Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Katekesi yake Siku ya Jumatano, tarehe 29 Januari 2013 alikemea vikali tabia ya michezo ya upatu inayodhalilisha utu na heshima ya binadamu na kwa kusema kwamba, huu si Ukristo wala si ubinadamu; ni tabia ambayo inapaswa kukomeshwa ndani ya Jamii kwani inawasababishia watu majanga ya maisha!
Baba Mtakatifu ameyasema hayo wakati alipokuwa anawasalimia wawakilishi wa Mfuko wa Yohane Paulo II wa washauri dhidi ya upatu kitaifa, ambao baadaye jioni waliadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwenye