
Albam hiyo iliyobeba nyimbo 12 ilizinduliwa siku ya Idd Al- Haji katika ukumbi wa Hock Up, jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashabiki lukuki kutoka ndani ya Nchi na Nchi jirani ya Kenya.
Katika uzinduzi huo Nakaaya alisindikizwa na wasanii mbalimbali akiwemo Naaziz kutoka Kenya, G Nako, Hisia, TID, Chid Benz na wengine.
Akizungumza na Tanzania Daima, Naakaya alisema sababu iliyofanya atoe albam hiyo kama zawadi kwa mtoto wake, ni kwa kuwa yeye ni Baraka kwake hata kama akiwa yupo mbali nae atakuwa na matumaini pamoja na faraja.
“Nawashukuru sana watu wa Arusha, wamenisapoti sana tofauti na nilivyotegemea, walijitokeza kwa wingi sana, nimefurahi nimeanza vizuri, ninaomba waendelee kunisapoti,” alisema.
Nakaaya ni dada wa mshindi wa taji la mrembo wa Afrika kwenye mashindano ya dunia ‘Miss World Africa’ na Miss Tanzania 2005, Nancy Sumari.