Week Hot newz

Batarokota anawashukuru wadau wa Tasnia ya habari!

Msanii wa Bongo Fleva na Nyimbo asili ya Kitanzania Batarokota, kwa kupitia mitandao ya kijamii leo asubuhi  amewashukuru waandishi wa habari njema  kwa njia ya mitandao mbalimbali.Anawashukuru wale wote waliosaidia kutangaza habari njema kwa njia ya mitandao na wanao endelea kutangaza kila siku,wakati wa raha, uchungu na magumu ya maisha.

Anamshukuru Mungu kwa kuweza kusaidiwa katika maisha na utume wao wote bila kubaguliwa wala kutengwa.Alisema hii ni dhamana kubwa ambayo ilikuwa inawajibisha sana, Batarokota anakiri na kusema kwamba, waandishi wamefanya yote kama mtumishi asiye na faida na ametenda yale aliyopaswa kutenda na kwamba, ataendelea kusikiliza sauti ya wale ambao wanapenda kuandika injili ya Yesu Kristo.

Batarokota anawashukuru na kuwapongeza wale wote wanaojisadaka katika uwanja wa mawasiliano ya jamii; kwa ajili ya huduma kwa jirani zao pamoja na dhamana inayoendana na wajibu huu.

Mwishoni, Batarokota anawatakia wadau wa mawasiliano ya jamii utume mwema.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni