Staa wa Bongo fleva na mziki wa asili ya Kitanzania Batarokota
“Kiukweli kwenye sanaa tumeanza kwenda kwenye njia mbaya sana,aina hii ya ushabiki wa mtindo wa uadui itatupeleka pabaya sana..Mashabiki wa Ali Kiba , Wema sepetu na Diamond wanapaswa kuliona mapema tatizo hili,” alisema mkali huyo wa bongo fleva na nyimbo asili Batarokota.
Aidha , Batarokota amewaomba mashabiki wake kujiandaa kuipokea nyimbo yake mpya ya ccm ju ambapo ndani ya songi hiyo amewashirikisha na wasanii L.L. J kutoka Rwanda na Castol kutoka DRS, “Ni songi kali sana itakayowavunja mbavu na kuwafundisha naomba muinunue itakapotoka”.