Week Hot newz

Njooni tumwabudu Mtoto Yesu! Mwaka 2014



Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii anawakumbusha kwamba, wanapotafakari sura ya Mtoto Yesu, wanatafakari pia uso wa Mwenyezi Mungu. Mwaliko wa kwenda kumwabudu! na kukaribisha Mwaka 2014.

Padri atahadharisha ndoa za jinsia moja, uzazi wa mpango


Geita
Imeelezwa kuwa kuna hatari ya familia kwa nchi zinazoendelea ikiwamo Tanzania kufikia ukomo wa ustawi na furaha na pamoja na kujenga taifa lisilo na uhai wa nguvu kazi na lenye maadili kutokana na ndoa za jinsia moja zinazoshika kasi katika mataifa ya Ulaya na Amerika.

Padri wa Kanisa Katoliki nchini amesema kuwapo kwa mazingira hayo matokeo yake ni watu kukoma kuzaa watoto na kukosa familia.

Familia ina dhamana kubwa kwa Kanisa na Jamii, ingawa inakabiliwa na changamoto nyingi!



Maadhimisho ya Siku kuu ya Familia Takatifu ya Yesu, Maria na Yosefu ni kielelezo cha upendo mkuu ambao Mwenyezi Mungu amemwonesha mwanadamu kwa kutaka Mwanaye wa Pekee, Yesu Kristo azaliwe katika familia ya binadamu, akiwa na Baba na Mama kama binadamu mwingine yoyote yule!

Liturujia ya Neno la Mungu inaonesha jinsi ambavyo Familia Takatifu ilivyoteseka hadi kukimbilia uhamishoni Misri ili kuokoa maisha ya Mtoto Yesu

Sherehe ya Familia Takatifu ya Yesu, Maria na Yosefu



Mpendwa mwana wa Mungu, leo tunasherehekea na kushangilia sherehe ya familia Takatifu. Masiha amezaliwa ndani ya familia hii. Ndani ya familia hii kuna majukumu ya kutekeleza ili Mwana wa Mungu akae mahali stahili na kwa namna hiyo atufundisha namna ya kutenda na kuishi kwenye familia zetu.

Somo la kwanza toka kitabu cha Hekima ya Yoshua bin Sira linaweka mbele yetu fahari na heri ya kuwaheshimu wazazi na kuwatunza katika uzee wao. Heri ambazo ziko wazi kadiri ya somo hili ni kuwa na uzao, na si uzao tu bali kufurahia uzao huo. Kuwa na maisha marefu na uzee wa kusifika. Kwa kuwatunza wazazi na kuwapa heshima stahili mmoja afanya malipizi ya dhambi zake. Kwa hakika somo hili lasisitiza na kuweka mkazo juu ya amri ya nne ya Mungu. Waheshimu baba na mama upate miaka mingi na heri duniani

Viongozi wa serikali waombewa msamaha kwa Mungu

28th December 2013

Waumini wa huduma ya Mtakatifu Prince Mission yenye Makao Makuu yake Sinza jijini Dar es Salaam, wameomba msamaha wa Mungu kwa baadhi ya viongozi  wa umma kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni kuusaliti umma wanaoungoza.

Hatua hiyo inatokana na matumizi ya misahafu wanapokula viapo vya kuutumikia umma, kisha kutotimiza azma hiyo badala yake kujinufaisha binafsi na ‘kuwaangamiza’ raia wanaowachagua.

Papa mstaafu Benedikto XVI apata chakula cha mchana na Baba Mtakatifu Francisko



Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI, Ijumaa, tarehe 27 Desemba 2013 amemtembelea Papa Francisko na kupata chakula cha pamoja kwenye Hosteli ya Mtakatifu Martha iliyoko mjini Vatican.

Francis prepares to celebrate first Christmas as Pope


Pope Francis marks his first Christmas as leader of the world's Roman Catholics on Tuesday and Wednesday, with crowds of pilgrims expected to attend the annual celebrations in the Vatican.


"Like the Virgin Mary, the Church this week is expecting a birth," the pope said on Monday in the homily at one of his daily masses in the Vatican residence, where he has been staying since his election in March.
"Is there space for the Lord or is there space only for parties, shopping and making noise?" he asked.
The Christmas festivities begin with the unveiling on St Peter's Square of a traditional Nativity scene named in honour of Latin America's first ever pontiff at 1530 GMT.
The 77-year-old Francis is expected to watch the ceremony from the window of the Apostolic Palace overlooking the square and light a candle for peace.
Then from 2030 GMT the Argentine will celebrate the solemn Christmas Vigil mass in St Peter's Basilica.
On Wednesday, Francis delivers the "Urbi et Orbi" ("To the City and the World") blessing at 1130 GMT on St Peter's Square -- where he first appeared after his momentous election by fellow cardinals on March 13.
Popes often use their "Urbi et Orbi" blessings to announce specific prayers, for instance, for the victims of conflicts or for global economic justice.

Papa Francis atetea wanyonge wa vita


Papa Francis akipungia mkono waumini Vatikani
Katika hotuba yake ya mwanzo ya Krismasi, Papa Francis amezungumza mjini Rome juu ya maeneo ya vita duniani.
Alitoa wito kwa pande zote zilizohusika na vita vya Syria ziruhusu msaada kufika kwa wanyonge.
Alisema:
"Maisha mengi yamevunjika katika vita vya Syria na kuchochea chuki na kulipiza kisasi.

"Hakuna Krismas bila Mama... Bikira Maria"

Padre Faustin Kamugisha katika Kitabu chake cha "Hakuna Krismas bila Mama... Bikira Maria" anasema baraka zitasimama ikiwa kama Jamii itamsahau mama. Mama ni nambari moja na wala hana mpinzani. Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa Bikira Maria Mama wa Mkombozi, siku moja Mama mmoja alipaza sauti akamwambia Yesu, "heri tumbo lililokuchukua na maziwa uliyonyonya"

Hizi ni sifa kwa Bikira Maria Mama wa Mungu, anayestahili kuheshimiwa hasa wakati huu, tunapoadhimisha Siku kuu ya Noeli. Mwenyeheri Yohane Paulo wa pili aliwahi kusema kwamba, wanawake ni walimu wa amani. Hawa ni wale wanaosimama kidete kupinga nyanyaso na kutoheshimiwa; ni watu wanaokumbatia Injili ya Uhai. Bikira Maria Mama wa Yesu, amepewa sifa ya kuitwa Malkia wa amani. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, alitunza zawadi ya Uhai, changamoto kwa wanawake wote kusimama kidete ili kulinda na kutetea Injili ya Uhai.

Mama Theresa wa Calcutta aliwahi kusema kwamba, wavurugaji wa amani leo hii ni wale wanaokumbatia utamaduni wa kifo unaokumbatia sera za utoaji mimba na kutowajali wanyonge na watu wasiokuwa na mtetezi. Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa ajili ya Siku ya Kuombea Amani kwa Mwaka 2014 anasema, Fumbo la Msalaba linawawajibisha binadamu kutaabikiana na kusumbukiana katika maisha kwani udugu unazima vita na madhara yake; udugu unaponya na kuganga mapungufu ya binadamu.

Kipindi cha Noeli kiwasukume wanawake kutolea ushuhuda wa sifa njema za kimama, kwa kuiga mfano wa Bikira Maria. Umama ni kazi nzito kama ambavyo aliwahi kusema Mwenyeheri Yohane Paulo wa Pili; kwani hawa ni wadau wakuu wa matunzo na makuzi kwa watoto wao: kiroho na kimwili. Mwanamke anayetunza watoto wake nyumbani kwa imani na mapendo makuu anafanya kazi halisi na yenye thamani kubwa katika Jamii. Wanawake wawe mstari wa mbele kutangaza Injili ya Uhai kwa njia ya ushuhuda wa maisha yao; na kwa kutimiza nyajibu zao kwa Familia na Jamii na Jamii pia ioneshe hali na moyo wa kuwajali na kuwasaidia wanawake.

Bikira Maria awe ni mfano wa tunza bora ya kimama kwa watoto kama alivyofanya kwa Mtoto Yesu, tangu alipozaliwa hadi pale aliposimama chini ya Msalaba akamwona Mwanaye akihitimisha kazi ya Ukombozi. Bikira Maria ni mwanamke wa imani na mfano bora wa kuigwa. Kwa kumwangalia Bikira Maria, mwamini anaweza kujifunza tena kujiachilia mikononi mwa Mwenyezi Mungu; ni Mama wa Matumaini hata pale ambapo hakuna tena cheche za matumaini.

Kwa kumwangalia Bikira Maria, waamini wajifunze kumpenda Mtoto Yesu na kwa njia hii, Bikira Maria anakuwa kweli ni Mama wa Mungu na Kanisa. Hongera Bikira Maria kwa kutuzalia Mtoto mwanaume, mwenye Ufalme na uku
u mabegani mwake!

Tafakari ya Neno la Mungu, Siku kuu ya Noeli, 2013

Mpendwa mwanatafakari, kwanza ninakutakieni heri na baraka tele za kuzaliwa Mwana wa Mungu.
Leo ni Krismas, ni Noeli, ni neema ya Mungu iliyofunuliwa kwa ulimwengu mzima. Kwa hakika ile ahadi ya Mungu aliyoitoa tangu zamani sasa imefunuliwa na hivi tunafurahi na kushangilia tukiimba utukufu kwa Mungu juu na amani duniani kwa watu wenye mapenzi mema. Mtoto Emanueli aliye na uweza wa kifalme mabegani mwake, Mungu pamoja nasi amezaliwa kwa ajili yetu. Kanisa duniani kote linaimba “pangoni Batlehemu amezaliwa Mtoto Yesu, twendeni sote tukamwone na kumpa zawadi”

MERRY CHRISTMAS – HERI KWA NOELI!


Kristmas ni Birthday ya mmoja katika UTATU aliyetumwa kufanya kazi kwenye sayari hii inayoitwa dunia. Hebu tujaribu kupiga twasira. Siku moja, huko mbinguni kulikuwa na mkutano wa Halmashauri kuu ya Utatu Mtakatifu.

Ajenda kuu ya mkutano ilihusu kuizungumzia sayari dunia. Hasa kutokana na mabadiliko makuu yaliyokuwa yanajitokeza hapa na pale baada ya uumbaji. Ikabidi

Ombi la Papa Francisko kwa niaba ya familia zisizo na nyumbani.



Baba Mtakatifu Francisko , Jumapili iliyopita, baada ya sala ya Malaika wa Bwana, alitoa ombi kwa watu wote, binafsi, Taasisi, Makampuni na mamlaka, kujali mahangaiko na mateso ya watu wasiokuwa na makazi maalum yaani wasiokuwa na nyumbani. Papa aliotoa ombi hili kwa niaba ya familia zisizo na makazi , mbele ya mahujaji na wageni waliokuwa wamekusanyika katika uwanja wa kanisa kuu la Mtakatifu Petro,Vatican.

Taarifa inabaini Papa alitoa wito huo kwa kuhamasishwa na

Maisha Mchanganyiko: Nani kama Mama!



Zikiwa zimebaki siku tatu, kuadhimisha tukio la Mama Bikira Maria kutuzalia Mtoto Yesu , Emannuel, Mkombozi wa Dunia, inafaa kwa wakati huu kumtafakari Mwanamke, mama mzazi, hadhi yake, wajibu wake na Kanisa lasema nini juu mwanamke mama mzazi.
Ni wazi kipindi cha Krismas, ni wakati wa hekaheka nyingi za katika jamii , na familia pia. Nyuso nyingi huonekana kuwa na furaha, na pia ndani ya familia, huonekana mshikamano zaidi, ambamo licha ya hamu ya kusubiri ibada ya kusisimua ya

Tafakari ya Neno la Mungu, Jumapili ya IV ya Kipindi cha Majilio



Hatuna budi kumshukuru Mungu kwa kutujalia tena siku nzuri kama hii na hasa tunapoijongea meza ya Neno lake. 

Ni Dominika ya IV ya Kipindi cha Majilio, tukikaribia kuzaliwa kwa Mwana wa Mungu, Mfalme wa amani, Mtoto Emanueli. Katika somo la kwanza tunapata kusikia kuwa Mungu atatoa ishara na hapa ndipo kuna mzizi na kiini cha masomo ya Dominika hii. Basi ishara yenyewe ni Mtoto Emanueli yaani Mungu pamoja nasi.

Mpendwa msikilizaji wa Neno la Mungu, katika somo la kwanza

West Ham yapeleka majanga Spurs.



West Ham wakipambana na Tottenham
Mabao mawili katika dakika 10 za mwisho yaliipa ushindi West Ham dhidi ya Tottenham na kuiwezesha kuingia nusu fainali ya kombe la Capital One ambapo itapambana na Manchester City. Tottenham walifungua mlango katika nusu ya pili wakati Emmanuel Adebayor alipofunga bao lake la kwanza tangu mwezi wa Mei.
Westham walisawazisha kupitia kwa Matt Jarvis na zikiwa zimesalia dakika tano mchezo huo kumalizika, Modibo

Mkalimani wa mazishi ya Mandela awa chizi


Thamsanqa Jantjie, mkalimani wa lugha ya ishara
Mkalimani wa lugha ya ishara katika siku ya mazishi ya kitaifa, ya aliyekuwa rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, amelazwa katika hospitali ya magonjwa ya ya akili.
Mkalimani huyo anashutumiwa kutoa ishara ambazo hazikuendana na kile kilichokuwa kikiongelewa.
Thamsanqa Jantjie "anaweza kuwa na matatizo", amekaririwa mke wake Siziwe akisema hayo.
Wataalam wa lugha ya ishara wamemshutumu kwa

Noeli ni Siku kuu ya imani



Na Paskal Linda,Vatican.
19/12/2013
Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 18 Desemba 2013 amefanya mazungumzo na Papa mstaafu Benedikto XVI, ili kutakiana kheri na matashi mema kwa ajili ya Siku kuu ya Noeli na Mwaka Mpya wa 2014. Baba Mtakatifu amekumbusha kwamba,

Chelsea yachapwa na Sunderland


Sunderland imesonga mbele hatua ya nusu fainali ya michuano ya ya Kombe la Capital One baada ya kuichapa Chelsea mabao 2-1.
Chelsea ilimiliki mchezo huo kwa muda mrefu katika dakika zote 90, huku Chelsea ikipata goli kutokana na mchezaji wa Sunderland, Lee Cattermole kujifunga mwenyewe.
Chelsea walionekana kufuzu kucheza hatua ya nusu fainali hadi dakika za mwisho za mchezo,

Noeli iwe ni siku kuu ya imani na matumaini; mapendo na amani

Baba Mtakatifu Francisko katika Katekesi yake, Jumatano, tarehe 18 Desemba 2013, amewakumbusha waamini kwamba, siku hizi za mwisho mwisho za Kipindi cha Majilio ni mwaliko kwa waamini kujiandaa kiroho ili kumpokea Yesu anayezaliwa tena katika maisha yao.

Baba Mtakatifu anasema, Noeli ni Siku kuu ya furaha na matumaini kwa Mwenyezi Mungu ambaye ameamua kuja na kuishi kati ya watu wake kwa njia ya Mwanaye wa

Mzee Nelson Mandela alikuwa pia shujaa wa Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa Baba wa Demokrasia ya Afrika Kusini, Mzee Nelson Mandela alikuwa pia kiongozi wa Tanzania, shujaa wa Watanzania na Baba wa wananchi wa Tanzania kama alivyokuwa kwa wananchi wa Afrika Kusini.

Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa Tanzania na Afrika Kusini zina uhusiano wa kindugu na wa karibu sana kwa sababu ya kazi kubwa iliyofanywa na waanzilishi wa mataifa hayo mawili, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na Mzee Mandela.