NDUGU yangu, ninatumaini nimekufikisha mahali pazuri. Hiyo ndiyo
historia ya mshazari wa Kanisa la Wasabato. Kifupi haina mashiko na
mtiririko wa kimantiki. Hata hivyo baada ya kuzaliwa kimtindo namna
hiyo, Kanisa la Wasabato halikubaki moja kifikra na kimtazamo.
Ukilichungulia ndani, Kanisa la Wasabato ni Muungano wa Vikundi vitatu
vya Waadventisti; Kikundi cha Bw. Hiram Edson, kilichosisitiza zaidi
mafundisho ya huduma ya Yesu Patakatifu pa Patakatifu mbinguni, Kikundi
cha Bw. Joseph Bates, kilichosisitiza zaidi kufuata Sabato ya Agano la
Kale na Kikundi cha Bi Ellen G. White, kilichomwona Bi Ellen kama nabii
ambaye unabii wake ni lazima ufuatwe na Waadventisti wote duniani.
Vikundi hivi vilipoungana Waadventisti Wasabato wakapata kujichipusha
duniani. Mwaka 1860, Jina la Seventh Day Adventist lilichaguliwa nalo
likawa jina rasmi la Waadventisti hao. Mei, 1863, katika mkutano mkuu wa
kwanza, uliokuwa na wawakilishi kutoka majimbo yote Marekani, isipokuwa
jimbo la Vermont, kanisa la Wasabato likazaliwa rasmi duniani. Kwa
vyovyote kanisa la Wasabato halikubaki moja isipokuwa liliendelea
kumegekamegeka kiasi kwamba leo hii kuna zaidi ya makundi hamsini ya
Wasabato duniani. Ndugu yangu, niache nikomee hapa hapa. Bila shaka,
niliyoyasema yanatosha Muhtasari Basi, tukipiga muhtasari wa historia ya
Wasabato, tuseme tu kwamba Mwasisi wa Waadventisti Bw. William Miller
(1782-1849) alikuwa ni mkulima Mbaptisti wa Massachusetts. Yeye
alifuatiwa na Bw. Joseph Bates aliyeliamsha wazo la Wakristo kurudi
kwenye Sabato ya Wayahudi ambaye alikuwa bado Mbaptisti. Lakini hatimaye
mshamirishaji mkubwa wa Usabato yaani Bi Ellen G. White alikuwa ni
Mmethodisti. Hatimaye, kwa kuhitimisha sehemu hii, yafaa sote tukumbuke
kwamba makanisa hayo mawili, yaani Wabaptisti na Wamethodisti si
chochote isipokuwa matawi ya Kanisa la Anglikana, kanisa lililoanzishwa
na Mfalme Henry VIII wa Uingereza hapo mwaka 1534 baada ya kukasirika
kukataliwa na Kanisa Katoliki kumwacha mkewe aliyeshindwa kumzalia mtoto
wa kiume. Jumla ya yote haya ndiyo chuki ya Wasabato inayorindima hadi
leo hii hata sisi sote kunyanyasika, pasipo kuwakosea lolote. Lakini
nimeshakuonesha kwamba wameibukia kwenye fedheha ya kutokutimia kwa
utabiri wa siku ya mwisho wa dunia na kutoka hapo wamekuwa wakigeuka
geuka kwa tikitaka nyingi za kindoto ambazo kwazo hawakuwa na haki
kutunyanyasa watu tuliobaki kwenye ukweli wa Agano Jipya. Hayo ndiyo
yanayoitwa majanga, kukosea akosee kiongozi wao kutukanwa tutukanwe
sisi. Si ajabu hiyo? Basi, si kitu, tudumu katika mema na Kanisa letu
jema. Uamuzi wetu tulioufanya si wa kujutiwa. Sisi tunamfuata Yesu
Kristo ambaye tumeagizwa tumsikilize na si mtu yeyote ambaye anataka
kupotosha ukweli wa Kanisa Katoliki (rej. Mk 9:7). Wewe basi fanya
uamuzi sasa, je unataka kuwafuata watu wanaoficha historia yao ya aibu
au unataka kumfuata Yesu kweli kweli? Mimi mwenzio sidanganyiki, labda
wewe. Lakini lisingelikuwa jambo la hekima katika karne hii ya ishirini
na moja. Hii si karne ya kudanganyika wala ya kubaki katika limbikizo la
uongo. Amka usibaki gizani. Funguka na ukweli huu mpya. Yesu alikuja
kutukomboa (rej. Luka 4:18-19). Wasabato wanaolitusi Kanisa wanaweza
kuitwa Mitume wa Matusi Dhidi ya Kanisa la Kweli. Msomaji wangu, bila
shaka umeiona historia ya na zigzaga ya Wasabato. Wenyewe wanaificha
sana historia hiyo, hasa kwa wafuasi wao wanaoingia katika kanisa lao
ili wasijue undani wao. Wanakatazana kusoma vitabu vilivyoandikwa na
wasio wasabato na hata jibu kama hili hawaruhusiwi kulisoma. Wanaogopa
ukweli kutoka nje. We acha wafiche, lakini sisi tunajua na leo
nimekuambia ukweli kuhusu historia yao! Umeshaona? Kifupi historia yao
isiyoeleweka ipo katika mizizi mitatu. Mosi, mambo yameanzia kwenye
kuthubutu kutabiri tarehe, siku na saa ya mwisho wa dunia, mambo
yasiyoweza kutabirika na mwanadamu yeyote. Pili, mafundisho mengine
yamejengwa kwenye ndoto za kuota kuweko kwa hekalu mbinguni, wakati
Maandiko Matakatifu yanasema mbinguni hakuna hekalu. Hatimaye, tatu,
ndoto na mafundisho yenyewe yanapingana na Bwana wa Ukristo. Yesu
alifundisha amri kuu ni upendo, wakati waota ndoto hao wanasema ni
kuishika sabato. Wao wanasema hayo kama nani? Kama huo si upinga Kristo
ni kitu gani, ndugu yangu msomaji? Hivi ndugu zangu wanachuo wa Chuo cha
Udaktari, KCMC, Moshi na wasomaji wengine wote, kile mlichosikia kwamba
Kanisa la Sabato lilianza kwa kufunika aibu ya utabiri wa tarehe ya
mwisho wa dunia ambao haukutimia ni kweli kabisa. Historia ya Kanisa la
Sabato ndiyo hiyo niliyowadadavulia ijapokuwa labda kwa ufupi tu.
Ipuuze, ni historia ya aibu na ndiyo kisa inafichwa. Yaani kama
ulivyonifuatilia, ni historia isiyo na kichwa wala miguu, achana nayo
kabisa. MWISHO Mwandishi ni Padri, Mtaalamu wa Biblia na Gombera wa
Seminari Kuu ya Peramiho iliyopo katika Jimbo Kuu Katoliki la Songea
Week Hot newz
-
Tafakari ya Neno la Mungu Jumapili ya IV ya Mwaka C wa Kanisa. - OSS_ROM 28/01/2016 14:25 Mitandao ya kijamii: “...
-
Rubani msaidizi, Andreas Lubitz, aliangusha makusudi ndege hiyo kwenye milima ya Alps. Wachunguz...
-
Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI, Ijumaa, tarehe 27 Desemba 2013 amemtembelea Papa Francisko na kupata chakula cha pamoja...
-
Watawa wa Mama Theresa wa Calcutta waliouwawa huko Yemen ni mashuhuda wa upendo na wahanga wa utandawazi usiojali wala kuguswa na maha...
-
Yesu amekuja ulimwenguni ili kuufunua, kuutangaza na kuus...
-
Daily Reading for Tuesday, March 22nd, 2016 Reading 1, Isaiah 49:1-6 1 Coasts and islands, listen ...
-
Watu 6 wamejeruhiwa katika mlipuko uliotokea katika uwanja wa ndege ulioko mjini Beledweyne nchini Somalia.
-
By Paskal Linda (Batarokota Network ) Feast Day October 22 With St. John Paul II feast day just around the corner, T...
-
Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya maadhimisho ya Ib...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni