Week Hot newz

Batarokota: Sijawahi kutumia dawa za kulevya

Pichani juu kutoka kushoto Daniel Renatus akiwa na Msanii wa bongo fleva na mziki wa asili ya kitanzania Batarokota.
 
Nyota wa muziki wa kizazi kipya na mziki wa asili ya Kitanzania , Batarokota, aliyetamba na nyimbo za 'kwejanga nyangisha' na 'sauti ya haki ', amekanusha tuhuma mbaya zinazomzunguka kwamba anatumia dawa za kulevya.
 
Akizungumza na  'http://batarokota.blogspot.com/' leo asubuhi, msanii Batarokota alisema anahisi kufananishwa kwake na nyota wa Bongofleva,  'Chid Benz' aliyekuwa akitumia dawa hizo huenda ndiyo chanzo cha kuzushiwa kashfa hiyo. 
 
"Kiukweli mimi situmii dawa za kulevya hata kidogo, na huwa naumia sana ninapoambiwa taarifa hizi, sijui hata ladha yake, ila nadhani watu wanakuwa wakinifananisha, unajua mimi huwa nafananishwa sana na Chib Benz, hivyo labda ndiyo sababu ya kuwapo kwa taarifa hizi mitaani, ila kiukweli mimi si mtumiaji wa dawa za kulevya," alisema.
 Pichani juu kutoka kushoto msanii Shingwengew  akiwa na Msanii wa bongo fleva na mziki wa asili ya kitanzania Batarokota
 
Batarokota, msaniii huyo ambaye sasa anatarajia kuachia wimbo mpya, amesema nje ya kazi yake ya muziki kwa sasa anafanya biashara ya urembo wa kiasili  kama uchuraji na kutengeneza mavazi  kama njia ya kujiongezea kipato.