Yesu amekuja ulimwenguni ili kuufunua,
kuutangaza na kuushuhidia ukweli, ambao umekuwa ni sababu ya kugawanyika
kwa walimwengu kwani wanataka kutembea katika giza la dhambi na mauti. -
RV
11/08/2016 16:08
Mitandao ya kijamii:
Ukweli
ni uthibitisho wa kitu chochote au tukio lolote lile kadiri ya uhalisia
wake. Kwa mfano ukweli kuhusiana na maji katika hali ya kimiminika ni
kwamba yanapokutana na mteremko na hakuna kizuizi chochote basi
yatatiririka kuelekea chini. Kwa maneno mengine ukweli unatupeleka
katika kuutafakari ulimwengu huu kadiri ulivyopangwa na kuumbwa na
Mwenyezi Mungu. Hivyo ukweli huo ambao huelezewa kwetu kwa njia ya neno
lake unabaki daima kama ulivyo na kamwe hauwezi ukabadilika kama
asemavyo Mungu kwa kinywa cha Nabii Isaya kwamba: “Majani yakauka, ua
lanyauka; Bali neno la Mungu wetu litasimama milele” (Is 40:8).