“Katika
Waraka Uso wa huruma, maalum kwa ajili ya kuzindua Maadhimisho ya Mwaka
Mtakatifu wa Jubilei ya huruma ya Mungu niliwaomba kwamba ‘Kwaresima ya
Mwaka huu tuiishi kwa uzito zaidi kama muda mahsusi kwa kuadhimisha na
kuonja huruma ya Mungu. Ni kurasa ngapi za Maandiko Matakatifu, zinaweza
kutafakariwa katika majuma ya Kwaresima kwa lengo la kutusaidia
kuugundua tena uso wa huruma wa Baba!”
Kwa kifungu hiki cha maneno
ndivyo Baba Mtakatifu Francisko anavyoanza ujumbe wake wa Kwaresima kwa
mwaka 2016. Ni nukuu ambayo inatuelezea kwa kifupi kabisa maana na
makusudi ya kipindi hiki katika mwaka wa Kanisa, yaani, ni majira
yaliyowekwa mahasusi kabisa kwa kumrudia na kujipatanisha na Mungu kwa
kufanya toba na wongofu wa ndani.Katika Dominika hii ya kwanza ya Kwaresima, Mama Kanisa anatuwekea
mbele yetu tafakari juu ya ushawishi wa shetani ambaye daima anatutafuta
na kutushawishi kusudi tuweze kuacha kuutafuta uso wa huruma ya Mungu
na kuingia katika dhambi.
Lakini pia tunaoneshwa namna ya kumshinda huyu
shetani na kumpatia Mungu utukufu. Hii ni tafakari nzuri tunayoanza
nayo katika kipindi hiki cha toba kusudi tuweze kutambua kinagaubaga juu
ya njia na mbinu za huyu muovu na kutafuta njia za kumwepa, yaani
kutafuta namna ya kujishikamanisha zaidi na Mungu na kumkimbia shetani,
na kwa kweli hili ndilo lengo la kipindi hiki cha Kwaresima. Mambo
matatu yanatajwa katika Injili ambayo yanakusanya kwa ujumla vishawishi
vyote vya mwovu shetani. Mambo hayo ni matamanio yetu ya kimwili, tamaa
zetu katika mali za kidunia na tamaa zetu katika madaraka.
Mwili wetu huwa unapatwa na njaa za kila aina ambazo kwa bahati mbaya
hutufumba macho na kushindwa kuyaona mapenzi ya Mungu. Tupo tayari
kukurupusha ahadi zetu za ubatizo kusudi tuweze kujituliza na adha za
kiulimwengu ambazo hupita baada ya kitambo. Hii ni changamoto inayowekwa
mbele yetu ili kuona kwa jinsi tunavyomwacha Mungu na neno lake na
kuchuchumilia faraja za kiulimwengu. Mali ni tamanio la kila mwanadamu.
Watu wengi huangaika kwa ajili ya kutafuta kujilimbikizia mali. Utajiri
huu wa kidunia hutugeuza kuwa waabudu wa nguvu za giza na kupoteza
upendo wetu kwa Mungu na jirani zetu. Leo hii tunawaua ndugu zetu wenye
ulemavu wa ngozi kwa ajili ya kupata mali; leo hii tunawanyonya watu
haki zao za msingi kusudi tu tuzidi kujilimbikizia utajiri. Badala ya
kuwa na furaha au uhuru tunafanywa kwa watumwa wa mali za kidunia.
Madaraka na vyeo vya kidunia hutufanya tujione kuwa ni miungu katika
jamii. Mwanadamu wa leo anachuchumilia nafasi hizi za kimadaraka ili
kupata jina kubwa na umaarufu kati ya watu.
Changamoto zote hizi tatu hutuweka mbali na Mungu. Kristo leo hii
anakuja kwetu kama mfano wa namna ya kuzishinda na kumpatia Mungu
utukufu. Mtume Paulo anatuambia katika somo la pili kwamba “ukimkiri
Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa
Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka”. Bwana wetu Yesu Kristo
anajidhihirisha kwetu kwamba Yeye ndiye njia tunayopaswa kuifuata katika
kupingana na shetani na kumtii Mungu. Alikuwa tayari kuitii sauti hiyo
ya Mungu hadi akapokea kifo cha Msalaba. Kwa njia yake nasi tuliopokea
hadhi ya kuitwa waana warithi wa Mungu tunaalikwa kujiweka katika hali
ya kugutuka na kuiepa mitego ya shetani katika juhudi zetu zetu za kila
siku za kumtukuza mwenyezi Mungu kwa maisha yetu.
Tunalojifunza kwa Kristo ni fadhila ya unyenyekevu. Kinyume cha
fadhila hii ni kiburi na majivuno. Kristo anatuonesha kwamba ni kwa njia
ya kuwa tayari kujishusha na kujitambua nafasi yako mbele ya Mwenyezi
Mungu na kuanza kuhusiana naye kama Baba yetu mwema. Yeye anatupenda
daima na ulimwengu wote aliouumba vizuri ametukabidhi ili kuuratibu
vema. Tunapaswa kumpatia Yeye heshima inayomstahili kwa sala zetu za
shukrani na kwa sadaka zetu na tutalifanikisha ili pale tu tutakapokuwa
tayari kuyafanya yale yaliyo mapenzi yake. Leo hii tunajiondoa katika
hadhi hii nzuri ya kuwa watoto wa Mungu. Tamaa zetu za kidunia
zinatufunika kiasi cha kushindwa kuuona wema wa Mungu. Tunapata wapi
wasiwasi wa kuwa na ulimwengu huu na mali zake wakati mwenyezi Mungu
mwenyewe amekwisha tupatia tuutunze? Hapa kweli ndipo tunapopaswa
kuistukia kazi ya adui mwovu shetani.
Mwanadamu anapomkaidi Mungu anaingia katika hali ya utumwa.
Sehemu ya
kwanza ya somo la kwanza inalionesha ili kwa njia ya ishara ya Taifa la
Israeli ambao walikuwa taifa teule la Mungu lakini pale waliamua kwenda
kukaa ugenini Misri waliishia kuwa watumwa karibu kupotea. Lakini
sehemu ya pili ya somo hilo inatufunulia uso wa Baba mwenye huruma
ambaye anashuka na kuwarudishia tena utu wao wale aliowachagua, wale
aliowapenda. Hapa tunapata kwa ufupi mwaliko wa toba na wongofu wa ndani
tayari kuambata huruma ya Mungu. Mungu wetu mwenye huruma alitupatia
nchi ya ahadi iliyo na kila aina ya wema wake, lakini bado tunataka
kukimbilia ugenini ambako tunaishia katika utumwa: tunakuwa watumwa wa
pesa na madaraka, watumwa wa vyeo na umaarufu, watumwa wa tafrija na
anasa na mengineyo mengi ya kidunia yanayotufunga. Fungua macho yako,
ikimbilie huruma ya Mungu.
Antifona ya mwanzo ya Dominika hii inatupatia maneno ya matumani:
“Ataniita nami nitamwitikia; nitamwokoa na kumtukuza; kwa siku nyingi
nitamshibisha.” Ni mwaliko huo wa mwenyezi Mungu, Baba yetu mwenye uso
wa huruma ambaye yupo tayari mlangoni kutupokea, kutubusubusu,
kutusafisha na kutuvisha vazi lililo bora zaidi. Mtume Paulo alitualika
siku ya Jumatano ya majivu: “Wakati uliokubalika nalikusikia, siku ya
wokovu nilikusaidia; tazama, wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama,
siku ya wokovu ndiyo sasa”.
Ndiyo wakati huu wa Kwaresima na kwa namna
ya pekee katika mwaka huu wa huruma ya Mungu. Tuikimbilie basi huruma
hii ya Mungu kwa toba, tumrudie Mungu wetu kwani daima yupo tayari
kutupokea.
Tafakari hii imeletwa kwako na Padre Joseph Peter Mosha.
Week Hot newz
-
Tafakari ya Neno la Mungu Jumapili ya IV ya Mwaka C wa Kanisa. - OSS_ROM 28/01/2016 14:25 Mitandao ya kijamii: “...
-
Rubani msaidizi, Andreas Lubitz, aliangusha makusudi ndege hiyo kwenye milima ya Alps. Wachunguz...
-
Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI, Ijumaa, tarehe 27 Desemba 2013 amemtembelea Papa Francisko na kupata chakula cha pamoja...
-
Watawa wa Mama Theresa wa Calcutta waliouwawa huko Yemen ni mashuhuda wa upendo na wahanga wa utandawazi usiojali wala kuguswa na maha...
-
Yesu amekuja ulimwenguni ili kuufunua, kuutangaza na kuus...
-
Daily Reading for Tuesday, March 22nd, 2016 Reading 1, Isaiah 49:1-6 1 Coasts and islands, listen ...
-
Watu 6 wamejeruhiwa katika mlipuko uliotokea katika uwanja wa ndege ulioko mjini Beledweyne nchini Somalia.
-
By Paskal Linda (Batarokota Network ) Feast Day October 22 With St. John Paul II feast day just around the corner, T...
-
Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya maadhimisho ya Ib...