Nyota wa muziki wa Bongofleva na mziki wa asili ya Kitanzania, Batarokoa akisoma somo katika kanisa la Mt Patric Morogoro.
Nyota wa muziki wa Bongofleva na mziki wa asili ya Kitanzania, Batarokota, amesema nje ya kazi yake ya sanaa ni mchoraji mzuri wa picha asili na mpambaji wa nyumba kwa mitindo ya kiasili na alikuwa akifanya kazi hiyo tangu akiwa shuleni.
Batarokota, ambaye hivi jana alitawala vichwa vya habari vikitaharifu ya
kwamba amejiunga na chama cha siasa cha ACT-Wazalendo, amesema
hadi sasa bado anaipenda kazi hiyo ya kuchora na anazidi kujifunza
mambo
mbalimbali yanayohusu zana za kale kwa sababu ndiyo mambo anayoyapenda.
Msanii wa Bongo fleva na nyimbo za asili ya Kitanzania Batarokota wa pili kushoto akiwa na meneja wako Alon kwa kushoto na Mr Kwiproducer wakiwa kwa shaga ya amani
Alisema wakati alipokuwa shuleni alikuwa maarufu sana kwa uchoraji na
mcheza ngoma za kisukuma na alikuwa mwalimu wa wanafunzi wenzake na
watu wengine, na licha ya kwamba alikuwa
analipwa ujira mdogo, alikuwa anafurahi kuona watu waliomzunguka
wamependeza na michoro yake.
"Walikuwa wakinilipa pesa ndogo Sh. 500 tu, lakini nilikuwa napenda
kuchora na walikuwa wanapendeza hivyo, hali hiyo iliendelea hata
nilipokuwa nyumbani. Kuchora na ngoma ni vipaji vyangu , ndiyo maana
najitahidi sana niwe na shule ya sanaa," alisema Batarokota.
Batarokota alisema angeweza kuwa na shule ya sanaa za kale na
mababu,"Unajua mimi jina langu kwa sasa ni kubwa na thamani yake pia ni
kubwa, hivyo siwezi kusema nifungue tu kijishule. Napaswa kufungua
shule ya Kimataifa kubwa yenye sifa kama ya jina mababu zetu kwama
Mwanamarundi, na wengine wengi, kiasi kwamba hata mtu
akiangalia na kuambiwa hii shule ni sanaa za makabila makubwa akubali
na kusema 'yes'