
Hizi ni juhudi zilizofanywa na Askofu mkuu Konrad Krajevski, mtunzaji mkuu wa Sadaka ya Papa mjini Vatican, kwa kuwagawia waamini Rozari Takatifu na Picha ya Huruma ya Mungu, inayoonesha matumizi sahihi ya dawa hii ya maisha ya kiroho katika hija ya waamini kuyataktifuza malimwengu. Dawa hii imefungwa kitaalam kama Wafamasia wanavyofunga dawa kwa ajili ya matumizi ya binadamu, hali inayoonesha kipaji cha ugunduzi hata katika mambo ya kiroho.
Vifurushi vya dawa ya maisha ya kiroho vimeandaliwa katika lugha mbali mbali, kati ya lugha hizi ni Kiingereza, Kiitaliani, Kihispania na Kipolandi. Kwa hakika, watu wengi waliguswa na ugunduzi huu, kiasi cha kubaki wamepigwa na bumbuwazi!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni