Papa amesema Ukristu ni maisha ya mwanafunzi , kuliko maisha ya utafiti. Mkristu kuujua ukweli wa Yesu ni nani kwake, ni kuingia katika hija na kufuata nyayo za Mwalimu wa ushuhuda wazi , na uvumilivu katika yote, usaliti , udhoofu wa mwili na kupita katika mashinikizo mapya yenye mikingamo mikali. Papa Francisko alieleza na kutoa mfano wa Petro , ambaye katika Injili ya siku ilimwonyesha yote kwa wakati mmoja, kama shahidi shupavu , anayejibu maswali ya Yesu kwa Mitume , “Na ninyi je, mnasema mimi ni kwenu”? akijibu "Wewe ni Kristo" , na mara baadaye akawa kinyume chake, akamkana kama adui , na mara akipatwa na aibu , akaona anahitaji kukutana tena na Yesu, ambaye alikuwa tu ametangaz a mateso na kifo na ufufuko wake. Papa aliasa, mara nyingi ,Yesu anarudi kwetu na kutuuliza , “Mimi ni nani kwako” na tunampa jibu kama hilo la Petro, , Jibu tulilojifunza wakati wa Kateksimu , lakini jibu hilo halitoshi.
Papa aliendelea kufafanua kwamba, inaonekana kutoa jibu katika swali hilo tunaliliosikia ndani ya mioyo yetu , Yesu ni Nani kwatu, kwa yale ambayo tumeyasikia na kujifunza haitoshi. Wala kusoma na kuelewa peke yake haitoshi . Kumjua Yesu kweli , ni kutembea na Yesu katika njia yake, kama Mtume Petro alivyofanya ,baada ya kumkana, aliuona ukweli wa Yesu ni nani na kubadili mwenendeno wake . Petro alikwenda mbele na Yesu,alizona ishara alizofanya, aliona nguvu za Yesu, na kumkiri kuw andiye Kristu.
Petro , Papa Francisko aliendelea, aliomba msamaha kwa Yesu - na bado, baada ya ufufuo, aliulizwa na Yesu mara tatu katika mwambao wa ziwa Tiberia : " Wanipenda ?". Pengine, Papa alisema ,Yesu alitaka kuthibitisha upendo kamili wa Petro kwa Bwana wake , Petro alitokwa namachozi na kuona ea aibu wakati alipomkana mara tatu wakati wa mateso yake.
Papa anasema , ni kukutana kila siku na Bwana, kila siku ni kumshudia ushindi wetu na udhaifu wetu." Lakini , safari hii hatuwezi kuifanya wenyewe, tunamhitaji Roho Mtaktifu , aingilie kati , kama jambo muhimu.
Papa amehimiza, kumjua Yesu ni zawadi itokayo kwa Baba , ni Yeye anaye tufanikisha kumjua Yesu. Ni kazi ya Roho Mtakatifu, anaye fanya kazi hii kubwa. Hizi si kama juhudi za kibiashara au mashirikisho ya wafanyakazi , lakini ni Roho Mtakatifu, Mfanyakazi hodari ambaye daima huifanya kazi yake . Huifanya kazi hii ya kueleza fumbo la Yesu na kutupatia sisi maana ya Yesu ni nani kwetu. Papa aliomba tuyaweke mawazo yetu wakati ule wa Yesu akiwauliza mitume wake , Petro , Mitume ,tulisikie swali hilo a ndani ya mioyo yetu, “ Mimi ni nani kwako”? Na kama wafuasi wake na tumwomba Baba atujalie sisi sote, kumjua Kristo katika Roho Mtakatifu, ambaye atatupa jibu , la siri huu kuu , Yesu ni nai kwetu. .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni