Week Hot newz

P- square Live in Dar, Bwana Arusi Pater Okoye ndani



Embedded image permalink
P-square live jijini Dar es salaam kwa show ya kesho picha ya pamoja na wasaniii wa nchini Tanzania.
Pater Okoye akiwa na Diamond Lagosi, Pater Okoye ndio msanii wa P- square ambaye amepata jiko hivi majuzi naye ndio amekuja Dar kwa show.


Wanamuziki wa kundi la P-Square Peter na Paul baada ya kutua jijini Dar usiku wa kuamkia leo. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkrulu ambao ndio wadhamini wakuu wa onesho lao ambalo limeratibiwa na East Africa Radio na EATV.
 
 Hapa wakifanya mahojiano na kituo cha East Africa TV ambao ndio wenyeji wao.
Mahojiano na picha za hapa na pale zikiendelea.


kupagawisha kesho

Nyota wa muziki wa Nigeria, Peter na Paul Okoye wanaounda Kundi la P-Square wamewasili nchini Tanzania.

Nyota wa muziki wa Nigeria, Peter na Paul Okoye wanaounda Kundi la P-Square wamewasili nchini Tanzania juzi usiku majira ya saa 5 kwa ajili ya kutoa burudani kwa Watanzania na wengine wengi kutoka nchi mbalimbali katika tamasha kubwa linalotarajiwa kufanyika kwenye Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es Salaam kesho.

Kundi hilo la wanamuziki mahiri lilikuja nchini kwa mara ya kwanza 2008 katika tamasha lililofanyika kwenye viwanja hivyo hivyo na kuteka maelfu ya Watanzania walioburudika na kufurahi kwa burudani zao.

Kampuni ya huduma za simu ya Vodacom Tanzania ni moja kati ya wadhamini wakuu wa tamasha hilo linalotarajiwa kuwaleta pamoja wateja wake wote na Watanzania kwa ujumla na kuwapa burudani waliyokuwa wakiisubiri kwa muda mrefu.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa akizungumzia shoo ya wanamuziki hao wenye mafanikio kutoka nchini Nigeria, alisema hilo ni moja ya matamasha makubwa ya burudani kuwahi kufanyika nchini.

“Ujio huu wa wanamuziki wa Kundi la P-Square ulikuwa ukisubiriwa kwa hamu na wapenda burudani wengi nchini. Siku zote kampuni yetu imekuwa mstari wa mbele kuunga mkono shughuli za michezo na burudani nchini na hivyo kuwa chaguo nambari moja na la pekee kwa wateja wetu.

Tunaahidi kushirikiana na wadau mbalimbali wa burudani kuhakikisha tunawaletea kilicho bora wateja wetu, hakuna asiyefahamu kuwa kundi hili ndilo linaloongoza Afrika kwa kuwa na mialiko mingi duniani kutokana na ubora wake,” alisema Twissa.

Wasanii hao wameletwa nchini kwa ushirikiano mkubwa wa udhamini wa Vodacom Tanzania pamoja na East Africa Radio na TV na watatumbuiza pamoja na nyota kadhaa wa muziki wa Tanzania wakiwamo Profesa Jay, Lady Jaydee Ben Pol na Joh Makini.

Alisema kwa ambao hawajanunua tiketi hadi sasa wanachelewa kwani zitakwisha. Alisema kwa sasa tiketi zinapatikana kwa fedha taslimu Sh.35,000 tu kwenye maduka mbalimbali kila wilaya.

Alisema Kinondoni zinapatikana Engine Petrol Station Mbezi Beach, Image View Tegeta, Puma Petrol Station Mwenge, Samaki Samaki, Photo Point – Mlimani City, Hill Park Restaurant – UDSM, Zizzou Fashion Sinza, Rose Garden Mikocheni, Photo Point Mayfair, Best Bite Namanga, Le Tasi Lounge Coco Beach.

Kwa Ilala, alisema tiketi zinauzwa Steers, Samaki Samaki - Samora, Break Point Bar iliyo jirani na Club Billicanas, Photo Point, Ambassador Lounge - Mkapa Towers, Photo Point Quality Centre.

Temeke tiketi zinauzwa TCC Club Chang’ombe, Dar Live Mbagala, Mafuvu Baby Barber Shop Mtoni, na Kisuma (zamani Sugar Ray).
 Photo: Kumekucha.....# press conference at Hyatt #p square live in DAR



P-square wakiwa mbele wa vyombo vya habari . kwa maojiano zaidi  tayari kwa kazi ya kesho



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni