![]() |
|
|
|
"Robin Van Persie atakuwa nje mwezi mmoja. Alipata jeraha kwenye paja akipiga kona ambayo ilizaa goli (dhidi ya Shakhtar Donetsk on Tuesday)," Moyes aliambia kikao cha wanahabari kabla ya mechi yao ya Jumapili Aston Villa.
Mholanzi huyo, ambaye amefunga mabao saba katika mechi 11 za Ligi ya Premia msimu huu, alirejea baada ya kuuguza jeraha la mtoki wikendi iliyopita wakati wa
kichapo cha 1-0 nyumbani mikononi mwa Newcastle United.
Kukosekana kwake kutakuwa pigo kubwa kwa Moyes huku United wakijaribu kuziba ufa uliotokana na mwanzo mbaya wa thuluthi ya kwanza ya msimu huu ambao umewaacha wakiwa nambari tisa, alama 13 nyuma ya viongozi Arsenal.
"Ni jambo la kusikitisha kwa sababu nafikiri ukiangalia rekodi yetu tukiwa na Wayne Rooney na Robin kwenye timu, ni nzuri sana na hatujakuwa nao wawili kwa muda sasa karibuni,” Moyes alisema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni