Batarokota Gospel Media !
Sanduku la Agano na huruma ya Mungu! Utuombee!
Week Hot newz
Batarokota asema kipindi cha mapumziko ni muhimu na wala si uvivu
Kipindi cha mapumziko baada ya kazi, ni zawadi ya thamani ambayo Mungu alifanya kwa familia ya binadamu", ambayo haipaswi kupita au kupuuzwa katika mipango ya utendaji wa familia na mtu binafsi . Ni maelezo ya msanii wa nyimbo za asili nchini Tanzania Batarokota aliyoyatoa jana jumatano wakati wa kuinjilisha katika kanisa la Mt Bakita Oilcom nane nene Mjini Morogoro. msanii Batarokota alitoa wito kwa familia kuiishi kama inavyotakiwa Siku ya Mapumziko ya Jumapili, kwa kushiriki katika Ibada ya Ekaristi inayobadili kila wakati wa maisha, hata wakati wa uchungu. Batarokota akitafakari umuhimu wa mapumziko ya baada yakazi, alisema, mapumziko yaliwekwa na Mungu mwenyewe,kama nafasi ya kutafakari uzuri wa kile kilichofanyika au kuumbwa kama Mwenyezi Mungu mwenyewe alivyofanya baada ya kuiumba dunia na vyote vilivyomo. Na hivyo mapumziko inakuwa nafasi nyingi wazi ya kufikiria pia jinsi ya kusonga mbele kwa mafanikio zaidi katika kazi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Chapisho Jipya
Taarifa za zamani
Nyumbani
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni