Week Hot newz

Batarokota: Uibilisi zimetutenga na huruma ya Mungu

 Batarokota wa pili kushoto akiwa na rafiki zake 
 
MSANII wa Bongo Fleva na nyimbo asili ya Kitanzania, Paskal Linda ‘Batarokota’, amesema kukithiri kwa matumizi ya dawa za kulevya, utoaji mimba, ufisadi, choyo, dhuruma, kutosamehana katika jamii zinazo tuzunguka kunatukosesha na huruma ya Mungu.

“Mimi binafsi nashindwa kuelewa kwanini jamii inayotuzunguka tunajitumbukiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya, utoaji mimba, utumiaji dawa wa kuzuia mimba, utumiaji wa kondomu,  ufisadi, choyo, dhuruma,uuaji, uzinzi, uasherati,  na kila siku tunafanya lakini tumeshindwa kumrudia Mungu wa huruma kwa kuomba toba kwa Mungu wa huruma, inabidi tupigane kwa pamoja kwa nguvu moja kukataa uibilisi kwa kutumia hata mitandao ya facebook, blogu,tovuti twitter, au kutumiana sms za mafundisho kwa simu, huku tukishirikishana sisi kwa sisi kumuomba Mungu toba kila siku na upendo wake wa Kimungu  ili uwe nasi” alisema Batarokota.

Batarokota akizungumza leo na mwandishi wa blogu hii leo asubuhi baada ya kuudhuria misa katika kanisa la St Josephine Bakhita Oilcom nane nane Morogoro,  aliongeza kwa wanajamii ya Mungu na watoto wa baba mmoja,  wana nafasi kubwa kwa kutumia mitandao kukemea uovu na mambo yasiyo kuwa na utukufu wa Mungu.

“Kinachotakiwa kwa sasa, wanajamii wote tumie fursa za kushirikishana kwa njia ya mitandao ya kijamii kutangaza habari njema, siyo kujiingiza katika matumizi au uuzaji wa dawa za kulevya,utoaji mimba, uchoyo, ulevi wa chakula, pombe na madaraka, ’’ alifafanua Batarokota.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni