Akiandika katika ukurasa wake wa Histogram, Wema alisema anachukizwa
sana na kitendo hicho, kwani kinamfanya asikae kwa amani na watu walio
karibu yake, na wengine wanamtenga kupitia vichwa vya habari tofauti
vya magazeti, ambavyo kwa asilimia kubwa anasema vinatumika kuuzia
magazeti hayo.
“Hivi karibuni kuna gazeti moja limeandika, ‘Ishu ya dawa za kulevya –
Wema kunyongwa China,
aomba Watanzania kumuombea’, jamani siwezi
kusema kama nina furaha, sijawahi kufikiria kwamba magazeti yetu ipo
siku yatakuja kuandika uongo wa namna hii, kwa sababu nakaaga kimya ndio
wameona ni njia ya kunionea muda wote, roho inaniuma sana,” aliandika
mwanadada huyo ambaye amewahi kuwa Miss Tanzania mwaka 2006.
Wema alifafanua kuwa kutokana na kuona hapa nchini kuna maneno mengi
yasiyokuwa ya msingi, aliamua kwenda China kwa ajili ya kufanya mambo
yake binafsi, lakini watu ambao hawapendi maendeleo yake wamekuwa
wakimfuatilia na kuamua kumchafua katika magazeti.
“Sidhani kama nishawahi kumkosea yeyote katika maisha yangu, maskini
ya Mungu naishi maisha yangu mwenyewe sina habari na mtu, sijawahi hata
kufikiria kufanya biashara kama hii, muda uliopita niliambiwa nina
pepo la ngono, leo ninalia tena kwa kuambiwa nauza madawa ya kulevya,
eee Mungu nisaidie mimi,” alilalamika Wema.
Week Hot newz
-
Tunaendelea kama kawaida katika kipindi chetu, tafakari masomo Dominika, na leo tunatafakari masomo Dominika ya 33 ya mwaka C wa Kanisa...
-
Teach me, Lord Jesus, to be generous: to serve You as You deserve; to give, not counting the cost; to fight, not heeding the wound...
-
Uchunguzi wa mwili wa Askofu Józef Wesolowski, umekamilika na matokeo kwamba amekufa kifo cha kawaida. Kuf...
-
Baraza la Kipapa la Elimu Katoliki limezindua tovuti yake inayotoa habari muhimu kuhusu mchango wa Kanisa Katoliki katika sekta ya elimu ...
-
Reading 1, Romans 6:19-23 19 I am putting it in human terms because...
-
NA OSCAR ASSENGA, TANGA-Tanzania.Gazeti Mtanzania. KATIBU wa Chama cha Watu Wenye Albino Mkoa wa Tanga (TAS), Mah...
-
Mpendwa mwana wa Mungu, tuko tena pamoja katika ile habari ya furaha ndiyo kushirikishana mapendo ya Mungu kwa njia ya meza y...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni