Week Hot newz
-
Tunaendelea kama kawaida katika kipindi chetu, tafakari masomo Dominika, na leo tunatafakari masomo Dominika ya 33 ya mwaka C wa Kanisa...
-
Teach me, Lord Jesus, to be generous: to serve You as You deserve; to give, not counting the cost; to fight, not heeding the wound...
-
Uchunguzi wa mwili wa Askofu Józef Wesolowski, umekamilika na matokeo kwamba amekufa kifo cha kawaida. Kuf...
-
Baraza la Kipapa la Elimu Katoliki limezindua tovuti yake inayotoa habari muhimu kuhusu mchango wa Kanisa Katoliki katika sekta ya elimu ...
-
Reading 1, Romans 6:19-23 19 I am putting it in human terms because...
-
NA OSCAR ASSENGA, TANGA-Tanzania.Gazeti Mtanzania. KATIBU wa Chama cha Watu Wenye Albino Mkoa wa Tanga (TAS), Mah...
-
Mpendwa mwana wa Mungu, tuko tena pamoja katika ile habari ya furaha ndiyo kushirikishana mapendo ya Mungu kwa njia ya meza y...
TANZIA:Askofu John Simalenga afariki dunia!
Kanisa la Anglikani Tanzania limepata pigo la kufiwa na Askofu John Simalenga (60) wa Dayosisi South West Tanganyika iliyopo Njombe, Mkoani Iringa. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma Katibu mkuu wa Kanisa Anglikani Tanzania Canoni Dk. Dickson Chilongani alisema kuwa Kanisa limepata pigo kubwa kutokana na kifo cha Askofu Simalenga ambaye aliugua kwa muda mfupi.
Alieleza kuwa kifo cha Askofu Simalenga kimetokea Novemba, 24, 20013 muda mfupi baada ya kuruhusiwa kutoakatika hospitaliya ya kanisa hilo iliyopo Njombe. Alisema kuwa askofu alianza kuumwa alikwenda hospitali kwa ajili ya kupima afya yake na alipofika hospitali ilibainika kuwa alikuwa na maralia pamoja na sukari kupanda hadi kufikia 30 huku shinikizo la moyo kuwa juu.
Canon Dk. Chilongani alisema kuwa baada ya madaktari kubaini kwamba Askofu anasumbuliwa na matatizo hayo alipewa dawa na kuruhusiwa kwenda nyumbani wakitegemea kuwa dawa hizo zingemsaidia kutuliza magonjwa ambayo alibainika kuwa nayo. Alisema kinyume na matarajio ya madaktari, Askofu Simalenga baada ya kurudi nyumbani hali ilibadilika ghafla na kufariki dunia majira ya saa 11 alfajiri.
Marehemu Askofu John Simalenga alizaliwa tarehe 30 Novemba 1953 na kufariki dunia tarehe 24 Novemba 2013. Alisema Kanisa Anglikani linaendelea na taratibu za maandali ya utaratibu wa mazishi ya mwili wa askofu huyo ikiwa ni pamoja na kuendelea kutoa taarifa kwa wachungaji pamoja na viongozi mbalimbali wa dini na Serikali.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni