Baraza la Maaskofu Katoliki Angola, Sao Tome na Principe linasema, sera za utoaji mimba ni mauaji ya watu wasiokuwa na hatia, ni kinyume cha Amri za Mungu; utamaduni na utambulisho wa wananchi wa Angola. Wananchi wanakumbushwa kwamba, maisha ya
binadamu ni matakatifu tangu pale mtoto anapotungwa mimba tumboni mwa mama yake hadi mauti ya kawaida yanapomfika kadiri ya mapenzi ya Mungu.
Hakuna mtu mwenye mamlaka yanayomruhusu kuwapokonya wengine zawadi ya uhai kwa kisingizio chochote kile. Ni jukumu na dhamana na wanafamilia, wahudumu wa sekta ya afya na wanasiasa kutoruhusu wala kushabikia sera za utoaji mimba na badale yake, wawe mstari wa mbele kulinda na kutetea zawadi ya uhai kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Maaskofu wanasema kwamba, kadiri ya mila na tamaduni za wananchi wa Angola katika ujumla wao, vitendo vya utoaji mimba havikubaliki kamwe kwani ni kielelezo cha mkosi katika familia. Hii ni changamoto kwa waamini na watu wenye mapenzi mema kusimama kidete kulinda na kutetea Injili ya uhai, kwani sera dhidi ya Injili ya uhai ni kutaka kusababisha majanga katika Jamii
.
Ni matumaini ya wananchi wa Angola kwamba, wabunge wao watasimama kidete kulinda na kutetea zawadi ya uhai na kamwe hawatakubali kushinikizwa ili kuunga mkono sera za utoaji na vizuia mimba.
Week Hot newz
-
SIKU moja baada ya kifo cha Rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, Mzee Nelson Mandela (95), mazishi yake yanatarajiwa kufanyika wiki m...
-
Baba Mtakatifu Francisko katika tafakari yake kwa Jumapili ya tatu ya Kipindi cha Majilio, anawaalika waamini na watu wote wenye mapenzi ...
-
Na Paskal Linda,Vatican. 19/12/2013 Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 18 Desemba 2013 amefanya mazungumzo na Papa ms...
-
Mpendwa mwana wa Mungu, leo tunasherehekea na kushangilia sherehe ya familia Takatifu. Masiha amezaliwa ndani ya familia hii....
-
Ndege iliyokuwa imetekwa Rubani msaidizi wa ndege ya abiria ya shir...
-
Na Dina Ismail, Dar es Salaam MSANII wa muziki wa asili nchini, Pascal linda maarufu kama Batarokota amewaomba mashabiki wa muziki nc...
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni