
Papa Francisko akimpokea Waziri Mkuu Kuwait Sheik Jaber Mubarak Al-Hamad Al Sabah - ANSA
(Vatican Radio) Jumatano, Septemba 10, 2015, Papa Francis alimpokea na kuzungumza nae , Waziri Mkuu wa Kuwait, Sheikh Jaber Mubarak Al-Hamad Al-Sabah.
Katika mazungumzo yao ya kirafiki , waligusia mandhari mbalimbali ya maslahi kwa pande zote ikiwemo michango chanya ya kihistoria ya Wakristo wachache miongoni mwa jamii Kuwait. Na pia walilenga umuhimu wa elimu katika kukuza utamaduni wa kuheshimiana, mshikamano na ujenzi wa amani kati ya watu tofauti na wenye dini tofauti.
Baada ya Kukutana na Papa, Waziri Mkuu Sheikh Jaber na ujumbe wake alikutana na Katibu wa Nchi wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin,akiwa amefuatana Askofu Mkuu Paulo Ghallager , Mkuu wa Idara ya mahusiano ya nchi za nje wa Vatican. Lengo la kukutana kwao ilikuwa kutia saini katika Mkataba wa Maridhiano kati Sekretarieti ya Nchi ya Vatican na Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi ya Kuwait . Utiaji huo wa saini, ulifanywa na Askofu Mkuu Paulo Gallagher na Waziri Sheikh Sabah Khalid Al-Hamad Al-Sabah, Naibu Waziri katika waziri wa Mambo ya Nje, Kuwait.
Taarifa inataja kuwa Mkataba huo, unawezesha utendaji thabiti zaidi kwa pande zote mbili, kuimarishwa zaidi na kuwa na mahusiano thabiti baina ya nchi, katika kushirikiana , kuheshimiana, kujenga amani na utulivu wa kikanda na kimataifa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni