- Kitaalamu, mtindio wa ubongo unaelezwa kuwa ni hali inayompata mwanadamu kwa ubongo wake kushindwa kufanya kazi katika utaratibu wa kawaida. Kimsingi, ni uwezo wa ubongo kutokukua vizuri na kushindwa kufanya kazi yake katika mazingira yake ya kawaida.
Inaelezwa pia kwamba, watoto hawa wanaweza kubadilika, iwapo tu watafundishwa kwa makini, utulivu na uvumilivu mkubwa.
Mtu anayemfundisha mtoto wa aina hii hatakiwi
kamwe kuwa na hasira, na pia inashauriwa sana kuwapongeza wanapofanya
vizuri japo kidogo.
Kejo anasema mwalimu anatakiwa awe mpole na
ufundishaji wake usiwe wa haraka haraka, aonyeshe mapenzi kwa mtoto,
hapaswi kumkemea hata kama anakosea. “Utakuta mwingine hacheki, au
anatoka udenda lakini kama akicheza akili inajitengeneza na inaweza
kufikia mate yanakatika na hata kucheka na wakati mwingine hurudi katika
hali ya kawaida,” anasema.
Watoto wa aina hii inashauriwa wapewe nafasi ya kujenga urafiki na watoto wenzao wa rika lao.
Awali, watoto wenye matatizo ya akili walikuwa wanatengwa na watoto wenzao katika madarasa, kwa kuwekwa kwenye madarasa maalum.
Siku hizi inashauriwa kuwa watoto hao wachanganywe
na wanafunzi wenzao wasio na matatizo ya akili, japo hata kwa nusu
siku. Utaratibu huu hujulikana kitaalamu, mainstreaming.
Mbali na hayo, inaelezwa pia kuwa wakati mwingine
watoto kabla ya kufikwa na hali hiyo ya ulemavu wa akili, wakati
mwingine huzaliwa njiti (premature) ambayo mara nyingi mtoto huwa na
udhaifu wa viungo.
Matatizo ya uzazi, na uzazi usio salama hufanya
mtoto kuzaliwa kabla ya wakati na hiyo husababisha ulemavu wa akili
kwani wakati mwingine ukuaji wa ubongo hauwi katika mazingira ya
kawaida.
Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Save
the Children, Steve Thorn anasema watoto 210,000 huzaliwa kila mwaka na
watoto wa kiume ama hufa au kupata ulemavu kwa kuzaliwa kabla ya
wakati.
Anasema kwa mwaka jana pekee, watoto wa kiume
njiti 114,000 walizaliwa ikilinganisha watoto wa kike 97,000 na kuongeza
idadi ya vifo ama wakati mwingine kupatwa na matatizo ya upofu, uziwi
na mtindio wa ubongo.
Dk Daphne Austin wa Mtandao wa Kamisheni ya Afya
ya Jamii Uingereza anasema hana shaka kuwa watoto njiti hukua vizuri
hadi kufikia wiki 23, 24 na 25 lakini wengi wao hupatwa na ulemavu wa
viungo na ubongo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni