Mabingwa Yanga walishikwa kwa sare ya 0-0 ugenini mkoani Tanga dhidi ya Coastal Union na kushuhudia wakitema uongozi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya Azam FC kushinda 1-0 dhidi ya Rhino Rangers na kushika usukani wa ligi.
Mbeya City ambao waliianza siku ya jana wakiwa na pointi 30 sawa na Azam, nao walidondosha pointui mbili jana kufuatia sare ya 1-1 ugenini Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mabatini.
Matokeo hayo yalimaanisha kwamba Azam sasa wako kileleni mwa msimam