
Hivi karibuni, Baba Mtakatifu Francisko alimtembelea Papa mstaafu Benedikto XVI ili kumtakia kheri na matashi mema ya Siku kuu ya Noeli na kutumia fursa hii kumkaribisha kwa chakula cha mchana, kwenye Hosteli ya Mtakatifu Martha, iliyoko mjini Vatican.
Makatibu muhtasi pamoja na Askofu mkuu Dominique Mamberti, Katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican alialikwa kushiriki pamoja na Monsinyo Bryan Wells mratibu wa shughuli za mjini wa Vatican.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni