
Wanamichezo pia wamemkumbuka Mandela
Wanamichezo mashuhuri, duniani wametoa rambi rambi zao kwa hayati Nelson Mandela, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 95.
Mohamedi Alialisema: "Maisha ya Mandela yalikuwa na maana kubwa kwa dunia nzima , kwake mwenyewe, kwa taifa lake na dunia nzima.
Mwanasoka mashuhuri Bofya Pele naye amesema "Mandela alikuwa mtu mwenye ushawishi mkubwa sana maishani mwake. Ni shujaa wangu.’’
Mwanamasumbwi Bofya Ali aliongeza kusema kua, atamkumbuka Mandela sana kwa kuwa mtu mwenye roho safi na alichukizwa sana na mambo ya ubaguzi wa rangi pamoja chuki na uhasama.
Aliwatia moyo wengine kufikia mambo waliyoyaona kama yasiyowezekana.''
"Bofya Ali amesema kua Mandela alifunza watu umuhimu wa kuwasamehe wenzao, na leo ameweza kuwa huru.’’
Bofya Tiger Woods, naye ambaye ni mchezaji golfu mashuhuri zaidi duniani, alisema daima atamkumbuka Mandela.
Aliyekuwa nahodha wa timu ya Uingereza, Bofya David Beckham alisema kuwa anamlilia sana Mandela na kuwa yuko pamoja na familia yake. ''Tumepoteza mtu muhimu sana na shujaa wetu,’’ Alisema Beckham.
Naye mkuu wa shirikisho la soka duniani FIFA, Bofya Sepp Blatter, amesema kuwa anaomboleza sana na anahisi uchungu mwingi kufuatia kifo cha Mandela.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni