Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Farida ambaye pia ni msanii wa filamu nchini, alisema kuwa ameishi na mume wake kwa miaka tisa lakini kadiri siku zinavyokwenda, ndivyo upendo unavyopoa na kitendo cha kufikia uamuzi wa kuwa na mapenzi na Diamond na kuchora tattoo zake ili kujibu mashambulizi kwa mumewe ambaye naye alijichora jina la mwanamke wake mgongoni.
“Binafsi nilikuwa nampenda sana mume wangu, lakini kitendo cha kuwa anakuja na hawara zake nyumbani kwa nyakati tofauti, huku nikiwapikia bila kujua, kilinifanya na mimi niwe na hasira hasa baada ya kumuona mume wangu
amechora mgongoni jina la mwanamke ninayemfahamu kama ni mpenzi wake, hivyo nami nikaona nilipe kisasi,” alisema Farida ambaye pia ni msanii.
Farida ambaye pia anamiliki kundi lake la sanaa lijulikanalo kwa jina la Msofe Sanaa Group, alisema kuwa, kipigo alichokipata kikiambatana na talaka kutoka kwa mume wake, kilikuwa kama ukombozi kwake, kwani alikuwa amechoka kuishi maisha hayo ambayo mwisho wa siku huenda angejikuta anaambulia kuambukizwa maradhi ikiwamo VVU.
Hivi karibuni msanii huyo aliripotiwa kuwa amepewa talaka na mume wake kwa kile kilichodaiwa kutoka kimahaba na msanii huyo anayekimbiza kwenye muziki wa kizazi kipya.
Alipotafutwa Diamond kuzungumzia sakata hilo, simu yake ya mkononi iliita bila kupokewa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni