
Papa Francis katika Ibada ya misa Takatifu ya Mkutano wa Dunia wa Familia - ANSA
Papa alisema kweli huo unaleta mshangao; kwani Musa na Yesu wote wana uwezo wa kukemea. Yesu alikutana na vizingiti kutoka kwa watu wake ambao hawakupokea kile alichokuwa akisema na kufanya. Maneno yake yalipokelewa na watu wale walikuwa wazi na waaminifu na wa kweli katika imani ya wanaume na wanawake wengi ambao hawakuwa sehemu yoyote ya wateule wa Mungu.Aliongeza Papa ya kwamba wanafunzi katika sehemu yao walitenda kwa imani yao njema.
Lakini majaribu na mashaka yao yalikuwa kuhusu uhuru wa Mungu ambaye uwanyeshea mvua watu wote wanyoofu na wasio na haki (Mt 5:45), yaani wale wenye urasimu , wenye madaraka na duru za ndani , wanaotishia ukweli wa imani na kwa hivyo ni lazima kwa nguvu kukataliwa.
Lakini Papa akabainisha ya kwamba Mara sisi tunapolitambua , tunaweza kuelewa kwanini maneno ya Yesu yalileta kashfa miongoni mwao. Ukweli wa Yesu haujali kashfa za kila kitu ambacho ujaribu kuvunja na kuharibu imani yetu katika kazi ya roho! Mapenzi ya baba hayataisha kamwe ya kuendelea na ukarimu wake wa kupanda .Yeye utawanya mbegu za uwepo wake katika dunia yote , kwa maana upendo wake unasisitiza hivyo ya kwamba siyo sisi tuliyompenda Mungu bali kwamba Munga alitupenda yeye kwanza (Yn 4:10)
Upendo wake unatupqtia uhakika ya kwamba Mungu ametuchagua , na anatusubiri .Na hii ndiyo inawapa wanafunzi wake kuhamasika , na kutoa huduma ya kutenda mambo yaliyo mema yanayotekea kwa majirani zao wanao wazunguka. Kwani Mungua anataka watoto wake wote washiriki katika sikukuu ya Injili. Ni watu wangapi walioko pale katika madhimisho ya Familia; papa alisema: Hii peke yake ni jambo la unabii , ni aina ya miujiza katika dunia ya leo, wote wanaweza kuwa manabii, wote wanaweza kufungulia miujiza ya upendo kwaajili ya familia zote za dunia, na hivyo kushinda kashfa nyembamba, upendo mdogo uliojifungia ndani yake yaani ubinafsi.