
Aliyekuwa wakala wa nahodha wa zamani wa timu ya soka ya Taifa (Taifa Stars) na Klabu ya Simba,Ismail Balanga
Wakala huyo ambaye ameibukia katika timu ya Taifa ya Sudan Kusini ambayo inashiriki mashindano ya Kombe la Chalenji inayoendelea jijini hapa, alizungumza jijini hapa na kuanikia kila kitu kuhusu sakata hilo.
Balanga ambaye pia ni wakala wa wachezaji anayetambuliwa na Fifa, alisema kuwa, Watanzania ndiyo waliyompotezea Kaseja nafasi ya kusajiliwa na FC Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Balanga alisema akiwa katika hatua za mwisho ili Kaseja asaini mkataba wa kuichezea FC Lupopo, alipigiwa simu na mmiliki wa klabu hiyo akimueleza kwamba hawamuhitaji tena kipa huyo ambaye amejiunga na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Yanga kwa sababu anadaiwa kuwa na tabia ya "kuuza" mechi.
Kocha huyo ambaye timu yake ya Sudan Kusini ilipoteza mchezo wake wa kwanza kwa kukubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Zanzibar (Zanzibar Heroes), alisema soka la Tanzania limejaa siasa hali ambayo inazidi kuzuia kiwango cha mchezo huo nchini kukua.
"Baada ya Lupopo kukataa kufanya biashara, Kaseja alitakiwa na DC Motema Pembe ya DRC, lakini kuna viongozi wa Simba walipiga simu huko kumsemea maneno mabaya," aliongeza wakala huyo ambaye kabla ya kuachana na harakati za kumsajili Kaseja, alikamatwa kwa kuingia nchini bila ya kibali.
Alisema tabia hiyo ya kusema wachezaji wanahujumu timu, ni mbaya kwa sababu inaondoa hali ya uaminifu wa wachezaji na klabu wanazozichezea.
Kocha huyo aliyesaini mkataba wa miaka miwili ya kuifundisha Sudan Kusini, aliongeza kuwa licha ya 'siasa' hizo, bado hataacha kuwatafutia timu nje ya nchi wachezaji wa Tanzania.
Kwa upande wa Kaseja alipoulizwa , alisema hana muda wa kuzungumzia suala hilo kwa kuwa lilishapita na sasa ni mchezaji wa Yanga.
"Suala la Lupopo ni la muda mrefu na limeshapitwa na wakati na sasa mimi ni mchezaji wa Yanga.
Rushwa inakuwa na pande mbili, mtoaji na mpokeaji mimi sijawahi kutiwa hatiani kwa kosa lolote na kama kuna mtu yeyote aliyewahi kushuhudia nikipokea rushwa ajitokeze athibitishe," alisema Kaseja jana alipopigiwa simu kuzungumzia tuhuma hizo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni