SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limeihamisha mechi ya kuwania tiketi ya fainali za Kombe la Dunia kwa wanawake wenye umri chini ya miaka 20 kati ya Tanzania ‘Tanzanite’ na Afrika Kusini ‘Amajita’ kutoka Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza hadi Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Tanzanite inajiandaa kuikaribisha Amajita Desemba 7 katika mechi ya kwanza ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia zitakazopigwa mwakani nchini Canada, baada ya kuwang’oa Msumbiji kwa jumla ya mabao 15-1.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Saad Kawemba kwa niaba ya ofisa habari, shirikisho lake limeamua kufanya mabadiliko ya uwanja kutokana na CCM Kirumba kutokuwa na ubora stahili.
Kawemba alisema licha ya jitihada zilizofanyika katika kuufanyia marekebisho, bado jaribio la kuwahi muda sahihi kuelekea mechi hiyo haliwezi kuzaa matunda, kutokana na ubovu wa vyumba vya kuvalia na miundombinu.
“Tunaposema vyumba vya kuvalia tunajumuisha vyoo, bafu na sehemu ya kupumzikia wachezaji. Hali katika vyumba vya Kirumba ni mbaya ikiwamo ukosefu wa umeme na aina ya matangazo yasiyohitajika kwa mechi rasmi kutokana na sababu za kiudhamini,” alisema Kawemba.
Aliwataka wakazi wa Kanda ya Ziwa kuwa wavumilivu kutokana na uamuzi huo wa TFF, huku akiwataka kuvuta subira kwani safari ya Tanzanite ni ndefu na kama itafanikiwa kukitoa kikosi cha Amajita, wanaweza kurejea huko kwa mechi zijazo.
“Kama itafanikiwa kuitoa Afrika Kusini, Tanzanite itaingia raundi ya tatu na ya mwisho, wakati huo naamini maboresho Kirumba yatakuwa yamefikia pazuri, hivyo tunaweza kurejea Mwanza kwa mechi ya nyumbani,” alisisitiza Kawemba.
Amajita inayonolewa na Maqsood Chenia, ilitinga raundi ya pili baada ya kuwang’oa vijana wenzao wa Botswana kwa mabao 7-2.
Timu mbili kutoka Afrika zitafuzu kwa fainali za Dunia, zitakazofanyika mwakani kuanzia Agosti 5 hadi 24.
Week Hot newz
-
SIKU moja baada ya kifo cha Rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, Mzee Nelson Mandela (95), mazishi yake yanatarajiwa kufanyika wiki m...
-
Baba Mtakatifu Francisko katika tafakari yake kwa Jumapili ya tatu ya Kipindi cha Majilio, anawaalika waamini na watu wote wenye mapenzi ...
-
Na Paskal Linda,Vatican. 19/12/2013 Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 18 Desemba 2013 amefanya mazungumzo na Papa ms...
-
Mpendwa mwana wa Mungu, leo tunasherehekea na kushangilia sherehe ya familia Takatifu. Masiha amezaliwa ndani ya familia hii....
-
Ndege iliyokuwa imetekwa Rubani msaidizi wa ndege ya abiria ya shir...
-
Na Dina Ismail, Dar es Salaam MSANII wa muziki wa asili nchini, Pascal linda maarufu kama Batarokota amewaomba mashabiki wa muziki nc...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni