Week Hot newz

Rage awarejesha Kibadeni, Julio Simba


KIbadeni na Julio 



MWENYEKITI wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, ameendelea kuonyesha makucha yake baada ya kuamua kuwarudisha kazini makocha Abdallah ‘King’ Kibadeni na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ambao walitoswa na Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo.
Akizungumza na wanachama wa klabu hiyo juzi jijini Dar es Salaam, Rage aliwaambia kuwa Kibadeni bado ni kocha wao mkuu halali anayesaidiwa na Julio.
Alisema uamuzi wa kumuachisha kazi kocha huyo, ulitolewa kinyume cha taratibu, hivyo haoni sababu za msingi zinazomnyima haki Kibadeni kuwa kocha wa Simba.
“Kocha wa Simba bado ni Kibadeni kwa mujibu wa mikataba yetu na hatuna mpango wa kuleta kocha mwingine,” alisema Rage huku akiingia ndani ya gari iliyokuwa ikimsubiri nje ya jengo la ofisi za makao makuu ya Simba.
Rage alibainisha kuwa amewarudisha Kibadeni na Julio ambao alidai wataendelea na kazi kama kawaida bila kupingwa na mtu.

Novemba 18, Kamati ya Utendaji ya Simba chini ya Kaimu Makamu Mwenyekiti, Joseph Itang’are, ilimsimamisha Rage kwa madai ya kukosa uadilifu na kupoteza imani naye na kuwatosa Kibadeni na Julio baada ya kupitia ripoti ya Kamati ya Ufundi.
Hata hivyo, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limemwagiza Rage aitishe mkutano mkuu wa dharura ndani ya siku 14 ili kujadili mtafaruku huo ulioibuka ndani ya klabu hiyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni