
Mapema Ijumaa hii 25 Septemba 2015,
Baba Mtakatifu alitembelea Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa yaliyoko
mjini New York, na kuwahutubia wafanyakazi wote wa Ofisi hizo za Makao
Makuu ya Umoja wa Mataifa. Katika hotuba yake fupi, Papa aliwashukuru
kwa dhati na kuonyesha furaha yake kuwa mahali hapo. Aliwatia nguvu
akiwataja kwamba wote wake kwa waume, wao ni uti wa mgongo wa chombo
hiki muhimu cha Kimataifa.
Baba Mtakatifu Francisko akihutubia wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa mjini New York 25.09.2015 -
Baba Mtakatifu Francisko akihutubia wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa mjini New York 25.09.2015 -
Papa aliwashukuru wote kwa moyo wa dhati, kwa kila jambo wanalolifanya kwa manufaa ya wote na hasa kwa majitoleo yao ambayo si tu huchangia katika ufanikishaji wa kazi za Umoja wa Mataifa, lakini pia zenye kuwa na maana kubwa, pia kwao wenyewe binafsi. Papa alisema jinsi mtu anavyofanya kazi zake huonyesha pia heshima ya mtu mwenyewe alivyo.
Na kwamba wengi wao wametoka katika nchi mbalimbali duniani kote. Na hivyo wanakuwa mfano wa jinsi watu mbalibmali wanavyoweza kuungana na kuwa kitu kimoja katika utumishi kwa manufaa ya wote, na hasa kwa jinsi wanavyoonyesha ustawi wa watoto kupitia mipango mbalimbali ya elimu na lishe. Na pia katika kujali mustakabali wa dunia na vizazi vijavyo.
Papa alieleza na kutoa ombi kwa kila mmoja wao, akimtaka bila kujali hadhi yake, wajenge umoja na mshikamano, wakihudumiana mmoja kwa mwingine. Kufanya kazi zao kwa ukaribu zaidi na zaidi katika hali za kuheshimiana na umoja kati yao ili shirika hili liwe mfano wa familia ya binadamu , yenye kuishi katika hali ya mapatano na maelewano si tu kwa ajili ya amani lakini katika amani , kufanya kazi si tu kwa ajili ya haki lakini katika roho ya haki.
Papa alieleza na kuwahakikishia kwamba kila mmoja wao yumo ndani ya moyo wake . Na kwamba atatolea sala zake kwa ajili yao na familia zao na akawaomba wao pia wamkumbuke katika sala zao .Na kama kuna wasioamini basi amewaomba wamtakie yaliyo mema. "Mungu awabariki wote. Asante" alimalizia Papa Francisko na kupigiwa makofi mengi .