Batarokota, msaniii huyo ambaye sasa anatarajia kuachia wimbo mpya, amesema nje ya kazi yake ya muziki kwa sasa anafanya biashara ya
urembo wa kiasili kama uchuraji na kutengeneza mavazi kama njia ya kujiongezea
kipato.