NA MWANDISHI WETU, MWANZA AZAM FC wameshindwa kuibuka na ushindi katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, baada ya kula...
Utafiti: Watu wanene 'ndio wengi duniani'
Utafiti mpya
umeonesha watu wazima wengi duniani ni wanene kupita kiasi na kwamba
hakuna matumaini ya kufikia lengo la kupunguza idadi ya watu wanene
duniani.
Wanasayansi waliofanya utafiti huo ambao walitoka Chuo
cha Imperial cha London, wakiandika katika jarida la kimatibabu la
Lancet la Uingereza, wanasema miongo minne iliyopita, kuwa na uzani wa
chini kupita kiasi lilikuwa tatizo kubwa kuliko unene.
Wanasema idadi ya wanaume wanene imeongezeka mara tatu, nayo ya wanawake ikaongezeka mara dufu.
Profesa Majid Ezzat, aliyeongoza utafiti huo, anasema ni kana kwamba kuna "mkurupuko wa unene".
Wanasayansi
hao wanaonya kwamba tatizo hilo ni kubwa sana kiasi kwamba haliwezi
kutatuliwa kupitia njia za kawaida za matibabu au kutenga maeneo ya
kuendeshea baiskeli.
wanandoa wanene Duniani ni awa.
Baada
ya kuchunguza takwimu kutoka nchi 186, watafiti hao walibaini kwamba
idadi ya watu wanene duniani imeongezeka kutoka 105 milioni mwaka 1975
hadi 641 milioni mwaka 2014.Idadi ya watu walio na uzani wa chini ya kuwango imeongezeka kutoka 330 milioni hadi 462 milioni katika kipindi hicho.
Viwango
vya unene miongoni mwa wanaume kilipanda kutoka 3.2% mwaka 1975 hadi
10.8%, na miongoni mwa wanawake viwango vya unene vilipanda kutoka 6.4 %
mwaka 1975 hadi 14.9%.
Hii ina maana kulikuwa na wanaume wanene 266 milioni na wanawake wanene 375 milioni mwaka 2014.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni