Week Hot newz
-
SIKU moja baada ya kifo cha Rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, Mzee Nelson Mandela (95), mazishi yake yanatarajiwa kufanyika wiki m...
-
Baba Mtakatifu Francisko katika tafakari yake kwa Jumapili ya tatu ya Kipindi cha Majilio, anawaalika waamini na watu wote wenye mapenzi ...
-
Na Paskal Linda,Vatican. 19/12/2013 Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 18 Desemba 2013 amefanya mazungumzo na Papa ms...
-
Mpendwa mwana wa Mungu, leo tunasherehekea na kushangilia sherehe ya familia Takatifu. Masiha amezaliwa ndani ya familia hii....
-
Ndege iliyokuwa imetekwa Rubani msaidizi wa ndege ya abiria ya shir...
-
Na Dina Ismail, Dar es Salaam MSANII wa muziki wa asili nchini, Pascal linda maarufu kama Batarokota amewaomba mashabiki wa muziki nc...
St. Joseph yakumbuka watoto yatima
na Paskal Linda-Dar es salaam
SHULE ya Msingi St. Joseph iliyopo Mbezi Beach, Dar es Salaam, kwa kushirikiana na wazazi wa wanafunzi wa shule hiyo, imetoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa kituo cha kulelea watoto yatima cha Mwandalwa kilichopo Mbweni Vijibweni, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Msaada huo wenye thamani ya sh milioni tatu uliotolewa kwa watoto 92 wanaolelewa na kituo hicho, ni chakula, sabuni, sukari, vinywaji baridi, mafuta ya kupikia na nguo.
Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji wa msaada huo juzi, Mkurugenzi wa shule hiyo, Christa Rweyemamu, alisema uamuzi wa kusaidia kituo hicho ulifikiwa kupitia kitengo cha klabu ya huduma ya jamii ya shule hiyo na kuwashirikisha wazazi.
“Tulishirikisha wazazi ambao waliitikia kwa moyo mmoja na tukafikia mchango wa vifaa hivi na fedha taslimu sh 600,000 ambazo zitasaidia kulipia ada za watoto,” alisema.
Akitoa shukrani, mmiliki wa kituo hicho, Halima Mpeta, alisema wamefarijika na msaada kwa watoto hao ambao umetokana na ushawishi wa watoto wenzao
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni