Week Hot newz

Njoo Roho Mtakatifu!



Kumsadiki Roho Mtakatifu ni kukiri Nafsi ya tatu ya Fumbo la Utatu Mtakatifu, atokaye kwa Baba na Mwana na anayeabudiwa na kutukuzwa pamoja na Baba na Mwana. Huyu ndiye Roho Mtakatifu aliyetumwa mioyoni mwa waamini, ili kupokea uzima mpya wa wana wateule wa Mungu. RealAudioMP3

Katika Fumbo la Utatu Mtakatifu usiogawanyika, Mwana na Roho ni Nafsi tofauti lakini hawatenganiki. Tangu mwanzo hadi mwisho wa nyakati, Baba anapomtuma Mwanaye, anamtuma pia Roho wake anayewaunganisha na Kristo kwa imani ili waamini wakiwa wamefanywa waana waweze kumwita Mungu, Abba, yaani Baba.

Siku hamsini baada ya ufufuko wake nidyo Siku kuu ya Pentekoste, Yesu Kristo aliyetukuzwa mbinguni alimmimina Roho Mtakatifu pasi na kipimo, akamdhihirisha kuwa Nafsi ya Kimungu, hivi kwamba, Fumbo la Utatu Mtakatifu limefunuliwa kikamilifu. Utume wa Kristo na ule wa Roho Mtakatifu vilikuwa utume wa Kanisa, lililopelekwa litangaze na kueneza Fumbo la Umoja wa Utatu Mtakatifu.

Kwa ufupi, Roho Mtakatifu anajenga, anahuisha na kutakasa Kanisa. Roho Mtakatifu anawarudishia Wabatizwa hali ya kufanana na Mungu iliyopotezwa kwa njia ya dhambi na anawafanya waishi ndani ya Kristo uzima uleule wa Fumbo la Utatu Mtakatifu. Anawatuma washuhudie ukweli wa Kristo na kuwapanga katika kazi zao maalum, ili wote wazae tunda la Roho.

Hili ndilo Fumbo ambalo linatarajiwa kuadhimishwa na Baba Mtakatifu Francisko katika Siku kuu ya Pentekoste, Jumapili ijayo kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican kuanzia saa 4:00 asubuhi kwa saa za Ulaya, kadiri ya taarifa iliyotolewa na Monsinyo Guido Marini Mshereheshaji mkuu wa Ibada za Kipapa.

Historia ya Kanisa la Sabato (4)

NDUGU yangu, ninatumaini nimekufikisha mahali pazuri. Hiyo ndiyo historia ya mshazari wa Kanisa la Wasabato. Kifupi haina mashiko na mtiririko wa kimantiki. Hata hivyo baada ya kuzaliwa kimtindo namna hiyo, Kanisa la Wasabato halikubaki moja kifikra na kimtazamo. Ukilichungulia ndani, Kanisa la Wasabato ni Muungano wa Vikundi vitatu vya Waadventisti; Kikundi cha Bw. Hiram Edson, kilichosisitiza zaidi mafundisho ya huduma ya Yesu Patakatifu pa Patakatifu mbinguni, Kikundi cha Bw. Joseph Bates, kilichosisitiza zaidi kufuata Sabato ya Agano la

Mwanamke Aadhibiwa kwa kumtelekeza mume


Roseline anadaiwa kuwatelekeza watoto wake wanaoishi na baba yao
Na Paskal Linda-Kenya.
Mwanamke mmoja nchini Kenya ameamrishwa na mahakama kumlipa mumewe shilingi elfu tatu au dola 35 kama hela za kukidhi mahitaji yake na watoto wake kila mwezi.
Mwanamke huyo kwa jina Roselyn Muyonga, ambaye anatuhumiwa kwa kuwatelekeza mumewe na watoto wake watatu , huenda akafungwa miezi mitano jela au kutozwa faini ya shilingi laki mbili ikiwa atakosa kutekeleza amri ya mahakama.
Mwanamume huyo hufanya kazi za kibarua.

Kila toba ni Pentekoste Mpya!

 Na: Paskal LindaKardinali Mauro Piacenza, mhudumu mkuu wa Toba katika barua yake kwa mapadre waungamishaji anasema kwamba, kila mara Mkristo anapoungama dhambi zake na kupokea msamaha, huruma na upendo wa Mungu kutoka kwenye kiti cha maungamo, kwa Mkristo hii ni Pentekoste Mpya! Siku kuu ya Pentekoste, ili ni fursa kwa waamini kujipatanisha na Mungu pamoja na jirani zao, ili kuweza kumpokea vyema Roho Mtakatifu anayemiminwa mioyoni mwao, tayari kumtolea Mwenyezi Mungu ushuhuda wa maisha adili na matakatifu!

Neema ya Sakramenti ya Upatanisho anasema Kardinali Piacenza ni mang'amuzi mapya ya Pentekoste kwani hapa Roho Mtakatifu anaendelea kulitakasa Kanisa la Kristo kwa njia ya huduma ya maungamo inayotolewa na Padre akiwa ameungana na Yesu Kristo, ili kusikiliza na kupima, kuamua na kutoa ushauri na hatimaye, kuponya dhambi kwa kumwondolea mwamini dhambi zake. Hii ni kazi ya Roho Mtakatifu anayetenda kwa njia ya wachungaji wake wanaojisadaka katika viti vya maungamano.

Mapadre wanakumbushwa kwamba, wamechaguliwa na kuwekwa wakfu kwa ajili ya kuwahudumia watu wa Mungu si kwa mastahili yao wenyewe bali kwa njia ya neema ya Roho Mtakatifu inayowaunganisha kwa dhati kabisa na Kristo mwenyewe, ili kushiriki upendo na kazi yake ya ukombozi. Kwa sababu hii, Padre ni mhudumu wa huruma ya Mungu na daraja kati ya waungamaji na Kristo mwenyewe.

Mapadre wanachangamotishwa na Mama Kanisa kuwa wasikivu kwa Roho Mtakatifu na karama zake zinazoliwezesha Kanisa kujitakasa na kuwatakatifuza watoto wake kwa njia ya Sakramenti ya Upatanisho!

Upendo kwa Mungu na jirani!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
 
Baba Mtakatifu Francisko katika utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro amegusia mambo msingi katika maisha na utume wa Kanisa kwa kukazia zaidi na zaidi kanuni maadili na utu wema; utu na heshima ya binadamu; tunu msingi za maisha ya ndoa na familia: Yote haya ni kadiri ya Mafundisho ya Kanisa Katoliki na Kweli za Kiinjili na wala hakuna mabadiliko! RealAudioMP3

Baba Mtakatifu Francisko anapozungumzia masuala haya kwa unyenyekevu mkubwa kutokana na uzoefu wake katika shughuli za kichungaji kuna baadhi ya watu wanapata hisia kwamba, pengine anataka kubadilisha mafundisho na msimamo wa Kanisa Katoliki katika masuala haya, lakini ukweli wa mambo ni kwamba, anachofanya ni kuendelea kukazia masuala haya kwa mwelekeo mpya zaidi!

Ametuacha vibaya!

Amepaa mbinguni na ameketi mkono wa kuume wa Mungu:

Siku arobaini baadaye ….. Mt. 1,23 – Mungu yu nasi leo tena tunasikia tamko hilo la Yesu mwenyewe.Maana yake nini? Hivyo tunaadhimisha leo uwepo wa Mungu kati yetu na uwepo wa Mungu kati yetu waoneshwa na kazi za watu wake wanaomtii Roho Mtakatifu.

I. Mdo 1,1-11
II. Efe. 1,17-23
III. Mt. 28,16-20

UTANGULIZI

Sherehe ya kanisa siku 40 baada ya sherehe ya Pasaka - kupaa mbinguni Bwana wetu Yesu Kristo. Mhubiri mmoja asema hakuna awezaye kukaa peke yake mke/mume ahitaji mke/mume mwema, mwalimu ahitaji wanafunzi wa kinyume chake nini?

Hivi pia kwa mkristo leo hii yupo Roho Mtakatifu na

Rais mpya wa Malawi aapishwa rasmi


Peter Muthirika anayeongoza chama cha DPP.
Rais mpya wa Malawi Peter Mutharika ameapishwa rasmi baaada ya kucheleweshwa kwa matokeo ya uchaguzi kufuatia madai ya udanganyifu na wizi wa kura.
Mutharika aliibuka mshindi wa uchaguzi huo baada ya kujipatia zaidi ya asilimia 36 ya kura zilizopigwa.
Rais anayeondoka mamlakani Joyce Banda alikuwa katika nafasi ya tatu.
Banda amewataka wafuasi wake kuheshimu matokeo hayo.
Mahakama kuu ilipinga ombi la kura kuhesabiwa upya baada ya Banda kudai kuwa kumekuwa na udanganyifu mkubwa katika shughuli hiyo.
Peter Mutharika aliwahi kuhudumu kama

Mchawi mtanzania jela miaka 3


Vifaa walivyopatikana navyo washukiwa walipokamatwa na polisi
Mchawi kutoka Tanzania amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu nchini Kenya kwa kumlaghai mwanamke mfanyabiashara mkenya na kumuibia shilingi milioni tisa.
Mchawi huyo alimhadaa mama huyo kuwa kwa kupitia njia za kichawi angeweza kuzifanya pesa hizo kuwa maradufu yaani milioni 18.
Bwana Amos Chipeta pia ataongezwa kifungo cha miezi tatu kwa kupatikana na vifaa vinavyoumiwa kufanya uchawi kama vile chupa, visu na ngozi ya Paka.
Kwa mujibu wa mtandao wa Daily Nation,

Tangazeni Injili ya Furaha kwa ari kuu zaidi!


Kamati kuu ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Amerika ya Kusini, CELAM, imehitimisha safari yake ya kikazi mjini Vatican iliyoanza tangu tarehe 20 hadi tarehe 28 Mei 2014 kwa kukutana na kuzungumza na Baba Mtakatifu Francisko kuhusu maisha na utume wa Kanisa Amerika ya Kusini.

Katika mazungumzo na Baba Mtakatifu, Kamati kuu ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Amerika ya Kusini, linasema kuna haja ya kuendelea kuhamasisha waamini na watu wote wenye mapenzi mema kusoma, kutafakari na kumwilisha Waraka wa Kichungaji wa Baba Mtakatifu Francisko, Injili ya Furaha, "Evangelii Gaudium" huko Amerika ya Kusini.

Imekuwa ni fursa kwa viongozi hawa kumshirikisha Baba Mtakatifu Francisko yale yatakayojadiliwa na Maaskofu katika kongamano lao la mwaka, kuhusu familia linalotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 4 hadi tarehe 9 Agosti 2014. Baba Mtakatifu Francisko kwa kuangalia changamoto zilizopo kwa sasa anasema, pengine kuna haja ya kuadhimisha tena Sinodi Maalum kwa ajili ya Maaskofu wa Amerika ya Kusini, kama Kanisa lilivyofanya kwa Maaskofu Katoliki Barani Afrika, Sinodi iliyoitishwa kwanza kabisa na Mtakatifu Yohane Paulo II na kuridhiwa na Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI.

Kamati kuu ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Amerika ya Kusini na Caraibi, limepata nafasi ya kukutana na kuzungumza na viongozi wakuu mjini Vatican pamoja na kutembelea baadhi ya Mabaraza ya Kipapa kuhusu masuala ya: Mafundisho tanzu ya Kanisa, Utamaduni, Familia, Mawasiliano, Uinjilishaji Mpya pamoja na Sinodi za Maaskofu. Viongozi hawa walibahatika kuzungumza pia na Tume ya Kipapa kwa ajili ya Amerika ya Kusini pamoja na Mabalozi kutoka Amerika ya Kusini wanaoziwakilisha nchi zao mjini Vatican ambao wamekabidhiwa hati kuhusu hali ya wakimbizi huko Amerika ya Kusini!

Umefunga na nani pingu za maisha?


Tupo bado kwenye chumba cha karamu ya mwisho tukisikiliza Wosia wa Yesu. Lugha inayotumika leo ni ya kimahaba, yaani, lugha ya upendo wa dhati kama ile ya wanandoa wanaopendana. Lugha hiyo ndiyo anayoitumia Yesu anapoagana na wafuasi wake, na kuwafanya kuhamasika kumsikiliza.

Katika Wosia huo ulio katika sura tano za Injili, neno upendo linatumika mara ishirini na sita. Kwa mara ya kwanza unalikuta kwenye fasuli ya leo: “Mkinipenda, mtazishika amri zangu,” au vizuri zaidi lingetumika neno: “Kama” mkinipenda. Namna hii ya kuongea kwa upande wa Yesu ni ya kinyenyekevu, ya kuaminia, ya saburi na ya kujali, yaani inajali sana uhuru na hiari ya yule anayeambiwa; kama vile angesema: “Yote yanakutegemea wewe”.

Hiyo ni lugha huru ya Yesu aliye huru. Yesu anatumia lugha ya maelewano na ya makubaliano. Kama sote tujuavyo kwamba mambo mengine yanaweza kutendeka kirahisi, kwa ari na kwa moyo wote endapo yanafanyika kwa hiari, wasemavyo waswahili: “Ukipenda utakula nyama mbichi”.

Injili ya leo ina aya saba na kwa mara saba katika kila aya Yesu

Papa akamilisha Hija yake Mashariki ya Kati na wito wa amani

Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu jioni alikamilisha hija yake Mashariki ya Kati na wito wa amani. Hija hii ya siku ya tatu 24-26 Mei 2014 kutembelea maneneo Matakatifu katika Nchi Takatifu aliikamilisha, akiwa mjini Jerusalem ambako hatua ya mwisho aliongoza Ibada ya Misa akiwa na Maaskofu wa Nchi Takatifu, katika jengo lenye Chumba cha Juu ambako Kristo, alifanya karamu ya mwisho, kinachojulikana kama “cenacolo”.

Baada ya Ibada, alielekea uwanja wa ndege wa Monte Scopes , ambako alipanda helkoputa hadi uwanja wa Ndege wa Ben Gourion wa mjini Tel Aviv, ambako aliagana na wenyeji wake, viongozi wa kanisa na serikali wakiongozwa na Rais wa Israel, Shimon Peres. Mahali hapo Papa pia kulifanyika gwaride la heshima la wanajeshi. Na kabla ya kupanda ndege alitoa salaam zake za mwisho kwa wote.

Wachambuzi wa ziara hii wanasema ,

Braeking news:20 wafariki katika ajali ya treni


Treni
Maafisa wa huduma za treni nchini India wanasema kuwa takriban watu 20 wanahofiwa kufariki katika ajali ya gari moshi katika jimbo la Uttar Pradesh.
Treni hiyo ya kubeba abiria iligongana na treni ya jizigo iliyokuwa imeemgeshwa katika kituo cha treni cha Chureb.
Mabehewa sita ya treni hiyo ya Gorakhdham Express yaling'oka kutoka kwenye treni hiyo.
Waokozi wanajaribu kuwaokoa abiria waliokuwa ndani ya treni hiyo na ambao bado wamekwama.
Treni hiyo ilikuwa inasafiri kutoka mjini Gorakhpur hadi katika jimbo la Hisar Haryana

Bikira Maria linda familia, vijana na wazee!



Baba Mtakatifu Francisko Jumapili tarehe 25 Mei 2014 baada ya maadhimisho ya Ibada ya Misa Takatifu kwenye Uwanja wa Pango la Mtoto Yesu mjini Bethlehemu, amesali pamoja na waamini Sala ya Malkia wa Mbingu, mahali hapa ambapo Bikira Maria alimzaa Mtoto Yesu, akapata nafasi ya kuutafakari uso wa Yesu kuliko mtu mwingine yoyote duniani. Akasaidiwa na Mtakatifu Yosefu kumlaza Mtoto Yesu katika Pango la kulishia wanyama!

Baba Mtakatifu amewaweka wananchi na wakazi wote wa eneo hili chini ya ulinzi na tunza ya Bikira Maria, ili waweze kuishi katika haki, amani na udugu. Amewaweka pia mahujaji wote wanaotoka sehemu mbali mbali duniani kuja mjini Bethlehemu ili kujichotea neema kutoka kwenye kisima cha imani ya Kikristo, chini ya ulinzi wa Bikira Maria.

Baba Mtakatifu anamwomba Bikira Maria kulinda familia, vijana na wazee; kuwasaidia wale ambao wamepoteza imani na matumaini; awafariji wagonjwa, wafungwa na wote wanaoteseka; awaimarishe viongozi wa dini na Jumuiya nzima ya waamini, ili kweli waweze kuwa ni chumvi na mwanga wa katika Nchi hii. Baba Mtakatifu anamwomba Bikira Maria alinde huduma za elimu zinazotolewa katika eneo hili, lakini zaidi kutoka Chuo Kikuu cha Bethlehemu.

Baba Mtakatifu anapotafakari kuhusu Familia Takatifu, mawazo yake yanakwenda moja kwa moja mjini Nazaret ambako anatamani kwenda kutembelea Mwenyezi Mungu akipenda wakati mwingine tena. Ameonesha upendo na mshikamano wake kwa waamini wote wanaoishi katika eneo hili. Anamwomba Bikira Maria asaidie mchakato wa ujenzi wa udugu, mshikamano na amani
!

Roho Mtakatifu ni kocha wa maisha ya kiroho!


Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican inapenda kukushirikisha utajiri wa tafakari ya Neno la Mungu, Jumapili ya Vi ya Kipindi cha Pasaka inayomwonesha Roho Mtakatifu kuwa kweli ni kocha na mwalimu wa maisha ya kiroho! Kazi kwako!

Katika Injili NENO KUPENDA/PENDO linatawala – hivi unajisikiaje unapoambiwa nakupenda au unapohisi kuwa unapendwa? Hakika kupenda kunawajibisha - tamko hilo lasubiri jibu. Wengi wetu twafahamu fika jinsi ilivyo vigumu kupenda upeo/kweli. Upendo unadai matendo. Kinachofuata ni wajibu.


Ndicho kinachoonekana katika masomo yetu ya leo = kutii amri na kuabudu. Ndiyo maana Yesu anaweza kusema mkinipenda mtazishika amri zangu. Mtakatifu Tomas wa Akwino - sheria za Mungu ni nyepesi kwa wapendao na mzigo kwa wasiopenda.

1 Jan 4,8 yeye asiyependa hakumjua Mungu kwa maana Mungu ni upendo -hivyo ili kupenda vizuri ni lazima kumjua Mungu sababu yeye ni PENDO. Mapendo ya kweli yadai sadaka. Ili kushika amri au sheria inavyotakiwa yahitaji sadaka kubwa na inayodai utumishi.

Mt Agustino anapotafakari juu ya upendo wa Mungu anasema - umegusa mioyo yetu kwa pinde za upendo wako na akili zetu kwa mishale ya neno lako.

Baada ya utangulizi na kusikia masomo

Papa Francisko aanza hija yake ya kichungaji Nchi Takatifu

Baba Mtakatifu Francisko ameondoka mjini Roma asubuhi, tarehe 24 Mei 2014 tayari kwa hija ya kitume huko Yordani, Palestina na Israeli kama kilele cha maadhimisho ya Jubilee ya Miaka 50 tangu Papa Paulo VI alipokutana, akazungumza na kusali pamoja na Patriaki Anathegoras wa Yerusalemu, huu ukawa ni mwanzo mpya wa mchakato wa majadiliano ya kiekumene.

Baba Mtakatifu katika Uwanja wa ndege wa Fiumicino, Roma amesindikizwa na viongozi mbali mbali wa Kanisa na Serikali ya Italia. Ametumia nafasi hii kuwasalimia mmoja mmoja na kuwatakia kheri na baraka. Kama desturi, Baba Mtakatifu alibeba mkoba wake mweusi tayari kuanza safari ya kitume Nchi Takatifu.

Baba Mtakatifu amewaandikia wakuu wa Nchi ya Italia, Ugiriki, Cyprus na Israeli ujumbe wa matashi mema wakati alipokuwa anasafiri kuelekea mjini Amman, kituo cha kwanza cha hija yake ya kitume! Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe aliomwandikia Rais Giorgio Napolitano wa Italia, anamwambia kwamba, anaelekea Nchi Takatifu ili kuadhimisha Jubilee ya Miaka 50 tangu Papa Paulo VI alipokutana na Patriaki Anathegoras wa Yerusalem pamoja na kusali kwa ajili ya kuombea haki, amani pamoja na kukoleza majadiliano ya kiekumene na kidini. Anawatakia kheri na baraka wananchi wa Italia, anawaomba pia kumkumbuka katika sala zao.

Naye Rais Giorgio Napolitano wa Italia amemshukuru Baba Mtakatifu Francisko na kwamba, Jumuiya ya Kimataifa ina matumaini makubwa katika hija hii ya kitume huko Nchi Takatifu, mahali ambapo kuna kinzani kubwa katika historia yake na ulimwengu kwa ujumla. Ni matumaini ya Rais Napolitano kwamba, hija hii itakuwa ni cheche za matumaini kwa wale wanaotaka kusimama kidete kuendeleza amani na utulivu. Rais Napolitano anamtakia mafanikio mema katika hija hii ya kitume.

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa Rais Karolos Paoulias wa Ugiriki anamtakia mafanikio mema katika kukuza na kudumisha misingi ya haki na amani, anawaombea baraka tele kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Baba Mtakatifu Francisko akimwandikia Rais Nicos Anastasides wa Ugriki anasema, anawatakia kheri na baraka tele wananchi wa Ugiriki na kwamba, anawaombea furaha na amani kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Mwishoni, Baba Mtakatifu Francisko amemwandikia pia ujumbe Rais Shimon Peres wa Israel kwa kumtakia matashi mema na wananchi wote wa Israeli na kwamba, ana matumaini ya kukutana naye Nchi Takatifu wakati wa hija yake ya kichungaji. Anawatakia wote baraka tele!




Tafakari ya Neno la Mungu, Jumapili ya 6 ya Kipindi cha Pasaka


Karibuni ndugu msikilizaji wa Radio Vatican katika kipindi cha Liturujia ya Neno la Mungu, tukiwa tayari Dominika VI ya Kipindi cha Pasaka, ambamo tunasikia na kuona Bwana mfufuka akihaidi zawadi ya Roho Mtakatifu. RealAudioMP3

Mpendwa mwana wa Mungu, katika somo la kwanza (Mdo, 8: 5-8, 14-17) tunakutana na Filipo ambaye yuko mji wa Samaria akihubiri habari njema huko. Katika mahubiri yake hayo au tuseme kazi zake za kichungaji atatenda ishara nyingi na mojawapo ya ishara hizi ni watu kunasuliwa toka pepo wachafu, waliopooza kuponywa na ishara nyingine kama hizo zilengazo kuleta uhuru katika maisha ya watu.

Kwa hakika watu walifurahi kama mwandishi anavyosema “ikawa furaha kuu katika mji ule”. Mitume waliposikia kuwa Samaria wamepokea Neno la Mungu waliwatuma Petro na Yohane ili wawawekee mikono kwa ajili ya kushukiwa na Roho Mtakatifu, maana walikuwa wamebatizwa tu kwa jin

Papa Francisko ajikabidhi chini ya ulinzi wa Bikira Maria!

Baba Mtakatifu Francisko Ijumaa, tarehe 23 Mei 2014 asubuhi na mapema, aliondoka kutoka mjini Vatican na kwenda kusali kwenye Kanisa kuu la Bikira Maria mkuu lililoko mjini Vatican, kuomba ulinzi na tunza ya Bikira Maria kabla ya kuanza hija yake ya kichungaji Nchi Takatifu itakayomwezesha kutembelea: Yordan, Palestina na Israeli kama sehemu ya maadhimisho ya Jubilee ya Miaka 50 tangu Papa Paulo VI alipokutana, akazungumza na kusali na Patriaki Anathegoras wa Yerusalemu.

Baba Mtakatifu Francisko alipokuwa anatangaza hija hii ya kitume aliwaambia waamini waliokuwa kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican kwamba, hija hii itafikia kilele chake wakati viongozi wawakilishi wa Makanisa watakaposali kwa pamoja kwenye Kaburi Takatifu, mwendelezo wa mchakato wa majadiliano ya kiekumene, ili wote wawe wamoja!


Kumekucha!

Ili wote wawe wamoja ndiyo kauli mbiu inayoongoza Hija ya kitume ya baba Mtakatifu Francisko katika Nchi Takatifu kuanzia tarehe 24 hadi tarehe 26 Mei 2014, kama sehemu ya Maadhimisho ya Jubilee ya Miaka 50 tangu Papa Paulo VI alipokutana na kusali pamoja na Patriaki Anathegoras wa Yerusalemu, tarehe 5 Januari 1964. RealAudioMP3

Baba Mtakatifu anatarajiwa kuondoka mjini Roma, Jumamosi, tarehe 24 Mei 2014 majira ya Saa 2:15 asubuhi na kuwasili Amman, Yordani saa 7:00 mchana na baadaye yatafuatia mapokezi ya heshima yatakayofanyika kwenye Jumba la Mfalme Al – Husseini majira ya Saa 7: 45. Baba Mtakatifu anatarajiwa kukutana na kuzungumza na viongozi wa Serikali ya Yordani majira ya saa 8:20 na baadaye Saa 10: 00 anatarajiwa kuadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwenye uwanja wa Kimataifa wa Amman. Jioni Baba Mtakatifu atatembelea kwenye eneo la Ubatizo wa Yesu, Ng’ambo ya Mto Yordan. Baadaye atakutana na kuzungumza na wakimbizi, wahamiaji na vijana walemavu.

Jumapili tarehe 25 Mei 2014, Baba Mtakatifu

Jengeni utamaduni wa watu kukutana na kudumisha amani!

Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 19 Mei 2014 amekutana na kuzungumza na Baraza la Maaskofu Katoliki Mexico kwa kuwataka kujenga na kudumisha utamaduni wa watu kukutana pamoja na kujenga amani. Ili Kanisa liweze kuendelea kuwajengea watu imani na matumaini, halina budi kushikamana na wahanga wa biashara haramu ya dawa za kulevya pamoja na maskini!

Baba Mtakatifu anasema, hakuna sababu ya Kanisa kuogopa au kutishwa na nguvu za giza, bali linapaswa kusimama kidete na kwa ujasiri pamoja na watu wanaoendelea kuteseka, kwa kutetea haki zao msingi pamoja na kushiriki katika mchakato wa kuwaletea maendeleo endelevu yanayomlenga mtu mzima: kiroho na kimwili. Mambo haya yanajikita katika mchakato wa Uinjilishaji pamoja na kutafuta mafao ya wengi.

Barua ya Papa Francisko kwa ajili ya Familia

Baba Mtakatifu Francisko kama sehemu ya maandalizi ya Maadhimisho ya Sinodi Maalum ya Maaskofu kwa ajili ya Familia itakayoadhimishwa Mwezi Oktoba 2014 hapa mjini Vatican, kwa kuongozwa na kauli mbiu "Changamoto za kichungaji kuhusu familia mintarafu Uinjilishaji" ameandika barua kwa familia zote duniani ili kukazia dhamana ya Kanisa kuendelea kutangaza Injili kwa kukabiliana kinaga ubaga na changamoto mpya zinazohusu familia.

Baba Mtakatifu anasema, maandalizi haya yanawahusu Watu wote wa Mungu kwa kuhakikisha kwamba, wanashiriki kikamilifu kwa kutoa mawazo pamoja na kusindikiza mchakato mzima kwa njia ya sala, jambo muhimu sana kutoka kwa familia zote. Sinodi hii ni maalum kwa ajili ya: wito na utume wa Kanisa na Jamii; matatizo yanayowakabili wanandoa; maisha ya kifamilia, elimu na malezi kwa watoto; dhamana na utume wa familia katika maisha ya Kanisa.

Baba Mtakatifu anazialika familia kusali na kumwomba Roho Mtakatifu ili aweze kuwaangazia Mababa wa Sinodi katika kutekeleza wajibu wao huu nyeti. Sinodi hii maalum, itafuatiwa tena na Sinodi ya kawaida ya Maaskofu itakayojadili kuhusu tema ya familia mwaka 2015 sanjari na Maadhimisho ya Siku ya Familia Kimataifa itakayofanyika mwezi septemba, mjini Philadelphia, nchini Marekani.

Baba Mtakatifu anawaalika wanafamilia pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kusali kwa ajili ya kufanikisha matukio haya makuu ndani ya Kanisa, ili liweze kung'amua na kupata mikakati itakayosaidia familia ili kukabiliana na changamoto kadiri ya mwanga na nguvu ya Kiinjili.

Baba Mtakatifu Francisko anasema, ameitunga barua hii wakati Mama Kanisa alipokuwa anaadhimisha Siku kuu ya kutolewa Bwana Hekaluni. Ni tukio ambalo liliwakutanisha Mzee Simeoni na Anna kwa nguvu ya Roho Mtakatifu wakamtambua Yesu kuwa ni Masiha. Mzee Simeoni akamshukuru Mungu kwa kuwa ameuona wokovu na Anna kwa upande wake akasimulia matendo makuu ya Mungu licha ya uzee wake.

Inafurahisha kuona kwamba, wazee wawili na vijana wawili wanakutanishwa na Yesu. Hii inaonesha kwamba, Yesu ana uwezo wa kukutanisha na kuunganisha vizazi, kwani Yeye ni chemchemi ya upendo inayovuka ubinafsi, upweke na masikitiko. Baba Mtakatifu anasema, familia katika hija ya maisha yao wanashirikishana na kumegeana mambo mengi mema: chakula na mapumziko; kazi za nyumbani, starehe, sala, safari na hija ya maisha ya kiroho pamoja na matendo ya huruma.

Pale panapokosekana upendo, hapo kutakosekana furaha na kwamba, upendo wa kweli unabubujika kutoka kwa Kristo kwa njia ya Neno lake ambalo ni mwanga katika mapito ya waamini; anawapatia Mkate wa maisha ya uzima wa milele, unaowasaidia waamini kupambana na changamoto za maisha ya kila siku.

Baba Mtakatifu anahitimisha barua yake kwa familia kwa kuhimiza kwamba, mchango wao wa sala ni muhimu sana katika Maadhimisho ya Sinodi ya Maaskofu kuhusu Familia. Anawaomba pia kumwombea ili aweze kuwahudumia Watu wa Mungu katika ukweli na upendo. Baba Mtakatifu anawaombea ulinzi na tunza kutoka kwa Bikira Maria na Mtakatifu Yosefu, ili waweze kutembea huku wakiwa wameshikamana katika upendo na huduma.


Papa Francisko: Jengeni umoja na mshikamano; saidieni familia na maskini!

Kwa mara ya kwanza katika historia ya Baraza la Maaskofu Katoliki Italia, Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu, tarehe 19 Mei 2014 amefungua mkutano wa sitini na sita kwa kuwataka kutambua kwamba, wao ni wachungaji wa Jumuiya ya Kristo Mfufuka. Wao ni wachungaji wa Fumbo la Mwili wa Kristo yaani Kanisa, wachungaji wanaoendeleza ujio wa Ufalme wa Mungu kati ya watu kwa kutoa kipaumbele cha kwanza kwa familia, maskini na wote wanaosukumizwa pembezoni mwa Jamii.

Baba Mtakatifu Francisko katika hotuba yake ya ufunguzi amewataka Maaskofu Katoliki Italia kushikamana na Kristo pamoja na Kanisa lake, ili aweze kuwaimarisha katika imani, matumaini na mapendo, kwa kuendelea pia kuwa ni waaminifu katika utekelezaji wa mapenzi ya Mungu katika maisha na utume wao.

Kanisa ni Jumuiya ya Kristo Mfufuka inayojikita katika imani ambayo inarutubishwa kwa Neno na Sakramenti za Kanisa, changamoto na mwaliko wa kuepukana na vishawishi vinavyoweza kuwasonga na hivyo kushindwa kutekeleza wajibu wao kikamilifu: kwa kutokuwa na mikakati makini ya kichungaji, kwa kujiamini sana na kutoona umuhimu wa kumtegemea Kristo katika maisha na utume ndani ya Kanisa. Baba Mtakatifu anawaalika Maaskofu kumtegemea Kristo na kumkaribisha ili aweze kutenda pamoja nao, ili waweze kuwa kwelini watakatifu na mifano bora ya kuigwa.

Maaskofu ni wachungaji wa Kanisa ambalo ni Fumbo la Mwili wa Kristo, linalowashirikisha kwa namna ya pekee Fumbo la Pasaka na huduma inayowawajibisha kujenga na kudumisha umoja, upendo, mshikamano na ukarimu, bila kumezwa na malimwengu wala kuwadharau wengine. Huu ndio mfano bora uliooneshwa na Watakatifu Yohane XXIII na Yohane Paulo II.

Mama Kanisa anapojiandaa kumtangaza Mtumishi wa Mungu Papa Paulo VI hapo tarehe 29 Oktoba 2014 kuwa Mwenyeheri, Maaskofu wanakumbushwa maneno yake aliyowataka Maaskofu Katoliki Italia kujisadaka kwa ajili ya ujenzi wa umoja wa kitaifa, kwa kuondokana na udhaifu unaoweza kujitokeza kwa kutokuwa na mawasiliano makini, kwani kinzani na utengano ndani ya Kanisa ni kashfa kubwa na hakuna mtu anayeweza kuhalalisha kitendo hiki.

Baba Mtakatifu anawakumbusha kwamba, umoja na mshikamano wao unapata chimbuko lake katika maadhimisho ya Fumbo la Ekaristi Takatifu; kwa kujenda na kudumisha amani na utulivu hata katika nyakati ngumu. Tasahufi ya Ekaristi takatifu inajenga mshikamano, majadiliano, udugu, uhuru na uwezo wa mtu kuchangia kadiri ya Roho Mtakatifu anavyowakirimia. Baraza la Maaskofu linapaswa kuwa ni kwa ajili ya huduma ya umoja, mahusiano ya dhati, mahali pa kubadilishana na kushirikishana mang'amuzi na changamoto katika shughuli za kichungaji.

Baba Mtakatifu anawataka Maaskofu kuwa karibu na Mapadre wao katika maisha na utume wao; kwa kuwapatia majiundo makini ya awali na endelevu katika maisha ya kiutu, kitamaduni, kiroho na kimahusiano. Mkutano mkuu wa Baraza la Maaskofu utakaofanyika mwezi Novemba, 2014 utajikita katika maisha ya Mapadre, changamoto ya kufanya maandalizi makini.

Maaskofu wawasaidie watawa kutekeleza utume wao ndani ya Kanisa na kuishi kadiri ya kweli za Kiinjili, ili waweze kuwa ni mashahidi wa Injili ya Furaha. Maaskofu wajenge utamaduni wa kusikiliza watu wao, wawaimarishe katika imani, wawasaidie waamini walei katika maisha na utume wao wa kuyatakatifuza malimwengu. Wawapatie mikakati itakayowawezesha waamini walei kutangaza Neno la Mungu kwa njia ya ushuhuda wa maisha yao na Katekesi. Utume wa Kanisa unajikita katika umoja na upatanisho kama kielelezo cha unabii katika ujenzi wa Ufalme wa Mungu.

Baba Mtakatifu Francisko anasema, matendo ya huruma ni muhimu sana katika ujenzi wa Ufalme wa Mungu kati ya watu. Kanisa liguswe na matatizo yanayowakabili watu katika hija ya maisha yao hapa duniani, lisaidie kupambana na ukosefu wa haki msingi za binadamu. Kanisa linatumwa kutangaza ukweli kuhusu Kristo na huruma kwa waja wake, kwa kutambua kwamba, upendo katika ukweli ni kikolezo cha maendeleo endelevu katika familia ya binadamu, tunu zinazopaswa kumwilishwa katika matendo!

Maaskofu wawe ni wachungaji wasiomezwa na malimwengu, watu wanaopenda na kuishi ufukara, kwa kuonesha huruma na unyenyekevu katika maisha. Wawe ni watu huru wanaweza kuwakaribia watu kwa upendo na kuwasindikiza wale wanaotembea katika upweke na giza la uvuli wa maisha, ili hatimaye watu hawa waweze kuonja tena utu, matumaini pamoja na kuwa na maisha mapya.

Hapa Familia zinapaswa kupewa kipaumbele cha pekee katika maisha na utume wa Kanisa, kwa kusimama kidete kulinda, kutetea na kudumisha tunu bora za maisha ya kifamilia. Familia ni kiini cha Jamii na ushuhuda wa uzuri wa maisha. Hapa ni mahali ambapo watu wanapaswa kufundishwa namna ya kukumbatia Injili ya Uhai, kwa kuwasaidia wazazi katika mchakato wa malezi ya watoto wao, kwa kuwaganga wale waliopoteza dira na mwelekeo wa maisha.

Baba Mtakatifu Francisko anawaambia Maaskofu wa Italia kwamba, waoneshe mshikamano wa upendo na watu wasiokuwa na fursa za ajira au wale ambao wamepoteza ajira kutokana na sababu mbali mbali, watu ambao kwa sasa maisha na utu wao uko mashakani. Wawafungulie milango wakimbizi na wahamiaji wanaotafuta faraja na kutaka kusalimisha maisha yao kutoka kwenye vita, nyanyaso na dhuluma, kwani upendo ni kielelezo kikuu cha ushuhuda wa ukarimu, kwani hii Injili itaenea sehemu mbali mbali kwa kuonesha mvuto na mashiko!

Baba Mtakatifu anasema kuna haja ya kuwa na sera mbadala katika mikakati ya maendeleo ya kiuchumi kwa kutoa kipaumbele cha kwanza kwa binadamu na mahitaji yake msingi, kwa kulinda na kuboresha mazingira sanjari na kuwajengea watu matumaini wakati huu wanapopambana na athari za myumbo wa uchumi kimataifa; mmong'onyoko wa kimaadili na utu wema pamoja na watu kupoteza mwelekeo katika maisha ya kiroho. Hapa kuna haja ya kuwa na mikakati makini kwa kuona ukweli wa mambo, ili kujenga na kudumisha, udugu na mshikamano.

Mwishoni, Baba Mtakatifu Francisko amewaomba Maaskofu wa Italia kumsindikiza katika hija yake ya kitume huko Nchi Takatifu, kama sehemu ya maadhimisho ya jubilee ya Miaka 50 tangu Papa Paulo VI alipokutana, akazungumza pamoja na kusali na Patriaki Anathegoras wa Yerusalemu. Anakwenda huko ili kuwaonjesha mshikamano wa Kanisa kwa ajili ya watu wanaoishi katika eneo ambalo limebarikiwa na Yesu kwa kufa na kufufuka kwake!


Apewa adhabu ya kifo kwa kuolewa na Mkristo!



Mahakama moja nchini Sudan imemkuta na hatia Meriam Yahya Ibrahim Ishaq, mwanamke mwenye umri wa miaka 27 ya kukufuru na kuzini kwa kuwa ameolewa na raia mmoja Mkristo kutoka Sudan ya Kusini na hivyo kuhukumiwa kuchapwa viboko mia moja na kunyongwa hadi kufa!

Adhabu hii imewashtua watetezi wa haki msingi za binadamu, kwa kuitaka Serikali ya Sudan kuheshimu uhuru wa kuabudu kadiri ya Katiba ya nchi iliyotungwa kunako Mwaka 2005.

Mahakama hiyo imetumia "Sharia" za dini ya Kiislam zilizoingizwa nchini humo kunako mwaka 1983 zinazopiga rufuku kwa mwamini wa dini ya Kiislam kuoa au kuolewa na Mkristo. Viongozi mbali mbali wa Jumuiya ya Kimataifa wameitaka Serikali ya Sudan kuingilia kati ili kusitisha utekelezaji wa adhabu hii ambayo ni kinyume cha haki msingi za binadamu.


Tafakari ya Neno la Mungu, Jumapili V ya Pasaka



Ninaendelea tena kuwa nawe katika kipindi cha Liturujia ya Neno la Mungu, tukiwa tayari Dominika ya V ya Pasaka. Ujumbe wa Neno la Mungu umezama katika kuamini kina katika Bwana na kisha kutoa huduma katika jumuiya kama njia ya kukamilisha unachoamini na hivi baadaye kukuwezesha kufika mbinguni. Bwana anaenda huko kutayarisha makao ya kutosha kwa ajili yetu. RealAudioMP3

Katika somo la kwanza: (Mdo, 6:1-7), tunakutana na ongezeko la wanafunzi katika jumuiya ya kwanza, na katika ongezeko hili, kunatokea malalamiko ya Wayahudi wa Kiyunani, dhidi ya Waebrania kwa sababu ya huduma pungufu kwa wajane. Basi Mitume wakishauriana na kusali wanaona kuwa haipendezi wao kuacha huduma ya Neno la Mungu na kuhudumu mezani.

Uamuzi unaotolewa ni kuwaambia wanajumuiya ya wa jumuiya ya kwanza wakisema chagueni kati yenu watu 7 wenye karama ya wema, wenye kujawa na roho na hekima, ili tuwaweke juu ya jambo hili na sisi tutadumu katika kuomba na kuhudumia lile Neno”. Baada ya ushauri huo wakachaguliwa watu 7 kati yao alikuwako Stefano aliyejaa imani na Roho Mtakatifu, wakasali na wakawawekea mikono na tayari wakawa mashemasi katika Kanisa.

Mpendwa msikilizaji kwa nini kunatokea malumbano na mikingamo katika Jumuiya ya kwanza? Kwa nini mwandishi anaweka jambo hili mbele yetu? Jambo la kukumbuka katika simulizi hili ni kwamba hapo mwanzo Jumuiya ilikuwa na Waebrania tu na polepole kadiri ya kazi ya kimisionari ilivyokuwa ikisonga mbele, wakajiunga hata Wayahudi wa Kiyunani ambao walikuwa wakitumia lugha ya Kigriki. Wayahudi wa Kiyunani walikuwa na mchanganyiko wa tamaduni kwa maana walikuwa wakiishi nje ya Palestina.

Waebrania ambao hawakuwa na mchanganyiko, wao waliendelea kutumia lugha ya Kiebrania kama kawaida! Basi jumuiya ilivyozidi kuongezeka vilianza kujitokeza vijidharau vya hapa na pale dhidi ya Wayahudi wa Kiyunani na hasa wajane na yatima wao kuhusiana na ugawanyaji wa mali za jumuiya! Kumbuka kuwa, tangu mwanzo walikuwa wameweka mali pamoja. Mambo haya yalianza kujitokeza baada ya miaka 3 hivi. Kilele cha dharau ni malumbano na madai ya kutaka Mitume washiriki katika kuhudumu mezani, ili kuweka haki katika maisha ya jumuiya kila siku.

Basi, shauri hilo likiwafikia Mitume, na Mitume wataamua kwa hekima ya kimungu kuwaweka wakfu watu saba kwa ajili ya huduma hiyo. Mpendwa msikilizaji hiki ndicho chanzo cha ushemasi katika Kanisa Moja,Takatifu, Katoliki na la Mitume.

Mpendwa mwana wa Mungu, tunajifunza nini katika hili? Jambo la kwanza tunajifunza kuwa tangu mwanzo Kanisa limekuwa likikumbwa na matatizo na hivi kuonesha sura mbili za Kanisa: Kanisa la wema na wadhambi. Kumbe hata hivi leo inapotokea purukushani fulani katika Kanisa tusishangae, ni hali ya mwanadamu tangu mwanzo. Wajibu na jambo la kufanya ni kusali na kuomba kwa ajili ya kupatikana suluhu kwa njia ya amani.

Jambo la pili Mitume wametupa mfano bora yaani wakati Kanisa linakua nao wanaona ni vema kushirikisha madaraka waliyokabidhiwa na Mungu kwa wengine, kwa ajili ya faida ya Taifa la Mungu. Wanapoamua jambo hili wanashirikisha jumuiya yote; huu ndio umoja wa Kanisa, ndicho Bwana anachotaka katika kuwa mchungaji mwema. Mitume wanabaki na lengo moja yaani utume wa Neno la Mungu.

Katika somo la Pili: (1Mt Petro 2:4-9) Mt Petro awaalika watu wote kumwendea Yesu Kristu jiwe hai, lililokataliwa na wanadamu, bali kwa Mungu ni teule. Jiwe hili ndo lile jiwe kuu la pembeni ambalo Mungu ndiye mjenzi wake. Mungu anapojenga nyumba yake akisha kuweka jiwe kuu anasonga mbele akitumia mawe mengine, yaani wanadamu ambao Mt Petro anasema “Katika yeye nasi tunaitwa kuwa nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu tena tunaalikwa kutolea daima dhabihu njema zinazokubaliwa na Mungu. Ndiyo kusema Mungu, anajenga nyumba yake kwa kutumia mawe yaliyohai, yaliyojaa upendo! Hawa ni wabatizwa wanaomkubali Kristu na hivi kujenga nyumba ya kiroho yaani Kanisa la Mungu.

Mpendwa msikilizaji yafaa kujiuliza ujenzi huu ulianza lini? Kwa hakika ujenzi umeanza wakati wa ufufuko wa Bwana, maana waashi walilikataa jiwe hai na Mungu akalifanya kwa njia ya ufufuko kuwa jiwe kuu la pembeni. Jambo hili lilishaaguliwa na manabii wa kale “tazama naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule lenye heshima”. Ni kwa jinsi hiyo basi uaguzi huu umekamilika katika ufufuko wa Bwana. Mpendwa msikilizaji kwa kuwa mawe hai ya nyumba ya Mungu, Bwana anatuita daima kuachana na giza na tunaalikwa kuzitangaza fadhili zake daima kwa mataifa ili waweze kuingia katika nuru yake ya ajabu.

Katika Injili: (Yn 14:1-12) Mwinjili anaweka mbele yetu mafundisho ya Bwana aliyoyatoa katika chakula cha jioni siku iliyotangulia kuteswa kwake. Ndiyo kusema anawaachia wosia Mitume na vizazi vyote. Mmoja anaweza kuuliza hivi kwa nini Mama Kanisa ameweka somo hili baada ya Pasaka? Ni kwa sababu moja ya kawaida kwamba wosia husomwa baada ya mwenye kuandika wosia anapokuwa ameondoka duniani!

Katika mafundisho ya Bwana tunaona jinsi Bwana mwenyewe akiwatayarisha wanafunzi wake kwa ajili ya Kupaa kwake. Anasema wasifadhaike bali wawe na imani katika Mungu na yeye mwenyewe, na kisha wakumbuke anaenda kuwatayarishia makao tele ili atakapokuwepo nao wawepo. Jambo la kwenda kutayarisha makao linashangaza kidogo kwa sababu kuna mawazo kwamba tayari pamekwishaandaliwa! Ni kweli, lakini ataka kutuambia suala la kusafiri na ugumu wake linahitaji maandalizi. Kwa sababu hiyo basi, Bwana ataongeza neno akisema huko niendako mwaijua njia!

Mpendwa mwanatafakari, kwa kuwa njia na makao tunayopaswa kuyafikia ni kazi nyeti, mara moja Tomaso atasema hatujui njia! Bwana mkarimu na Mchungaji mwema anamjibu “mimi ndimi njia na ukweli na uzima; mtu haji kwa Baba ila kwa njia ya mimi”. Hili maana yake nini? Jambo hili lamaanisha lazima kufuata njia ya mapendo, njia ya mateso hadi msalabani na kisha hapo kutakuwa na ufufuko.

Kumbe, matayarisho ya makao yanaanza na msalaba wake na kisha ufufuko furaha ya milele na Baba mbinguni. Ili tuweze kupita katika njia ya Bwana tunahitaji msaada wake na ndiyo maana alisema, nitaenda na kisha nitarudi kuwachukua pamoja nami! Katika kutangaza makao, Bwana ansema nyumbani mwa Baba yake, kuna makao mengi. Bwana ataka kusema nini katika hili? Ataka kusema tukikubali kumfuasa yeye basi kuna wajibu na shughuli za kutosha kama tuonavyo leo katika Kanisa. Nyajibu hizi tunaalikwa kuzifanya kwa mapendo tukishirikiana katika raha na taabu mpaka kufikia mwisho wa nyakati na hapa ndipo kuna kumwona Baba.

Wakati Bwana anatangaza kuwa yeye ni njia ya kwenda kwa Baba, mara moja Filipo anauliza utuoneshe Baba yatutosha! Ombi hili linamwendea Bwana na hata sisi wakristu wa leo. Kwa upande wake Bwana anajibu akisema aliyeniona mimi amemwona Baba, kwa kuwa mimi ni ndani ya Baba na Baba yu ndani yangu. Kwa upande wetu tunapaswa kusema daima aliyemwona Kristu amemwona Baba. Baada ya fundisho hilo lililo gumu kwao, Bwana atawaalika kusadiki hilo na kama hawasadiki basi wasadikini kwa sababu ya kazi zenyewe!

Mpendwa, kwa kumtambua na kumjua Baba haina haja ya kujenga falsafa ya pekee bali ni kuitikia kile ambacho Bwana anasema. Ndiyo kusema inatosha tu kumtazama Kristu yaani Mwana, ambaye ni sura kamilifu ya Mungu. Inatosha kumtazama Mwana, yamaanisha na yatulazimu kusoma Neno la Mungu na kutafakari, kusikia kile anachofundisha kwa njia ya Kanisa, kupambanua namna yake ya kupenda yaani mpende adui yako, namna yake ya kukosoa kunapokuwa na shida au dhambi na mwishoni kuyashika yale yote mema aliyoliachia Kanisa la Kitume.

Mpendwa msikilizaji, katika kusadiki yaani, kuamini kuliko kina Bwana anafungamanisha zawadi, yaani anasema kama mmoja akisadiki ataweza kufanya mambo makubwa katika maisha yake. Hili ni kweli nami nasadiki.

Nakutakieni furaha tele katika Dominika hii ya Pasaka na Mungu azidi kuwa nawe, ukitekeleza mapenzi yake katika maisha yako. Tukutane tena Dominika ijayo. Tumsifu Yesu Kristu. Tafakari hii imeletwa kwako na Padre Richard Tiganya C.PP.S.

Ekaristi Takatifu!

Ndugu msikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican, tulianza maandalizi ya hija ya kichungaji ya Baba Mtakatifu Francisko katika Nchi Takatifu kwa kukufanualia maeneo muhimu katika historia na maisha ya Yesu. Tumekwishatembelea Bethlehemu mahali alipozaliwa Yesu, tukavuka ng'ambo ya pili ya Mto Yordan, mahali alipobatizwa na leo tuko chumba cha juu, mahali alipoweka Ekaristi Takatifu na kuwataka wanafunzi wake wawe ni watu wa huduma! RealAudioMP3
Karibu Wainjili wote wanatupatia maelezo ya karamu ya mwisho. Katika chumba kilicho juu. Wainjili wanasema kwamba karamu hiyo ilikuwa ya Agano Jipya na la milele.

Katika mazingira hayohayo ya kula Yesu akawaosha miguu wafuasi wake. Kila mwenjili anajitahidi kutoa fundisho la pekee kadiri anavyoona yeye. Hapa sisi tufuate maelezo ya mwinjili Luka. Sote tunafahamu kilichotokea siku ile ya karamu ya mwisho. Maneno ambayo Luka anayoyatumia na ambayo yabidi kuyafanyia tafakuri ni yake tunayoyasikia katika kila misa: “fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.” Ni mwinjili Luka peke yake anayesema maneno hayo.

Lengo la Yesu lilikuwa ni kuwaalika wafuasi wake wote kumkumbuka Yeye, yaani daima kurudia kufanya kitendo hicho. Lakini zaidi pia aliwataka wamege mkate na kula ikiwa kama alama ya msingi katika imani yetu. Tendo la kumega mkate ni ufupisho wa maisha yake yote toka kuzaliwa hadi kufa kwake. “Mimi nimejifanya chakula ili kuyalisha maisha.” Ni kama vile angekuwa Bethlehemu inayotembea (mobile bakery).

Luka anataka kutuambia kuwa mnapokuwa katika karamu hii, au mnapokula chakula hiki, mnafanya uchaguzi kama wangu wa kujitoa na kujitolea. Huo ni mwaliko wa kuwa kama Kristu, wa kuwa mkate na kujigawa kwa wengine. Kwa hiyo haitaeleweka kabisa kumwona mkristu baada ya kuadhimisha ekaristi, anashindwa kusaidia wengine.

Hali halisi nyingine inayoonekana humo chumbani, wakati wa sherehe hiyo kuliibuka mabishano mazito hasahasa tungeweza kuyaita mahojiano makali kati ya mitume. Kisa walikuwa wanabishana juu ya ukuu, juu ya kuwa na heshima na cheo kati yao “ni nani anayehesabiwa kuwa mkuubwa.” Yesu akawaambia: “Wakuu wa mataifa huwatawala, na wenye mamlaka juu yao huitwa Wenye fadhili; lakini kwenu ninyi sivyo; bali aliye mkubwa kwenu na awe kama aliye mdogo; na mwenye kuongoza kama yule atumikaye. Mimi niko kati yenu kama atumikaye.” Haya tena ni maneno yanayoletwa na Luka peke yake wakati huu wa mlo. Ni maneno kwa ajili ya kila mtu hasahasa yule anayejiita mkristu. Hayo ndiyo mambo yanayoharibu jumuia za kiristu siku za leo. Kazi ya mtu aliyeshiba ni kutafuta cheo.

Mahojiano hayo ya mitume hayakuishia kwao tu. Mabishano hayo yameletwa hapa kuonesha kuwa yanaweza kumpata kila mmoja katika maisha yake. Hasa kuhusu kujihoji wewe mwenyewe kuhusu kuchagua mambo. Hali kadhalika Yesu Kristu katika maisha yake hapa duniani alikabiliwa na changamoto hii ya kujihoji nafsini mwake.

Mahojiano hayo ya Yesu tutayaona baada ya karamu ya mwisho akiwa kwenye mlima wa Mizeituni. Tunaambiwa kuwa alipatwa na uchungu sana ambao katika Injili ya Kiswahili wanafasiri kuwa ni dhiki. “Yesu akatoka akaenda mpaka mlima wa Mizeituni kama ilivyokuwa desturi yake; ...akajitenga na mitume wake… huko akasali... kwa vile alikuwa katika dhiki... hari yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka nchi.”

Alikuwa katika katika dhidi au tuseme alikuwa na hali mbaya sana. Yaani ni kama hali ile anayokuwa nayo mtu kabla ya kufa. Neno hili uchungu pia limetokea katika injili ya Luka peke yake, kwa kiingereza ni "Agony". Maana halisi ya neno hilo agoni lamaanisha mapambano, mashindano au mahojiano makali. Hasa mashindano kama yale ya wanariadha. Yesu aliingia katika mashindano kama hayo.

Toka mwanzo wa maisha yake, Yesu ilimbidi aingie katika mapambano na mashindano na nguvu za shetani. Mapambano hayo hayakwisha katika vishawishi, yaani pale shetani alipomjia Yesu jangwani mara tu baada ya kubatizwa. La hasha, baada ya vishawishi vile tunasikia kuwa shetani alimwacha Yesu kwa muda. “Basi alipomaliza kila jaribu, Ibilisi akamwacha akaenda zake kwa muda.” (Lk. 4:13). Shetani anakuja tena akijua kwamba hapa sasa ni lala salama!

Hapa kuna mapambano makali ya roho yanayomdai Yesu kuwa mwaminifu na inabidi kuyashinda. Yesu anashinda! Kuonesha kwamba hayo yalikuwa ni mashindano makali, Yesu anatoka jasho, hilo kama vile jasho linalomtoka mwanariadha wakati wa mashindano. Kwa hiyo "agony" siyo uchungu bali ni mapambano, kuvutana, ukinzani, ugomvi ndani ya mtu. Mapigano yaliyoko ndani ya mtu.

Katika mapambano hayo Yesu anajiandaa kwa kujitenga na kusali. “Mwenyewe akajitenga nao kama kiasi cha kutupa jiwe, akapiga magoti akaomba.” Anajiweka katika mahusiano na Mungu ili kuweza kuiona mipango ya Mungu. Anajiweka katika mahusiano na Mungu, ili kujua Mungu anao mpango gani kwa ajili yake. Yesu alisali sana na akawahimiza mitume wake kukesha na kusali. “Alipofika mahali pake aliwaambia: ‘ombeni kwamba msiingie majaribuni. Ondokeni, mkaombe msije mkaingia majaribuni.” Sala inamsaidia Yesu. Kisha wanafika malaika kumliwaza. Hiyo ni alama ya kuwa na mawazo ya ndani ya Mungu. Endapo alifikiria kutoroka maisha, kutoroka mateso sasa anaimarika, na kuhiari kuurekebisha ulimwengu. Kwa hiyo ili kushinda mapambano ya ndani ya mtu, yabidi kusali sana. Kuunganisha mipango yako na mipango ya Mwenyewe Mungu.
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican inakutakia hija njema na Baba Mtakatifu Francisko huko Nchi Takatifu kuanzia tarehe 24 hadi tarehe 26 Mei 2014 kwa kuongozwa na kauli mbiu " Wote wawe wamoja".

Imetaraishwa na
Padre Alcuin Nyirenda, OSB.



Nyumba ya Mkate!

Jina hili Bethlehemu linatokana na maneno mawili ya Kiebrania, Bet ni nyumba na Lehem (lexem) ni mkate, kwa hiyo Beth-Lehem au bet-lexem maana yake nyumba ya mkate. RealAudioMP3

Kwa lugha ya kigiriki cha zamani walitamka Bethleem. Ziko sehemu nyingi zenye nyumba ya mkate mathalani Beth-lehem-ephratah, Bethlehemjudah, lakini Bethlehemu iliyokuwa kusini karibu na Yerusalemu ndiyo iliyokuwa inaitwa Bethlehemu katika mji wa Daudi. Hapo ndipo alipozaliwa Yesu. Ni mji ambao toka zamani wameishi wakristu wengi, lakini sasa wanaishi pia watu wa dini mchanganyiko. Sehemu hii wanafurika wahaji na watalii wengi sana hususani wakati wa Kipindi cha Noeli.

Kisa cha kujulikana Betlehemu kilianza na safari ya Yosefu na Maria aliyekuwa na baraka tumboni. Walienda huko kwa ajili ya senza. Katika pilikapilika za kutafuta mahali pa kulala mama akajifungua mtoto wake hapo Betlehemu mji wa Daudi (Lk. 2:4). Baada ya kuzaliwa, mtoto huyo akaviringishwa nguo za mtoto mchanga na kulazwa kwenye hori la kulishilia wanyama.

Hii ndiyo alama ambayo malaika waliwapa maelezo wachungaji na kuwaagiza waende huko kumwona mtoto. Malaika wakawaambia wachungaji: “Leo katika mji wa Daudi amezaliwa kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristu Bwana. Na hii ndiyo ishara kwenu; mtamkuta mtoto mchanga amevikwa nguo za kitoto, amelala katika hoi ya kulia ng’ombe.”

Kumbe yawezekana malaika walikuwa wa kwanza kufika hapo Betlehemu na kushuhudia mambo yalivyo kabla ya kwenda kuwahabarisha wachungaji. Tunaambiwa pia kwamba mara tu baada ya malaika kuondoka, wachungaji nao wakaambizana wenyewe, Jamani tusiilazie damu taarifa hii ya malaika: “Twendeni mpaka Betlehemu, tukashuhudie tukio hilo alilotujulisha Bwana.” (Lk. 2:15). Baada ya kumwona mtoto wakaanza nao wakaanza kutawanya habari: “Walipomwona (mtoto Yesu) wakatoa habari waliyoambiwa juu ya huyo mtoto. Halafu wote waliosikia wakastaajabu kwa hayo waliyoambiwa na wachungaji.” (Lk 2:27).

Malaika walipoona utukufu umetua Bethlehemu, hawakuuacha utulie tu pale pangoni, bali wakaondoka kwenda kuutangaza kwa wachungaji. Kwa hiyo utukufu haukuhusu pango ila unawahusu wachungaji wanaowakilisha wanyonge wote. Wachungaji ndiyo wanaodhihirisha utukufu wa Mungu. Mungu anajidhihirisha na kutukuzwa pale tu ambapo wanyonge, fukara wanapofurahi. Huo ni utukufu wa Mungu.
Wachungaji wanafurahi kwa sababu kutokana na hali halisi ya unyonge wao, walijisikia kama watu waliolaaniwa, kwa hiyo hawakutegemea kabisa kupata mawasiliano na Mungu. Kumbe amezaliwa mchungaji mwenzao, anayejua unyonge wao. Hawakujiamini wenyewe, na mara moja wakaanza kushauriana wenyewe na kuchukua maamuzi ya kwenda kushuhudia na baadaye kutoa ushuhuda.

“Twendeni mpaka Betlehemu, tukashuhudie tukio hilo alilotujulisha Bwana.” Wanaenda haraka, kushuhudia utukufu wa Mungu, ambao ni kutaka watu wapate furaha haraka. Kwetu sisi tungetegemea kusikia mambo ya ajabu zaidi au hata kusikia muujiza. Hakuna maelekezo zaidi, ni kama vile amezaliwa mtoto wa kawaida. Maisha ya kawaida yanaendelea. Yesu kuwa Mungu hakutegemei muujiza wa pekee, bali yeye mwenyewe jinsi alivyo. Yeye ni kama sisi, Mungu amekuwa mwenzetu. Anayemtegemea Mungu wa kufanya miujiza, ujue mungu aina hiyo ni mungu wa kipagani.

Wachungaji wanaenda Betlehemu na wanamwona mtoto aliyeviringishwa nguo. Hiyo ndiyo picha mpya ya Mungu anayejidhihirisha kwa binadamu. Watoto waliviringishwa nguo ili kuwakinga na baridi lakini pia inayo maana ya kidini. Mtoto ni safi, hivi huwezi kumshika tu kwa mikono, lakini kuna maana pia muhimu ya kiroho, hasa mwinjili anaposisitiza jinsi mtoto alivyoviringishwa nguo, hoja kubwa ni kusudi mtoto huyo aweze kuguswa, kushikwashikwa na kubebwa na watu wote.

Aidha imeandikwa mara tatu kuwa aliwekwa katika hori la kulishia chakula wanyama (ng’ombe). Kwa hiyo msisitizo huo unahusu chakula. Mtoto aliviringishwa nguo, kama vile mkate unavyoviringishwa karatasi au majani na kuwekwa kwenye nyumba ya mkate (Bethlehemu). Kwamba Yesu anadhihirishwa hapa kama mkate yaani chakula. Malaika wanawaelekeza wachungaji kwenda kwenye nyumba ya mkate (bethlehemu) huko watauona mkate umeviringishwa.

“Na hii ndiyo ishara kwenu; mtamkuta mtoto mchanga amevikwa nguo za kitoto, amelala katika hoi ya kulia ng’ombe.”Yesu aliishi na kuhitimisha historia ya maisha yake hapa duniani akijionesha mwenyewe daima kuwa ni mkate utokao mbinguni. Maisha yake yote akayatolea hadi chembe ya mwisho ya mkate. “Twendeni mpaka Betlehemu, tukashuhudie tukio hilo alilotujulisha Bwana.”

Wachungaji wanapofika pangoni wakamwona Maria, Yosefu na mtoto mchanga amelala horini. Hawaoni cha pekee zaidi. Kisha wakatoa taarifa juu ya kile walichoambiwa juu ya huyo mtoto. “Walipomwona (mtoto Yesu) wakatoa habari waliyoambiwa juu ya huyo mtoto. Halafu wote waliosikia wakastaajabu kwa hayo waliyoambiwa na wachungaji.” Nadhani watu wote walishangazwa na taarifa hizo kwani ni Mungu aina gani anayeweza kuwatokea watu wanyonge kama wachungaji. Kama ndivyo basi hayo ni maajabu.

Tunaambiwa jambo jingine lililotokea pale Bethlehemu ni kuwa Maria akayaweka maneno hayo yote, akiyafikiri moyoni mwake. Neno kufikiri, siyo tafsiri sahihi, kwa kigiriki “sinmbalus” inamanisha kuweka mambo pamoja na kutafakari, hasa kule ambako mmoja unapoona mambo lakini unashindwa kuyaelewa. Maria anatulia, anaangalia, anaunganisha mambo anaweka pamoja mambo yanayomtukia. Atakuja kufahamu atakapokuwa amesimama chini ya Msalaba.

Wachungaji wanaondoka wakimshukuru na kumsifu Mungu – wameyaona maisha mapya. Wamemwona Mungu aliyejifanya binadamu na kulingana na watu. Wamemwona Mungu anayejiacha kushikwashikwa na watu wenye mikono michafu, watu wanaonuka, yaani wanyonge, maskini, wazee, wenye dhambi, walalahoi. Watu hawa wanyonge wameona na wanafurahi, wanamshukuru na kumsifu Mungu, kisha wanamshuhudia.

Kumbe, watu hawa wanyonge tu ndiyo wanaoweza kutambua na kushabikia sera hii kubwa ya Mungu kujifanya mtu. Ni watu kama hawa ndiyo wanaoweza kuwa na furaha, na kusifu na kumshukuru Mungu. Kwa wataalamu, wakuu, matajiri sera hii haiingii akili na mioyoni mwao.

Ni muhimu hata kwetu kwamba badala ya kujihoji na kufikri nini tufanye nini katika maisha, baada ya kumwona Kristu tubaki tu kufurahi. Tumeona tendo kuu la upendo alilotufanyia Mungu. Huo ndiyo mwanzo wa uchumba kati ya Mungu na binadamu, kati ya Yesu na Kanisa lake. Sisi tunafunganishwa na Yesu katika upendo. Ndiyo mwanzo wa maisha ya upendo na ya furaha. Wanaopendana daima wanashika simu mkononi wakisubiri ”message au kupib”, au kuitwa na mpendwa wao ili kuongeana.

Sisi tukitaka kugundua utukufu na upendo huo wa Mungu tuanza Bethlehemu, na kuendelea mbele hadi kwenye majitoleo kamili ya Yesu kule Kalvari. Kwa hiyo ndugu zangu “twendeni na Papa mpaka Betlehemu” tukirudi toka huko tuwapagawaze watu kwa tutakayoyaona. Hebu sasa tutoke Bethlehemu kuongozane na Papa hadi mto Yordani.

Imeandaliwa na
Padre Alcuin Nyirenda, OSB.


Twendeni Bethlehemu!

Katika dini nyingi iko desturi nzuri ya kiroho ya kufanya hija pahala patakatifu au sehemu za kihistoria za dini hiyo. Hija hiyo mara nyingi hufanyika kama moja ya kuadhimisha tukio fulani muhimu linalomhusu mtu binafsi ili kujichumia neema anayohitaji mhiji au alhaji. RealAudioMP3

Papa pia hufanya hija sehemu mbalimbali kama vile Lourdes, Fatima, Loreto, Namugongo, Nchi Takatifu, nakadhalika. Hija ya Papa haiwi kwa ajili yake binafsi tu, bali hasa ni kuchuma neema kwa ajili ya kanisa zima, pia inakuwa kwa ajili ya kuimarisha mahusiano ya kuletesha haki, amani na upendo kati ya nchi na nchi.

Mwaka huu kuna jubilei za dhahabu kadhaa za kikanisa zitokanazo na Mtaguso wa pili wa Vatican. Zaidi pia ni mwaka wa 50 tangu Papa Paulo VI alipohiji nchi ya ahadi na kuzungumza na Patriaki Anathagora wa Yerusalemu. Papa Fransis atahiji nchi ya ahadi ikiwa ni kuadhimisha jubilei ya dhahabu ya hija hiyo ya Papa Paulo VI. Katika hija hiyo, Papa atakutana na viongozi muhimu wa serikali na dini, atakutana pia na waumini wenzetu walioko huko.

Papa atazuru sehemu chache muhimu. Mosi, ataenda Bethlehemu kuzuru na kusali pahala alipozaliwa Yesu. Ataenda kuzuru na kusali kando ya mto Yordani alikobatizwa Yesu. Mwisho ataenda kuangalia chumba ambacho Yesu alikula Karamu ya Mwisho na mitume wake. Chumba hicho ni mandhali ya mwisho aliyokuwa Yesu kabla ya kuteswa na kufa kwake.

Kwa hiyo, Wakristu wote na watu wote wenye mapenzi mema tunaalikwa mosi, kuiombea hija hii ya Papa, kusudi asafiri salama, aende akatuombee na kufanikisha makusudio aliyojipangia kwa faida yake, na kwa manufaa ya kanisa zima na ulimwengu kijumla, na hatimaye arudi salama, kusudi Mungu atukuzwe katika yote.

Pili tunaalikwa sisi sote kutanguzana na Papa kwenda katika hija hiyo, usikose kuwepo katika msafara huo wa Baba Mtakatifu. Kutokana na msongamano wa watu na hasa kupanda gharama ya maisha, siyo wote watafanikiwa kwenda hiyo hija. Tunaalikwa kukata tiketi ya kiroho ambayo gharama yake ni bure sanasana inategemea uhuru wako mwenyewe, na mkatishaji tiketi ni Roho Mtakatifu mwenyewe ambaye hata Yeye mwenyewe ataenda kwenye hija hiyo ya awali tangu atoke huko alipokufa Yesu Msalabani. “Akainama kichwa akaitoa Roho yake”.

Kwa watakaoenda huko kwa tiketi ya Roho Mtakatifu, mnaalikwa kusoma ramani hii au mwongozo ufuatao, utakaowasaidia kujua sehemu mbalimbali mtakazotembelea na kuzihiji pindi mnaongozana na Papa. Hizo ni sehemu muhimu ambazo kulifanyika mambo makuu na mazito yahusuyo ukombozi wetu. Katika mwongozo huu tutajaribu kuzieleza kwa kifupi sana sehemu hizo kijiografia na kiteolojia. Tutaona pia matukio yaliyotokea sehemu hizo, yahusuhuyo Yesu au mitume wake na sisi tunaweza kupata fundisho gani toka sehemu hiyo.

Hebu twendeni kwanza Betlehemu alikozaliwa Yesu tuhimizane kwenda huko kwa maneno ya Wachungaji waliokuwa wanahimizana kwenda huko baada ya kupata taarifa toka kwa malaika: “Twendeni mpaka Betlehemu, tukashuhudie tukio hilo alilotujulisha Bwana.” (Lk 2:15).

Imeandaliwa na
Padre Alcuin Nyirenda, OSB.



Yaani, imekula kwao!

Kuna msemo ulioshamiri sana kwa Waswahili, hasa ikiwa mtu anayo matumaini ya kupata kitu katika biashara na anakikosa anaambiwa: “Imekula kwako”. Usemi huu ungeweza pia kutumika kwa mitume baada ya kifo na kuzikwa kwa Yesu. Mitume na wafuasi waliweka matumaini yao yote kwa Yesu, lakini sasa baada ya kufa kwake na kupita siku mbili tatu, wanakata tamaa na kujisikia “imekula kwao.”

Wengi wao waliingiwa na woga na kujifungia kwenye vyumbani, ili mradi tu kwamba walikuwa wameishiana na mradi wa kumfuata Yesu. Wengine baada ya kwisha tu sikukuu ya Pasaka ya kiyahudi siku iliyofuata kila mmoja akaanza kuchukua njia zake. Wafuasi wawili walitanguzana mmoja hatajwi jina na mwingine anaitwa Kleopa wakachukua zao kurudi kijijini Emmaus. Wamepoteza muda mrefu wa kutumaini, wa kujitoa, myaka mitatu ya ushindi mkuu, miaka ya imani, ya kusubiri, ya uzuri, miaka utamu ya mwanga. Lakini kifo kile cha Yesu ndicho kilichochafua kila kitu. Ama kweli imekula kwao!

Wafuasi hawa wawili walijisikia kuwa kama miali ya moto inayokaribia kuzimika. Hebu tuone jinsi Bwana mfufuka anavyoihuisha tena: Wafuasi hao wanatembea kwenye barabara kuu wanayopita watu wote, wakiwa katika huzuni kubwa, katika upweke, wakijadiliana. Yesu hawaiti toka mbali na kuwasimamisha, bali anawasogelea kama mtu mwenye haraka lakini anayetaka kutanguzana nao. Wao wanageuka na kugundua kwamba kuna mtu anawafuata. Hapa Yesu amejionesha kama msafiri wa kawaida tu ila mwenye haraka. Yeye mfufuka angeweza kusafiri kwa mwendo wa kasi sana, kumbe anatanguzana nao, anapima hatua zao zilingane na mwendo wao wa kuchoka, mwendo wa waliojeruhiwa.

Wanaelekea Emmaus, yaani anatanguzana nao katika kuchanganyikiwa kwao na katika matatizo na uchungu wao. Ndivyo Yesu anavyokutana na watu mbalimbali hapa duniani na kutanguzana nao katika safari yao ya maisha. Kila mmoja anamkuta akiwa na hali fulani ya pekee.

Tunasikia kwamba Magdalena alimkuta akiwa analia, kwa wale kumi na mmoja kule kwenye ziwa jumapili ijayo, anawakuta wana uchungu na wamechanganyikiwa baada ya kukesha usiku mzima wakivua bila kupata kitu, wakati Tomaso jumapili iliyopita alimkuta katika hali ya kutoamini. Wafuasi hawa anawakuta katika lindi la uchungu na la upweke. Wako wawili tu, lakini sasa wanakuwa wasafiri watatu.

Katika uchungu wao huo wanajadiliana na kuhubiriana juu ya suala zito na muhimu la maisha. Wanaongeana juu ya jambo linalowakereketa kabisa ndani ya mioyo yao. Wafuasi hawa wanazungumza juu ya Upendo. Yaonekana amewakimbilia, na kuwakuta ili kuwapa moyo, kuwahimiza na kuwangaza. Hawakatishi mazungumzo yao: Anatafuta mwanya wa kujiingiza katika mazungumzo yao kwa utulivu, kwa utamu kwa kuuliza swali jepesi na rahisi tu.

Tena anauliza kama vile mtu mjinga asiyefahamu kilichotokea. “Ni maneno gani haya mnayosemezana hivi mnapotembea?” Kwa swali hili Yesu anaonesha kuujali sana uchungu wao.

Swali hilo linamfanya Kleopa na mwenzake waanze kumshangaa. Yaani msafiri mwenzao aliyetokea upande wanakotokea wao kuwa hajavisikia vituko vilivyotokea huko Yerusalemu.

Habari hizo zimevuma mji mzima na watu wote wanavizungumzia sana. “Inawezekanaje, wewe unayetoka sasa hivi huko mjini usisikie habari hii ya kusikitisha?”

Angekuwa mtu mwingine yeyote angeweza kuwasimamisha na kuwaambia: “Kaeni chini hapa niwaeleze kinaganaga cha mambo yalivyotokea.” Kumbe Yesu ameanza kwa kuwaamshia hamu ya kujieleza zaidi hadi wanamgeuzia kibao: “Hivi wewe peke yako ni mgeni asiyejua…”. Huwezi kujua ni jinsi gani Yesu alilipokea swali hilo la wafuasi. Swali hilo la wafuasi linaonesha waziwazi vionjo vilivyokuwa vimejaa ndani ya mioyo yao. Hadi hapo ilimtosha kabisa Yesu kujisikia kuaminiwa na watu hawa. Kleopa aliyekuwa katika hali mbaya ya kukata tamaa, na aliyejaa jazba, amefanikiwa kujimwaga mbele ya mgeni huyu.

Yesu anawaacha waendelee kujimwaga. Bila kujitambua wakaendelea kujieleza hadi kufikia kuzungumza mambo ya kiroho waliposema: “Mambo ya Yesu wa Nazareti, aliyekuwa mtu nabii, mwenye uwezo katika kutenda na kunena mbele za Mungu na watu wote; tena jinsi wakuu wa makuhani na wakubwa wetu walivyomtia katika hukumu yak ufa, wakamshulibisha… Tena wanawake kadha wa kadha wa kwetu walitushitusha waliokwenda kaburini asubuhi na mapema, wasiuone mwili wake; wakaja wakasema ya kwamba wametokewa na malaika waliosema kwamba yu hai. Na wengine waliokuwa pamoja nasi walikwenda kaburini wakaona vivyo hivyo kama wale wanawake walivyosema, ila yeye hawakumwona.” (Lk 24:19-20, 22-24).

Hapa unaona kama vile wamechanganyikiwa. Yaani, wanaonekana kwa upande mmoja kama vile wanasadiki lakini halafu kwa upande mwingine hawasadiki. Watu hawa wanateseka sana kisaikolojia lakini walikuwa bado na imani mioyoni mwao. Kwa hiyo Yesu anawaambia: “Enyi wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyoyasema manabii!” (Lk.24:25).

Yaani, hawa walikuwa watu wa kutibiwa, siyo wa kuwalaani, watu wa kuwasahihisha na siyo kuwaachilia tu, watu wa kuwapoza siyo kuwagombeza! Baada ya kuwatulia kidogo, Yesu anaanza kuwapa dawa ya tiba. Anaanza kuwaelezea historia ya mambo yaliyokuwa kadiri ya Maandiko matakatifu hadi wanakaribia kijiji cha Emmaus.

Baadaa ya kumaliza kuwaeleza, Yesu angeweza kusema: “Sasa jamani baada ya kuwaeleza haya yote, tafadhali rudini Yerusalemu na mkawahabarishe wenzenu haya niliyowaambia ili msikose tena imani. Yesu hafanyi hivi badala yake anajifanya kama vile anapitiliza na kuendelea na safari zake. Hahitaji chochote, wala haulizi chochote, na wala hategemei chochote toka kwao. Ndiyo maana hawa wasafiri wawili wanaamua kumshawishi: “Kaa pamoja nasi, kwa kuwa kumekuchwa, na mchana unakwisha.” (Lk 24:29). “Mgeni afike mwenyeji apone”. Je, sisi tumwambie nani “Kaa pamoja nasi”?

Tunaweza kumwambia mtu aliyetutendea jema fulani “kaa nasi”, au mgeni yule ambaye hatutii hasara, mtu asiyekuwa mzigo. Wageni namna hiyo wako wachache sana na pengine hawako kabisa. Kumbe Yesu aliye Mungu hahitaji chochote. Yesu aliyesukumwa na upendo mtupu hataki kumtuliza tu mtu. Hatukani mtu, hasemi maneno yasiyo na maana, huyu mgeni alitoa maneno ya kuhuisha. Aligusa hata mioyo yao, aliwatia moyo, hadi wanamkaribisha kwao.

“Wakakikaribia kile kijiji walichokuwa wakienda, naye alifanya kama anataka kuendelea mbele.” (Lk 24: 28). Katika nafasi nyingine Yesu aliwapita wanafunzi wake: Mathalani kwenye mto Yordani, au mbele ya Yohane Mbatizaji kule Genesareti, au usiku ule wa dhoruba. Anapita pembeni ya Kanani bila kusimama. Anampita kipofu bila kumponya. Yesu anafanya hivi ili mmoja uweze kumtafuta, au uweze kumwita. Yesu anapenda kuitwa. Wakati mwingine anaweka hata mazingira ya kuja kwake na matendo yake ili aweze kuitwa na binadamu. Anavuvia, anadokeza, anashawishi, anahimiza lakini anasubiri. Wanafunzi wanamwomba atulie, abaki akae nao.

Wao wanahoja zao kinyume na ukweli ule wa ndani kabisa. Hoja wanayotoa ya kumshawishi abaki ni kwamba: “kumekuchwa, na mchana unakwisha.” Badala ya kumwambia kwamba tunapenda kuwa na wewe. Tumeshakupenda, licha ya kutukosoa na kutusahihisha, na hasa kutokana na hilo tunataka ubaki nasi. Yesu alilazimisha kwa wema. Alikuwa yeye wa kwanza kuwajongelea. Sasa wamekuwa wao kutaka kumshikilia asiondoke. Anaingia na katika tendo la kumega mkate, wanamtambua. Mioyo yao inafunguka: “Ni Yeye” wakasema. Lakini kabla hawajafanikia kuwasiliana naye, akawa ameshatoweka machoni pao.

Kumbe, ili aweze kutambulika, haoneshi vyeti vyake vya utambuilisho, na vyeti vya shule. Anajitambualisha kwa kumega mkate. Tendo ambalo wanafunzi wake wanamtambua mara moja. Yawezekana walimzoea akifanya hivyo kila walipokuwa wanakula pamoja. Aidha tendo hilo alilirudia karibuni tu kwenye karamu ya mwisho alipowaambia: “Fanyeni hivi kwa kunikumbuka mimi.” (Lk. 22:19).

Hapo hapo wale wanafunzi wawili wakaanza safari ya kurudi Yerusalemu, wale ambao walipokuwa wanakuja Emaus walikuwa wamechoka, na kuchanganyikiwa. Sasa wanarudi kwa mbio wakiwa na kiherehere cha kwenda kuwasimulia wenzao kwamba Yesu amefufuka, anaishi, na kwamba wao wameonana naye. Waliochoka kutembea sasa wanakimbia.

Kumbe umoja aina hii na Kristu unaleta nguvu mpya na ari mpya. Tunaalikwa kutanguzana na Kristu katika maisha yetu.

P. Alcuin Nyirenda



Tafakari ya neno la Mungu, Jumapili ya tatu ya Kipindi cha Pasaka


Mpendwa mwana wa Mungu ninakuleteeni tena furaha ya Pasaka kwa njia ya tafakari ya Neno la Mungu tukiwa tayari Dominika ya tatu ya Pasaka. Ujumbe wa Neno la Mungu Dominika hii ni ule usemao, "Wakamtambua katika kuumega Mkate". Katika somo la kwanza toka Kitabu cha Matendo ya Mitume tunapata kukutana na sehemu ya mahubiri ya Mtakatifu Petro. RealAudioMP3

Katika mahubiri haya Mtakatifu Petro akiwa amejawa na Roho wa Mungu na nguvu ya Pasaka anatangaza kuwa Kristu aliyedhihirishwa kwetu na Mungu na kuteswa na kisha kutundikwa msalabani, amefufuliwa na Mungu. Jambo hili ni la kweli na hakika, kwa maana sisi tu mashahidi. Mtakatifu Petro anashuhudia hilo akisema tulikula, na tukanywa pamoja naye na si hilo tu bali tumeshuhudia na kufuata mafundisho yake hadi anapofufuka.

Mpendwa msikilizaji, Mt Petro analenga kufundisha na kusimika imani katika Bwana mfufuka na tokea pale kuweza kusonga mbele katika utume kadiri Bwana alivyoagiza.

Mpendwa mwana wa Mungu, Mtakatifu Petro anasonga mbele akijaribu kuweka wazi mpango wa Mungu uliojificha katika kifo cha Bwana. Anakazia na anasema ni kweli kifo chake kilikuwa ni sehemu ya mpango wa Mungu. Katika hoja hii anajaribu kujibu maswali ya wale walioona kifo cha Kristu kama kikwazo na hasa wanapofikiri na kutambua kuwa yeye alikuwa Masiha! Anasema kile kinachoonekana kwetu kama makwazo na madhulumu kwa Mungu ni ishara ya ushindi! Kwa njia ya kifo kuna maisha mapya, yaani maisha ya ufufuko.

Katika somo II toka barua ya Mt Petro, (1Pet. 1:17-21) tunakutana na mwendelezo wa mafundisho juu ya ubatizo. Anawaambia wabatizwa wapya kwamba sasa wanao uwezo na nguvu za kumwita Mungu “Baba” kwa sababu wamepokea maisha mapya toka yeye. Ni zawadi kubwa na nono lakini pia inayo sehemu ya wajibu mkubwa nao ni kuwa mpya na daima kukaa katika hali ya utu upya! Mtakatifu Petro anasonga mbele akisema kwa kupata zawadi ya ubatizo na yote yaambatanayo na zawadi hiyo, mfano kumwita Mungu “Abba” kunatupasa kutambua kuwa kuna mmoja ambaye amelipia fidia.

Ndiyo kusema si kwa fedha wala dhahabu bali kwa DAMU YA MWANA WA MUNGU!, Damu ya Kristu mpakwa mafuta wa Bwana! Damu isiyo na doa la dhambi. Kumbe tumekombolewa kwa Damu ya thamani kuu mno! Yule kondoo ambaye Waisraeli walikuwa wakimchinja wakati wa sherehe za Pasaka ilikuwa ni kiashilio cha Kristu kondoo wa AJ ambaye anajitoa kwa ajili ya wokovu wa ulimwengu.

Katika somo III toka Mwinjili Luk 24:13-35, tunapata simulizi la wanafunzi 2 wa Emmaus. Mmoja wa wanafunzi hawa anaitwa Kleopa na mwingine jina lake halijulikani. Habari njema imewekwa katika mtindo wa katekesi, Ni Kristu mfufuka anafundisha watu wake na ndio sisi wenyewe na mafundisho ni juu ya ufufuko wake. Mwinjili Luka anamtaja mwanafunzi mmojawapo kuwa Kleopa ambaye kadiri ya tafiti za kibiblia alikuwa ni kaka yake na Yosefu, baba yake mlishi wa Yesu Kristu yaani Bwana.

Mwingine hatajwi jina, Luka akitaka kuacha nafasi kwa ajili yetu sisi ambao tunaalikwa kufuata nyayo zake tukimwelekea Bwana Mfufuka. Hawa wanafunzi wanakimbia toka Yerusalemu kwa maana matarajio yao hayakutimia. Walitarajia Masiha mshindi, mwenye nguvu, na mwenye kuishi maisha marefu na badala yake wanamwona akishindwa na kufa akiwa na miaka 33!.

Mpendwa msikilizaji, ndugu hawa wakiwa katika majadiliano ghafla Bwana ataingilia majadiliano yao na kuwauliza mnajadiliana nini? Hawa wanafunzi wawili wanasimama na kukasilika wakishangaa mtu huyu ni nani asiyejua kilichotokea Yerusalemu? Atawauliza tena kwani kumetokea nini?

Basi wanafunzi hawa watahadithia habari za Yesu Mnazareti jinsi alivyokuwa na uwezo mkuu lakini wakuu wa walimtia nguvuni na kumsulubisha! Wanafunzi hawa wanasema kwa kweli hatuoni tumaini tena na ndiyo maana tunakimbia! Mara kadhaa hata sisi tunalo tumaini fulani katika maisha, lakini inapojitokeza hatufaulu basi ni kuanza kulalamika na kukata tamaa kama ndugu hawa na hata wengine kuliacha Kanisa.

Angalia hali ya kisiasa kunakuwa na tumaini fulani kwa watu fulani na wanaponyamazishwa basi matumaini yetu huanguka pia! Hata hivyo mpendwa unayenisikiliza, mkristu anayeamini katika ufufuko hawezi kukatishwa tamaa na mikasa inayojitokeza katika maisha bali anasonga mbele kama Kristu mpaka Kalvari ambapo ndipo kuna ufufuko!

Mpendwa katika Bwana, wanafunzi wa Emmaus walikuwa na ujuzi juu ya Bwana lakini ujuzi wao uliishia katika kifo cha Bwana tu, hawakuweza kuendelea mbele! Hawakutambua kuwa Bwana alikuwa amefufuka na hiki ndicho kisa cha kukata tamaa, maana kama ni kifo tu, kwa hakika kinatisha na kukatisha tamaa. Ndiyo kusema nasi wakati fulani tunapoanza safari ya kumtafuta Bwana tunaishia kwenye kifo pasipo kwenda mpaka ufufuko na hapa ndo kuna taabu na mikato ya tamaa isiyohesabika! Tunaalikwa kwenda mbele mpaka ufufuko.

Hatupaswi kuishia katika kumwona Bwana kama mwana mapinduzi bali kama mwokozi wetu. Tunaalikwa kwenda mpaka ufufuko ambao huwezi kuufafanua kwa mahesabu bali kwa imani na hapa ndipo kuna hekima ya Kimungu. Wanafunzi wa Emmaus wana huzuni kwanza kuacha jumuiya yao ambamo wangeweza kupata majibu ya wasiwasi wao.

Shida nyingine hawakutaka kufanya utafiti juu Ya kile kilichosemwa na akina mama waliokwenda makaburini siku ya ufufuko. Pengine waliona kwa kuwa kimahesabu haiwezekani kukifafanua na hivi wanazama katika dharau na hili ni ukosefu wa imani! Leo hii katika Jumuiya yetu ya Kanisa kuna watu ambao kukitokea shida kidogo ni kuanza kukimbia wakifikiria wataweza kupata majibu na badala yake ni kukumbana na mkato wa tamaa na udhaifu wa kiroho kukua na kuongezeka. Fundisho katika hili ni kwamba yafaa siku zote kukaa na jumuiya na kutafuta suluhisho la matatizo yetu na ya Kanisa ndani ya Jumuiya yetu.

Mpendwa katika Bwana pamoja na kwamba ndugu hawa wawili wamekata tamaa na wanaujuzi nusunusu juu ya Bwana, Bwana hawaachi anaambatana nao na kuwasaidia polepole ili waweze kuelewa nini kilitokea na kwa nini ilikuwa vile. Hata kwetu hivi leo Bwana anatupa company tunapokuwa katika hali ya kukimbia matatizo na kukata tamaa. Ndiyo kusema nasi tuwape company kaka na dada zetu wakiwa katika taabu.

Mpendwa msikilizaji, ndugu hawa pamoja na kwamba Bwana amewasaidia katika shida yao ya kutoelewa vema maandiko matakatifu bado wanamwona kama msafiri mwenzao, mwenye shida kama wao. Mpendwa yatupasa kukazia lengo letu katika maisha, maana yake tukilipoteza hata mmoja anapojaribu kutueleza akili haipokei haraka.

Katika shida kama hii Bwana atafanyaje? Kwa hakika anaanza kuwafafanulia maandiko matakatifu kuanzia AK mpaka AJ linalomhusu yeye mwenyewe na hasa juu ya mateso hadi ufufuko wake. Ndiyo kusema Kwa njia ya Neno la Mungu mtu huweza kutambua mafumbo ya Mungu. Hata hivyo pamoja na hilo hawakuweza kuelewa kitu na Bwana atawakemea kwa mioyo migumu hiyo. Kwa hakika hata hivi leo shida ya kutoelewa na hasa kutoguswa na Neno la Mungu ipo, yafaa kuomba sana nguvu ya Roho Mtakatifu kwa ajili hiyo.

Mpendwa Bwana akiendelea na katekesi yake inafika jioni na anataka kuendelea mbele wakati wanafunzi wamefika. Basi wanamkaribisha nyumbani walipokuwa wanaenda na kisha ataketi chakulani pamoja nao na KUUMEGA MKATE na kuwapatia. Kwa tendo la kuumega mkate macho yalifunguka na wakamtambua kuwa ni BWANA MFUFUKA na mara atatoweka! Swali linawajia kwa nini hatukumtambua alipokuwa anatufafanulia Maandiko Matakatifu? Basi mara moja ndugu hawa walirudi Yerusalemu kwa furaha bila wasiwasi tena na kutangaza habari njema wakisema tumemwona Bwana mfufuka na kweli amefufuka.

Mpendwa katika Bwana simulizi la wanafunzi wa Emmaus kadiri ya Mt. Yustini ni chimbuko la mpango wa Misa Takatifu. Waamini kuingia mapema katika ibada, hii ni sawa na wanafunzi wa Emmaus kuwa njiani tokea Yerusalemu, kuingia kwa Padre kwa maandamano ni ishara ya kuingia kwa Kristu masiha katika majadiliano ya wanafunzi hawa. Mahubiri ni ishara ya ufafanuzi wa Neno la Mungu uliofanywa na Bwana mfufuka na Litrujia ya Ekaristi Takatifu yaturudisha katika ishara ya Kristu kuumega mkate na kuwapa wanafunzi wa Emmaus.

Mwishoni mwa Misa Padre huondoka kwa maandamano toka kwenye Misa kabla ya waamini wengine, hii yaturudisha katika lile tendo la Bwana kutoweka mara baada ya kumega mkate na kuwapatia. Wanafunzi wa Emmaus walipoelewa haya, walirudi Yerusalemu wa furaha kutangaza furaha ya ufufuko. Mpendwa, wewe je baada ya kuumega mkate waondoka katika Misa kwa furaha kwa ajili ya kutangaza kwa wengine au warudi nyumbani kwa huzuni? Tafakari hili!
Nakutakieni furaha tele katika kipindi chote cha Pasaka na Mungu azidi kuwa nawe, nawe ukitekeleza mapenzi yake katika Jumuiya ukienda kutangaza habari ya ufufuko wa Bwana kwa furaha kuu. Tukutane tena Dominika ijayo. Tumsifu Yesu Kristo. Tafakari hii imeletwa kwako na Padre Richard Tiganya C.PP.S.

Mtakatifu Yosefu Mfanyakazi, Utuombee!

JANA ilikuwa Siku kuu ya Wafanyakazi Duniani, maarufu kama Mei Mosi ni fursa inayotolewa na Jumuiya ya Kimataifa kila mwaka kwa wafanyakazi kufanya tathimini ya kina kuhusu kazi walizotenda, ufanisi na tija katika shughuli za uzalishaji na utoaji wa huduma pamoja na kujiwekea malengo kwa siku za usoni kwa kukazia umuhimu wa ushirikishwaji wa wadau mbali mbali katika kazi.

Katika mazingira ya utandawazi usiojali mateso na mahangaiko ya watu, kuna haja ya kuanzisha na kuimarisha mshikamano wa kidugu unaojengeka katika vyama vya ushirika miongoni mwa wafanyakazi, kwa kutambua na kuendelea kudumisha sheria, kanuni na usalama kazini. Mishahara mizuri, mazingira safi na bora ya kazi pamoja na vitendea kazi vizuri ni mambo ambayo yanaweza kuchangia katika maboresho na ufanisi kazini sanjari na ukuzaji wa pato la wafanyakazi.

Ubadhirifu wa mali ya umma, ufisadi, wizi na hujuma kazini ni mambo ambayo daima yamekwamisha ufanisi kazini na matokeo yake ni watu kuendelea kukomaa katika ubinafsi na utandawazi wa kutojali wala kuguswa na mahangaiko ya jirani. Siku kuu ya Wafanyakazi Duniani, iwe ni fursa ya kukuza na kuimarisha sheria za kazi, utawala bora na usalama kazini.

Siku kuu ya Wafanyakazi imewekwa chini ya ulinzi wa Mtakatifu Yosefu Mfanyakazi. Siku kuu hii ndani ya Kanisa ilianzishwa kunako mwak 1955 na Baba Mtakatifu Pio wa kumi na mbili. Lengo ni kutambua heshima ya kufanya kazi kama sehemu ya utimilifu wa utu na heshima ya binadamu. Huu ni mwendelezo wa kuutiisha ulimwengu, ili uweze kuwa ni mahali pazuri zaidi pa kuishi. Watu wanapaswa kutambua kwamba, kazi ni sehemu muhimu sana katika maisha ya mwanadamu kwani ni sehemu ya ubinadamu na matokeo ya kazi.

Utu na heshima ya mwanadamu ndicho kipimo sahihi cha heshima ya kazi. Kazi ni wajibu na utambulisho mwa wanadamu na kwamba, nguvu kazi ina kipaumbele cha kiasili zaidi ya mtaji, kumbe, kuna haja ya kuwa na uhusiano unaokamilishana kati ya kazi na mtaji, lakini utu na heshima ya binadamu vipewe kipaumbele cha kwanza.




Watakatifu wapya, miamba ya huruma ya Mungu !

Baada ya Baba Mtakatifu Francisko kuwatangaza Wenyeheri Yohane XXIII na Yohane Paulo II kuwa watakatifu, Jumapili tarehe 27 Aprili 2014 katika Ibada iliyohudhuriwa na maelfu ya watu waliokuwa wamefurika kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican pamoja na viunga vyake, watakatifu hawa wapya watakumbukwa kila mwaka mwezi Oktoba kadiri ya Kalenda ya Liturujia ya Kanisa.

Kadiri ya Kalenda ya Liturujia ya Kanisa kwa ajili ya kumbu kumbu ya Watakatifu, Yohane XXIII atakumbukwa kila mwaka ifikapo tarehe 11 Oktoba. Hii ni siku maalum ambayo, kwa takribani miaka hamsini iliyopita, Yohane XXIII alikuwa anafungua rasmi maadhimisho ya Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican, tukio ambalo limeleta mabadiliko makubwa katika maisha na utume wa Kanisa katika mapambazuko ya Millenia ya tatu ya Ukristo. Hili ni tukio la kishujaa lililomstahilisha Papa Yohane XXIII kuitwa Mtakatifu.

Mtakatifu Yohane Paulo II atakumbukwa kila mwaka ifikapo tarehe 22 Oktoba. Hii ni siku ambayo Papa Yohane Paulo II alipoanza utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro, akaendeleza maadhimisho ya Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican pamoja na kukazia umuhimu wa Mama Kanisa kujikita katika mchakato wa Umissionari na Uinjilishaji Mpya. Mwezi Oktoba ni mwezi wa shughuli na mikakati ya kimissionari ndani ya Kanisa.

Tangu sasa waamini na watu wenye mapenzi mema wanaweza kuwaenzi watakatifu hawa wapya kwa maadhimisho ya: Ibada, Liturujia pamoja na kuwaweka kuwa walinzi na wasimamizi wa shughuli mbali mbali katika maisha na utume wa Kanisa. Itakumbukwa kwamba, Mtakatifu Yohane Paulo II atakuwa ni msimamizi wa Siku za Vijana Duniani.


Papa Francisko anawaalika vijana kutoka kimasomaso kukutana na Yesu Mfufuka!


Vijana wanaalikwa kumwangalia kwa namna ya pekee kabisa yule kijana tajiri anayesimuliwa kwenye Maandiko Matakatifu aliyemwendea Yesu akiomba ushauri ili aweze kuurithi uzima wa milele. Mitume wengi walikuwa ni vijana na walifurahia sana walipokutana na kuzungumza na Yesu, kiasi hata cha kuwabadilishia mwelekeo wa maisha, kwani waliweza kusikiliza ufafanuzi wa Neno la Mungu kwa kina na mapana!

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake wa video kwenye maadhimisho ya Siku ya Vijana Kikanda nchini Argentina, iliyoadhimishwa, Jumamosi tarehe 26 Aprili 2014 nchini Argentina, katika mkesha wa kuwatangaza Wenyeheri Yohane XXIII na Yohane Paulo II kuwa watakatifu, anawauliza vijana, jinsi walivyojisikia kwa mara ya kwanza walipokutana na Yesu katika hija ya maisha yao ya kiroho, Anawaalika kuwaangalia Mitume waliokutana na Yesu kwa mara ya kwanza katika maisha yao.

Yesu alionesha upendo wa pekee kwa yule kijana tajiri aliyejitahidi katika maisha yake kushika Amri za Mungu, lakini akisoka ndani mwake ufukara wa maisha ya kiroho, ndiyo maana anapoambiwa kwenda kuuza vyote alivyonavyo na kuwapatia maskini, kisha amfuate Yesu, anashikwa na huzuni kubwa katika moyo wake.

Baba Mtakatifu Francisko anasema, Maandiko Mataktifu yamesheheni mifano ya vijana wa kina aina. Anawakumbusha yule kijana aliyeomba urithi kutoka kwa Baba mwenye huruma, kisha akatokomea mjini kwenda kuponda mali na baadaye akakiona cha mtema kuni kwa kukumbana na uso kwa uso na baa la njaa! Hapa akajifunza kutubu na kuongoka, ili kukimbilia tena huruma ya Mungu. Daima Baba yake alikuwa anamsubiri kwa hamu kubwa, kuona kijana wake akirudi tena nyumbani. Siku ile aliporejea nyumbani, akamkumbatia na kumwonjesha tena huruma na upendo usiokuwa na kifani.

Baba Mtakatifu amewakumbusha vijana wa Argentina kuhusu yule kijana wa Naini aliyekuwa amefariki dunia baadaye akafufuliwa na Yesu, kwa kumwonea yule mama mjane huruma? Baba Mtakatifu anawauliza vijana wao wanajisikia kuwa sehemu gani kati ya vijana wanaosimuliwa kwenye Injili? Je, wanaonesha ari na shauku ya kuwashirikisha wengine ushuhuda wa kukutana na Yesu? Au wamekata tamaa na kujikunyata? Au pengine tayari wamekwisha kupoteza maisha ya kiroho ndani mwao?

Baba Mtakatifu Francisko anawahamasisha vijana kuendelea kuwa waaminifu kwa Kristo na Kanisa lake, kwa kutolea ushuhuda wa imani katika matendo, ili kujenga na kuimarisha amani na furaha inayobubujika kutoka kwa Kristo na Kanisa lake sanjari na kukumbatia Injili ya maisha pamoja na kuguswa na mahangaiko ya wengine kama alivyofanya Bikira Maria kwenye arusi ya Kana na mwishoni akasimama chini ya Msalaba wa Kristo.

Baba Mtakatifu Francisko anawataka wasichana kuiga mfano wa Bikira Maria na wanawake watakatifu wanaosimuliwa katika Injili kwa kutolea ushuhuda wa imani yao kwa Kristo na Kanisa lake, wakimwachia Yesu nafasi ya kuwaongoza, ili waweze kukua na kukomaa, tayari kuwahudimia Watu wa Mungu katika medani mbali mbali za maisha.

Baba Mtakatifu amewatakia kheri na baraka vijana hao katika maadhimisho ya Siku ya Vijana wa Argentina Kikanda, ili wapate nafasi ya kukutana na Yesu katika hija ya maisha yao, bila kuwa na woga wala makunyanzi, bali wangalie Yesu na Bikira Maria, ili waweze kusonga mbele, tayari kukimbilia huruma na upendo wa Mungu kwa watu wake.