
Tume ya wataalamu wa afya imeonya kuwa aina sugu ya vidudu vya bacteria ni moja kati ya tishio kubwa kabisa katika matibabu.
Katika taarifa iliyoandikwa kwenye jarida la
kisayansi, The Lancet, wataalamu wanatoa wito mataifa yashirikiane ili
kupambana na tishio hilo.Wataalamu hao wanaonya kuwa bila ya antibiotics, matibabu mengi, kutoka upasuaji hadi kutumia kemikali kutibu saratani - hayo hayatowezekana.
Na vifo kutokana na magonjwa ya kuambukiza katika nchi zilizoendelea vinaweza kurudi katika viwango kama vile vya awali ya karne ya 20.
Piya wataalamu wanasema gharama za matibabu huenda zikapanda sana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni