Wakati dirisha dogo la usajili likitarajiwa kufungwa Desemba 15, mwaka huu, Shirikisho la Soka nchini(TFF), limezikumbusha klabu zote kuheshimu kanuni na kuzingatia muda uliowekwa.
Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Boniface Wambura alisema jana kuwa kitendo cha klabu kupeleka mchezaji kwa mkopo katika klabu nyingine hakutoi nafasi ya kusajili mchezaji mpya.
Tamko hilo la TFF lina maana kwamba, Yanga ambayo kwa sasa tayari imeingia mikataba ya kuwasajili kipa Juma Kaseja aliyekuwa huru na kiungo Hassan Dilunga kutoka Ruvu Shooting, haitakubaliwa kumsajili mmoja wa wachezaji hao kwani tayari ilikuwa na wachezaji 29.
"Kama klabu ilisajili wachezaji 30 maana yake ni kuwa, haina nafasi ya kuongeza wachezaji. Kwa upande wa wachezaji wa kigeni (foreign players), tunakumbusha kuwa, kuanzia msimu ujao 2014/2015 watakuwa watatu tu badala ya watano wa sasa," alisema Wambura.
Alisema mpaka jana jioni hakuna klabu hata moja iliyokuwa imeshaingia kwenye mfumo wa TMS kuomba uhamisho wa mchezaji wa kigeni na itakapofika Desemba 15, mwaka huu mfumo huo wa TMS utafungwa.
Week Hot newz
-
Tunaendelea kama kawaida katika kipindi chetu, tafakari masomo Dominika, na leo tunatafakari masomo Dominika ya 33 ya mwaka C wa Kanisa...
-
Teach me, Lord Jesus, to be generous: to serve You as You deserve; to give, not counting the cost; to fight, not heeding the wound...
-
Uchunguzi wa mwili wa Askofu Józef Wesolowski, umekamilika na matokeo kwamba amekufa kifo cha kawaida. Kuf...
-
Baraza la Kipapa la Elimu Katoliki limezindua tovuti yake inayotoa habari muhimu kuhusu mchango wa Kanisa Katoliki katika sekta ya elimu ...
-
Reading 1, Romans 6:19-23 19 I am putting it in human terms because...
-
NA OSCAR ASSENGA, TANGA-Tanzania.Gazeti Mtanzania. KATIBU wa Chama cha Watu Wenye Albino Mkoa wa Tanga (TAS), Mah...
-
Mpendwa mwana wa Mungu, tuko tena pamoja katika ile habari ya furaha ndiyo kushirikishana mapendo ya Mungu kwa njia ya meza y...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni