Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya maadhimisho ya Ib...
Breaking newz: Bomu la laptop lalipuka Somalia
Watu 6 wamejeruhiwa katika mlipuko uliotokea katika uwanja wa ndege ulioko mjini Beledweyne nchini Somalia.2 kati ya wale waliojeruhiwa ni maafisa wa polisi huku wengine wakiwa raia.
Bomu hilo linaaminika kuwa lilikuwa limetegwa ndani ya kipakatilishi (laptop).
Mtu
aliyekuwa ameibeba bomu hilo alikuwa anajaribu kuingia katika eneo
salama katika eneo la upekuzi la Beledweyne takriban kilomita 325km nje
ya Mogadishu.
Mwezi uliopita,kundi la kiislamu la Al-Shaabab
lilidai kutekeleza shambulizi lililosababisha shimo kutokea katika ndege
moja ya abiria.Shambulizi hilo lilitekelezwa na bomu lililotegwa ndani ya kipakatilishi (laptop).
''Afisa
wa ulinzi katika eneo hilo Luteni Kanali Ali Dhuh Abdi amesema kuwa
bomu hilo lililipuka kisha maafisa wa usalama wakaharibu mabomu mengine 2
yaliyokuwa yametegwa ndani ya kipiga chapa (printer)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni