Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya maadhimisho ya Ib...
Mwanamke wa miaka 72 ajifungua mtoto India
Mwanamke wa umri wa miaka 72 amejifungua mtoto mvulana katika hospitali moja nchini India.Mwanamke
huyo alipachikwa mimba kupitia njia ya kitaalamu ya IVF ambapo yai la
mwanamke hutolewa kutoka kwenye ovari, kutungishwa mbegu ya kiume na
kisha kurejeshwa kwenye mji wa mimba. Yai hilo linaweza kutolewa kwa
mwanamke mwingine.
Njia hiyo hutumiwa kuwawezesha wanawake tasa kupata watoto.
Daljinder Kaur alijifungua mtoto wake baada ya kupokea matibabu kwa miaka miwili katika hospitali iliyoko jimbo la Haryana.
Matabibu walifanikiwa kumtungisha mimba kupitia IVF mara yao ya tatu.
Mumewe Kaur ana umri wa miaka 79. Kisa hicho kimezua mjadala mkali kuhusu kutumiwa kwa
teknolojia hiyo ya IVF na umri ambao wanawake wanaweza kuruhusiwa
kuitumia kupata watoto.Dkt Kanad Nayar, katibu mkuu wa chama cha
upachikaji mimba nchini India anasema sheria ya kuamua umri wa juu ambao
mwanamke anaweza kuruhusiwa kutumia teknolojia hiyo itatungwa karibuni.
Sana umri huo utakuwa miaka karibu miaka 55.
Daktari huyo anasema jambo la kuzingatiwa zaidi ni uwezo wa mwanamke kumlea mtoto hadi akomae. "Ukimzaa mtoto lazima uweze kumlea mtoto kwa karibu
miaka 20 hivi. Huwezi kujifungua mtoto kisha uwaache watu wengine
wakimlea,” amesema Dkt Nayar.Ni mara ya pili kwa mwanamke mkongwe kujifungua mtoto India. Awali, mwanamke wa miaka 70 alijaliwa mtoto nchini humo.
Lakini mwanamke huyo alifariki miaka miwili baadaye na sasa mtoto huyo anatuzwa na jamaa zake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni