
Athari za uvutaji sigara
Idadi ya wavutaji wa sigara duniani imeongezeka kwa karibu bilioni moja kwa mujibu wa takwimu mpya.
Watafiti walioandika katika jarida la Shirika la
madaktari la Marekani wanasema hata hivyo kuwa idadi hiyo ni ndogo
ikilinganishwa na ongezeko la watu kwa ujumla duniani na kuelezea haja
ya juhudi zaidi kufanyika kuwazuia watu kuwa na tabia hiyo.
Idadi ya watu wanaovuta sigara kila
siku duniani imepanda kwa kiwango cha watu takriban milioni 250 million
kati ya mwaka 1980 na 2012, kwa mujibu wa ripoti .