
Dar es Salaam.
Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) limemfungulia mwandaaji wa shindano la urembo la Miss Tanzania, Lino International Agency baada ya kuomba radhi na kufanyia kazi baadhi ya mapungufu yaliyojitokeza na kutekeleza masharti aliyopewa.
Akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo,
Godfrey Mngereza amesema LINO International Agency imepewa kibali cha
muda kisichozidi miezi minne kwa ajili ya maandalizi ili kukamilisha
usajili wa mawakala katika ngazi husika.
Mngereza
amesema kuwa mapungufu yaliyobainishwa ni pamoja na kutofuata sheria
,kanuni za uendeshaji matukio ya sanaa nchini ,kutokuwakilisha nyaraka
mbalimbali za shindano lake na mikataba ya washirki,kutumia mawakala
ambao hawajasajiliwa na kupewa vibali na Baraza la sanaa la Taifa.
Amesema
miongoni mwa mapungufu yaliyofanyiwa kazi na Kampuni ya Lino ni
mchakato wa kusajili mawakala na kufanyia marekebisho kanuni na
taratibu za uendeshaji wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania.