Week Hot newz

Tafakari ya Neno la Mungu, Jumapili ya Tatu ya Kipindi cha Mwaka A wa Kanisa

Tupo pamoja tena nawe katika jiji la upendo wa Mungu, yaani Neno lake ambalo daima latupatia uzima na pia latufanya tuwe huru katika maisha yetu kama kweli tunaliishi na kulifuata kwa unyenyekevu. Ni Dominika ya III ya kipindi cha kawaida cha mwaka A, kipindi cha matumaini kama ambavyo chajionesha katika mavazi ya Misa Takatifu, yaani rangi ya kijani.

Masomo tunayoyatafakari tunayapata katika kitabu cha Isaya 9:1-4, 1Kor. 1:10-13,17 na Injili Mt. 4:12-23. Masomo haya yanatupa mwaliko wa kuona na kuupokea mwanga wa Kristu unaoanza

Pope Francis: appeal for peace in Syria



(Vatican Radio) Pope Francis appealed for peace in Syria on Wednesday, offering prayers for leaders and policy experts gathering in Switzerland for a conference aimed at working toward a resolution of the Syrian civil war that has claimed more than 100 thousand lives and driven millions of people from their homes. Listen:

Speaking at the end of his weekly General Audience, Pope Francis said, “I ask the Lord to touch the hearts of all [parties and participants], that, looking only to the greater good of the so sorely tried Syrian people, they might spare no effort to reach as quickly as possible the cessation of violence and the end of the conflict, which has already caused too much suffering.”

The Holy Father went on to say, “I hope for dear nation of Syria [that it undertake] with conviction the path of reconciliation, concord and reconstruction with the participation of all citizens, in which everyone can find in the other, not an enemy, not a rival, but a brother to welcome and embrace.”

The “Geneva 2” international conference for peace in Syria opens Today, Wednesday, January 22nd, in Montreaux, Switzerland, with negotiations to continue in Geneva starting on Friday, January 24th.



Text from page http://en.radiovaticana.va/news/2014/01/22/pope_francis:_appeal_for_peace_in_syria/en1-766183
of the Vatican Radio website

Jifunueni wazi kwa Injili na maajabu ya Mungu – Papa

Jumatatu , Baba Mtakatifu Francisko, alisema uhuru wa Mkristo hupatikana katika utulivu wa kulisikiliza Neno la Mungu na kuliishi. Papa alieleza wakati akihubiri katika Ibada ya Misa, asubuhi, katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta, ndani ya Vatican. Papa alisema daima ni lazima kuwa tayari kuupokea ujumbe wa injili na miujiza ya Mungu aliyo ihifadhi kwa ajili yetu sisi.

Alisisitiza kwamba,

Wakristu toeni cheche za imani yenu kila siku.



Jumapili, Papa Francisko alifanya ziara ya Kichungaji , katika Kanisa la Moyo Mtakatifu wa Yesu la Roma , katika mtazamo wa adhimisho la 100 tangu Kanisa kuanzisha Siku ya Kimataifa kwa ajili ya kujali hali ya Wahamiaji na Wakimbizi.
Kanisa hilo, ambalo pia lina hadhi ya Basilika, lililoko karibu na Kituo cha Kikuu Treni cha Kati, jijini Roma , huendeshwa na Wamisionari WaSalesians ya Don

Taharuki ya Mtakatifu Yosefu! Mtu wa haki!



“Kuzaliwa kwa Yesu Kristo kulikuwa hivi. Maria mama yake, alipokuwa mchumba wa Yosefu, kabla hawajakaa pamoja alionekana na mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Mumewe Yosefu akiwa mtu mwadilifu, hakupenda kumwaibisha hadharani. Basi akanuia kumwacha kwa siri.”
(Mt 1:18-19)

Moja ya kifungu cha maneno

Nyumba ya Papa ni mali ya Wakatoliki wote!

Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi, tarehe 16 Januari 2014 amekutana na kuzungumza na wafanyakazi wanaotekeleza dhamana na utume wao kwenye Makazi ya Papa mjini Vatican. Baba Mtakatifu amewashukuru kwa huduma na ukarimu wanaowashirikisha wageni mbali mbali wanaofika mjini Vatican kwa ajili ya kukutana na kuzungumza na Khalifa wa Mtakatifu Petro.

Baba Mtakatifu anasema kwamba, Nyumba ya Papa ni mali ya Waamini wote wa Kanisa Katoliki; mahali ambapo wanaonja tone la upendo na moyo wa ukarimu wa kifamilia pamoja na msaada wa kulinda na kudumisha imani ambayo ni zawadi kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Mmiliki mkuu wa Nyumba ya Kipapa ni Yesu mwenyewe na wengine wote ni wafuasi na wahudumu wa Injili.

Baba Mtakatifu anasema kutokana uelewa huu, kuna haja kwa wafanyakazi hao kukuza na kudumisha majadiliano ya kina kwa njia ya sala, ili kuimarisha urafiki na uhusiano wa ndani kabisa, tayari kutolea ushuhuda wa upendo na huruma ya Mungu kwa watu wake. Wafanyakazi hawa anasema Baba Mtakatifu wanapotekeleza utume wao, kazi inaweza kuwa ni fursa ya kuwashirikisha wengine furaha ya kuwa ni sehemu ya Fumbo la Mwili wa Kristo, yaani Kanisa.

Baba Mtakatifu anawaalika kuwa makini katika kuisikiliza sauti ya Mwenyezi Mungu inayowaita kila siku, kumtumikia kwa ukomavu na moyo wa ukarimu. Baba Mtakatifu amewatakia wafanyakazi hawa pamoja na familia zao, kheri na baraka kwa Mwaka Mpya 2014.

Ujumbe wa Papa Francisko kwa ajili ya Siku ya Wakimbizi na Wahamiaji Duniani kwa Mwaka 2014



Hali ya wakimbizi, wahamiaji na watu wasiokuwa na makazi maalum inahitaji kuangaliwa kwa usawa na ukamilifu zaidi, kwa njia ya ushirikiano wa kimataifa unaosimikwa katika mshikamano na huruma.

Hiki ndicho kiini cha ujumbe wa Siku ya 100 ya Wakimbizi na Wahamiaji inayoadhimishwa na Mama Kanisa kila mwaka ifikapo tarehe 19 Januari. Ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko kwa Mwaka 2014 unaongozwa na kauli mbiu “Wahamiaji na wakimbizi: kuelekea ulimwengu bora zaidi”.

Tafakari ya Neno la Mungu, Sherehe za Ubatizo wa Bwana



Mpendwa mwana wa Mungu, tuko tena pamoja katika ile habari ya furaha ndiyo kushirikishana mapendo ya Mungu kwa njia ya meza ya Neno lake.

Leo ndipo tunahitimisha kipindi cha Noeli kwa Sikukuu ya Ubatizo wa Bwana na tunaanza kipindi cha kawaida cha mwaka wa Kanisa. Kumbe leo pia ni Dominika ya kwanza ya kipindi cha kawaida cha mwaka wa Kanisa.

Katika somo la kwanza Nabii Isaya anatupeni habari juu ya mtumishi wa Mungu ambaye anapokea Roho wa Mungu na kazi

Vatican kujieleza kuhusu kashfa za ngono


Papa Francis
Maafisa katika Vatican makao makuu ya kanisa katoliki, wanatarajariwa kuhojiwa na maafisa wa Umoja wa Mataifa kuhusu dhuluma za kingono ambazo makasisi wa kanisa hilo waliwatendea maelfu ya watoto.
Maafisa hao walikataa ombi la awali ambapo Umoja wa Mataifa ulikuwa unataka taarifa za kina kuhusu dhuluma za kingono wakisema kuwa visa hivyo vinapaswa kushughulikiwa na idara ya mahakama katika mataifa ambako visa hivyo vilitokea

Idadi ya waamini na mahujaji waliokutana na Papa Francisko kwa Mwaka 2013 imeongezeka!

Takwimu zinaonesha kwamba, tangu Baba Mtakatifu Francisko alipochaguliwa kuliongoza Kanisa Katoliki hapo tarehe 13 Machi 2013, zaidi ya watu millioni sita wamekutana na kushiriki katika matukio mbali mbali yaliyoendeshwa na Baba Mtakatifu katika kipindi hiki hadi kufikia mwanzo mwa Januari 2014. Waamini, mahujaji na wageni walioshiriki katika katekesi zake zinazotolewa kila Jumatano walikuwa ni1, 548, 500.


Baba Mtakatifu alifanikiwa kukutana na kuzungumza na watu 87, 400 kwa faragha. Waamini na mahujaji wapatao 2, 282, 000 walishiriki katika Ibada mbali mbali zilizoongozwa na Baba Mtakatifu Francisko kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro na ndani ya Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican. Waamini zaidi ya 2, 706, 000 wameshiriki katika Sala ya Mchana na Baba Mtakatifu Francisko.

Takwimu hizi ni zile tu zilizokusanywa mjini Vatican na wala hazihusishi matuko kama: Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani kwa Mwaka 2013yaliyofanyika nchini Brazil, kule Rio de Janeiro; wala safari zake za kichungaji ndani ya Italia, Lampedusa, Cagliari na Assisi hata katika baadhi ya Parokia zilizoko katika Jimbo kuu la Roma.

Kwa ujumla waamini na watu wenye mapenzi mema wapatao 6, 623, 000 wamekutana na kushiriki katika Ibada, Katekesi na Sala zilizokuwa zinaongozwa na Baba Mtakatifu Francisko. Itakumbukwa kwamba, idadi hii ya watu ni ile tu ambayo ni rasmi kwa wale watu walioomba tiketi kutoka Vatican. Kumekuwepo na umati mkubwa wa watu wanaomiminika kwenye matukio mbali mbali anayoshiriki Baba Mtakatifu Francisko, hii inatokana na mvuto alionao kwa watu!


Uraibu wa sigara wawavutia wengi


Athari za uvutaji sigara
Idadi ya wavutaji wa sigara duniani imeongezeka kwa karibu bilioni moja kwa mujibu wa takwimu mpya.
Watafiti walioandika katika jarida la Shirika la madaktari la Marekani wanasema hata hivyo kuwa idadi hiyo ni ndogo ikilinganishwa na ongezeko la watu kwa ujumla duniani na kuelezea haja ya juhudi zaidi kufanyika kuwazuia watu kuwa na tabia hiyo.
Idadi ya watu wanaovuta sigara kila siku duniani imepanda kwa kiwango cha watu takriban milioni 250 million kati ya mwaka 1980 na 2012, kwa mujibu wa ripoti .

Matumaini ya kupata chanjo dhidi ya Malaria kwa Mwaka 2014?



Kuna matumaini makubwa kwa Bara la Afrika katika kipindi cha Mwaka 2014 kuweza kupata kinga dhidi ya ugonjwa wa Malaria ambao umekuwa ni tishio kwa maisha na maendeleo ya wananchi wengi Barani Afrika. Majaribio ya chanjo yaliyofanywa kwa watoto 15, 500 yanaonesha kwamba, ugonjwa wa Malaria ulipingua kwa kipindi cha miezi 18 ya majaribio ya chanjo hii mpya. 


Kampuni ya GlaxosmithKline inatarajiwa

مجلة لا شيفيلتا كاتوليكا تنشر نص الحوار بين البابا فرنسيس واتحاد الرؤساء العامين





نشرت مجلة لا شيفيلتا كاتوليكا يوم أمس الجمعة نص الحوار الذي أقامه البابا فرنسيس مع اتحاد الرؤساء العامين في التاسع والعشرين من تشرين الثاني نوفمبر الماضي، وأعلن الحبر الأعظم في ختام هذا اللقاء أن العام 2015 سيكون عام الحياة المكرسة. استغرق هذا الحوار قرابة الثلاث ساعات وتمحور حول أبرز التحديات المطروحة اليوم أمام الحياة الرهبانية والكنيسة بصورة عامة. قال البابا إن الرهبان والراهبات يتبعون الرب بطريقة خاصة ونبوية، وينبغي بالتالي أن يكونوا رجالا ونساء قادرين على إيقاظ العالم. وحض على تفادي التطرف الأصولي والنظر إلى الواقع

Epifania ya Bwana: Dhahabu, Uvumba na Manemane! Kazi kwako!

Sikukuu ya Epifania inayoitwa pia Tokeo la Bwana ni sherehe kubwa sana kwa wakristu. Kwa bahati mbaya siku hii imegeuzwa kuwa kama ya maigizo ya watoto wanaopita kuimba nyumba hadi nyumba na kupata zawadi. Kwa hiyo badala ya kuwa Epifania tungeweza kuiita kwa kiingereza Happy-funny.
 

Sikukuu ya leo inayo mafundisho ya maisha yanayoweza kumtosha kila mtu. Ukifaulu kutanguzana kidhati na wasafriri wanaotajwa katika sikukuu ya leo watakufikisha kwenye uhondo wa maisha. Wasafiri hao wanaitwa majusi. Wametokea mashariki ya mbali wakielekea Betlehemu. Wasafiri hao hawatajwi idadi wala majina kama tunavyosadikishwa kuwa walikuwa watatu. Tunaambiwa tu Kulikuwa majusi kutoka mashariki ya mbali.

Jubilee ya Miaka 50 tangu Papa Paulo VI alipotembelea Yerusalem!


Ilikuwa ni tarehe 4 Januari 1964, takribani miaka 50 iliyopita, Baba Mtakatifu Paulo wa sita alikuwa anaanza hija ya kichungaji Nchi Takatifu na kuhitimisha safari hii ya kihistoria, jioni baada ya Maadhimisho ya Siku kuu ya Tokeo la Bwana, maarufu kama Epifania ya Bwana.

Baraka kwa Mwaka Mpya 2014



".. Bwana akubarikie, na kukulinda. Bwana akuangazie nuru za uso wake, na kukufadhili; Bwana akuinulie uso wake, na kukupa amani.." (Hesabu 6:22-27).


Mwaka mpya 2014 umeanza. Tushukuru Mungu kama tuliuanza katika mazingira ya kanisani kwa Ibada au hata kwa sala fupi na familia zetu. Kuna waliouanza, kwa bahati mbaya katika bar au fukwe za bahari. Hujachelewa bado, fanya hima katika juma hili ufanye ibada fupi na familia yako ili uanze na Mungu Baba.

Waisraeli walitamani sana kuanza kila kitu kwa baraka. Na ndio maana Mungu alimpa Musa "formula" hii ya baraka ili kuzima kiu yao. Tuone umuhimu wa baraka katika Maisha yetu. Tusikurukupe kwa cho chote Mwaka huu. Tuwe na unyenyekevu
wa kuomba baraka. Omba misa kanisani kwa lo lote unalonuia kufanya. Usifanye kwa akili na karama yako tu. Ujue wazi, Bwana asipoujenga mji waujengao wafanya kazi bure.

Tuombe :

Baba twaingojea kwa hamu sana kila Baraka utakayotukirimia kwa Mwaka huu mpya 2014. Baba uwe faraja na kimbilio la kila mmoja ndani ya familia zetu, kazi zetu, watoto wetu na rafiki zetu. Nyoosha mkono wako kwa kila familia zetu.

Imeandaliwa na
Padre Beno Michael Kikudo
Jimbo kuu la Dar es Salaam

Unene kupindukia katika nchi zinazostawi


Unene kupinduikia ni tatizo
Kunenepa kupindukia ni tatizo ambalo sasa linatishia zaidi maisha ya wengi katika mataifa yanayostawi duniani kuliko katika mataifa tajiri ambako mambo yana afadhali.
Sasa serikali nyingi zinaombwa kuongeza Ushuru vyakula hivyo vinavyosababisha watu kunenepa kupindukia kama njia ya kuokoa maisha ya watu kutokana na mshutoko wa moyo, kisukari na kiarusi.

THANK`S GOD 2014

Mkurugnzi wa Paskal Linda Blog akiwa na wafanyakazi wake kwa pamoja anawatakiwa heri ya mwaka mpya 2014.

Paskal Linda Blog itakuwa kila siku na vitu vipya mwaka 2014 mnakaribishwa sana kuangalia leo ni mwanzo tu wa mwaka.

Kwa mawasiliano zaidi piga simu +255 492623 au tembelea ofisini kwetu Morogoro- Msamvu (Neema Hotel).

Thank`s God


Njooni tumwabudu Mtoto Yesu! Mwaka 2014



Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii anawakumbusha kwamba, wanapotafakari sura ya Mtoto Yesu, wanatafakari pia uso wa Mwenyezi Mungu. Mwaliko wa kwenda kumwabudu! na kukaribisha Mwaka 2014.