Week Hot newz

Baada ya Marekani Papa kuitembelea Afrika Mashariki na Kati


TOLEO 39.indd
Rais Kenyata asema ni Papa atakayeiunganisha Kenya kuwa kitu kimoja


Na Paskal Linda -Nairobi, Kenya


NCHI za Kenya  na Uganda zimeeleza shauku ya kumuona Papa Fransisko. Akizungumza na batarokota.blogspot.com, Mratibu wa Mawasiliano Baraza la Maaskofu Kenya (KCCB) David Omwoyo amesema kuwa, wananchi wa Kenya wanashauku ya kumuona Papa Fransisko kwani hiyo ni ziara ya kihistoria kwa nchi hiyo.
“Maandalzi kwa upande wa Kanisa yamekamilika na upande wa serikali imejiandaa vyema kwani hata serikali imetuma ujumbe kwamba imejipanga kumpokea Papa Fransisko ambaye licha tu ya kuwa kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani ni Rais wa nchi ya Vatikani,” ameeleza Omwoyo.
Aidha ameeleza kuwa, licha ya Papa kuitembelea Kenya ataitembelea pia nchi ya Uganda hivyo ugeni huo unageuka kuwa wa nchi za Afrika Mashariki.

Aidha serikali ya Kenya ilituma ujumbe kwenye ofisi za Mawasiliano KCCB ikieleza kuwa, serikali ya Kenya inayoongozwa na Rais Uhuru Kenyata iko makini kumpokea Papa Fransisko ambaye wana matumaini kwamba ataleta hamasa ya umoja na mshikamano baina ya wakenya.
“Baba Mtakatifu anakuja kututembelea kama kondoo zake, kuimarisha imani yetu na kututia moyo wa imani katika kutekeleza majukumu yetu kwa jirani na kujitoa sadaka kwa ajili yaw engine,” umeeleza ujumbe huo.
Omoyo amesema, Papa akiwa Kenya kwa siku hizo tatu, atafanya mazungumzo binafsi na Rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyata, atakutana pia na viongozi wa serikali ya Kenya na Maafisa Mazingira wa Umoja wa Mataifa na kuhutubia wajumbe wa kidiplomasia nchini humo.
“Papa atakutana pia na viongozi wa dini mbalimbali wakiwemo wakristo, waislamu, Hindu na viongozi wa jadi, vijana na kuongoza Ibada ya Misa Takatifu ambapo atahutubia taifa la Kenya.
Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Katoliki Uganda Askofu John Baptist Odama ameeleza kuwa, Kanisa nchini Uganda limejiandaa kwa ujio huo Mtakatifu.“Akiwa nchini Uganda, Papa ataungana na waamini kusherehekea Yubilei ya Dhahabu ya kutangazwa watakatifu Mashahidi wa Uganda 22.”

Baraza la Maaskofu Kenya laweka mikakati ya ujio huo.
Kamati ndogo ya Tume ya Mawasiliano na Matangazo ya Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya, imetoa baadhi ya mikakati mbinu, kwa ajili ya maandalizi ya ziara ya Papa Francisko nchini Kenya, mwezi Novemba mwaka huu.
Mratibu wa Mawasiliano wa KCCB, David Omwoyo amesema kuwa, tovuti maalum kwa ajili ya ziara ya Papa itazinduliwa katika siku chache zijazo. Na pia hivi karibuni, nembo ya ziara ya Papa itazinduliwa hivi karibuni.
Nembo hiyo ina alama 4 muhimu zinaashiria mada mbiu ya ziara: “Simama imara katika Imani … Usiogope.” Vitu hivyo vinne ni Njiwa kama alama ya amani, moto katika nafasi ya Roho Mtakatifu, ramani ya Kenya na Msalaba ambayo ni ishara ya Kanisa.
Na kwamba, kwa ajili ya kuwaandaa watu , katika kipindi hiki cha kusubiri ujio wa Papa, Kamati ndogo ya Mawasiliano imeunda mpango mpya wa utendaji kwa miradi maalum, inayolenga kufanikishaji wa ziara ya Papa kiroho na kijamii.
Miradi inayoendeshwa na Kanisa Katoliki Kenya ambayo itatagazwa kupitia vituo vya Televisheni. Aidha, kutakuwa na mengi yatakayotangazwa na vyombo vya habari kwa wakati huu.
Taarifa zote zitakuwa zinapatikana katika tovuti mpya itakayozinduliwa hivi karibuni, ikiwa wazi kwa mtu yeyote ambaye anayetaka kupata habarii za ujio wa Papa Kenya. 

Papa Fransisko anatazamia kuitembelea Afrika ambapo atatembelea nchi ya Kenya Novemba 25 hadi 27, Uganda Novemba 27 hadi 29 na Jamhuri ya Afrika ya Kati Novemba 29 hadi 30 Mwaka huu.